Naombeni CV ya Kapteni Komba, wa TOT

Ningekuelewa kama ungesema kagombee kule! Bila attachment na mafisadi wa CCM na lichama lao. Thanks kwa kuhisi naweza leta mabadiliko kule....

Mpwa ile kesi ya Mtikila ya mgombea binafsi vp ilikwendaje vile maana nimesha poteza CD yake kabisa
 
Josh Michael,

Li-CV la Major Komba ndilo hilo hapo.

Ukijumlisha Diploma tatu na Cerificate moja (2+2+2+1) na uzoefu nadhani yupo katika kiwango sahihi?
Hahaha, Hawa ndio Wanasiasa wetu tulio nao Tanzania na na wengi wao ndio wanatupangia maisha yetu
 
Mpwa watu wa Mbinga ni ovyo ovyo sana kama Mbunge wao Komba John. Unategemea jimbo litatoka vipi, jamaa huwa amelala bungeni kila siku? Kahawa na mazao yao ya biashara nani atawatetea? Kulingana na sensa ya 2002 mbinga ina wananchi 404,799...kati ya wote hawa John Komba ndiye bora zaidi na mwenye upeo!

Kazi kwelikweli,wakati wenzie wanatetea maendeleo ya majimbo yao yeye anafikiria mistari ya kampeni za uchaguzi wa 2010. LOL!!!
 
Hilo linakushangaza nini mkuu? Hayo ndo mambo ya CCM. Kina Hadija Kopa, Asha Baraka na yule mzee wa maigizo nshasahau jina lake (nadhani mzee Jongo) wote ni vigogo wa CCM. Wajumbe wa NEC. CCM Tambarare

Umemsahau mmoja hapo...ze Kanumba from saus afrika.
 
Hahaha unanichekesha sana, Sasa Kama na wewe utakuja kumchagua tena mtu kama huyu itakuaje?? hivyo watu wa Mbinga inabidi waje watueleze hapa, Je huyu jamaa alikuwa anapambanishwa na nani??
 
Diploma ya miaka miwili? Ujerumani , na alisoma kwa lugha gani?. Lugha tuu inachukuwa zaidi ya miezi sita
 
Diploma ya miaka miwili? Ujerumani , na alisoma kwa lugha gani?. Lugha tuu inachukuwa zaidi ya miezi sita

Hujui kuwa yeye ni msanii?
Atakuwa alisoma kisanii zaidi bila shaka. Atakuwa alipiga Dip ya mazoezi ya viungo.
 
Hujui kuwa yeye ni msanii?
Atakuwa alisoma kisanii zaidi bila shaka. Atakuwa alipiga Dip ya mazoezi ya viungo.

Si kweli aliisha wahi ingia darasani! Alete chuo tufatilie ...alikuwa anacheza ngoma na kuimba kwenye matamasha!
 
Si kweli aliisha wahi ingia darasani! Alete chuo tufatilie ...alikuwa anacheza ngoma na kuimba kwenye matamasha!
Kweli Wanasiasa wetu wa Tanzania ni Balaa tupu.. hivi hakuna watu wengine walio kuwa kamili lakini ni chuo gani alisoma ujerumani kama sio usanii huo jamani
 
Si kweli aliisha wahi ingia darasani! Alete chuo tufatilie ...alikuwa anacheza ngoma na kuimba kwenye matamasha!

Hahahaha ndo maana nakwambia alikuwa anasoma dip ya mazoezi moja wapo ni kuzungusha kiuno si unajua yule ni mwimbaji>?
 
Na mengine ni diploma ya kuzomea wakati wa kampeni. Sasa Kitengo cha Bunge hakina Idara maalumu kwa ajili ya kucheki kama kweli watu wamesoma katika idara husika
 
Na mengine ni diploma ya kuzomea wakati wa kampeni. Sasa Kitengo cha Bunge hakina Idara maalumu kwa ajili ya kucheki kama kweli watu wamesoma katika idara husika

Hahahaha nimecheka hiyo Dip ya kuzomea kwenye kampeni dah!!!
Bunge wakianza kuchambua vyeti hivyo si watanasa wabunge kibao na kufanya CCM waaibike hawataweza fanya hivyo.
 
Maana kuzomea kuzomea ndio na kutunga nyimbo za Kampeni maana ndio fani yake
 
Kama haikwisha si unajua katiba yetu Kimeo!

Hapana, haijaisha. Serikali ilikata rufaa kupinga hukumu ya mahakama kuu. Lakini nasikia ni shinikizo la Mkuu na CCM. Wanaogopa kukumbana na watu ambao wako CCM kwa sababu hawana pa kukimbilia na hawataki kuonekana wabaya kwa kujiunga na wapiganaji wa kambi ya upinzani. Pia CCM inaongopa kupoteza wabunge wengi ambao wanainigia bungeni kwa juhudi zao binafsi bila msaada wa chama; hata kama inasemekana kiasi kikubwa kati ya zile 40bn za Kagoda zilipelekwa CCM.
 
Hii mkuu alikuwa mwalimu wa UPE {Ualimu Pasipo Elimu} au nimeshindwa kuelewa hapo.

waalimu wa UPE walikuwa darasa la saba leavers, huyu alimaliza form four kisha akaenda Kleruu kwa training course ya miaka miwili na kupata certificate grade III.

zamani walimu wa shule za msingi walikuwa ni grade IIIA na IIIB. nadhani IIIA ni form four leavers na IIIB ndiyo UPE(naomba mnisahihishe kama nimekosea)
 
zamani walimu wa shule za msingi walikuwa ni grade IIIA na IIIB. nadhani IIIA ni form four leavers na IIIB ndiyo UPE(naomba mnisahihishe kama nimekosea)

Upo sahihi hujakosea mkuu.
Lakini huko Ugerman haileweki kozi gani alichukua.
 
Back
Top Bottom