Naomba utaalam wa kupika chai

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,485
54,855
Naomba nifundishwe kupika chai. nahita nijuie kupika kila aina ya chai. iwe ya rangi au maziwa. vilevile nahitaji kujua viungo vinavyo hitajika. ni hayo tu. mia
 
chai haipikwi ina chemshwa kama unataka kuchemsha chai ya rangi:-

Maji 1/2 lita
Sukari saizi unayotaka
Michaichai kiasi unachohitaji wewe
Tangawizi iliyokwanguliwa vijiko vya chakula 3
Iriki vijiko vya kula 2

Jinsi ya kuandaa

Chemsha maji kisha tia vitu vyote isipokuwa sukari kwani kila mtu anatumia anavyojisikia mtumiaji. Chemsha kwa dk 15 tayari kwa kunywa..

Cheers :coffee:
 
Chai ya rangi: Chemsha maji kwa kiasi utakacho. Wkt maji yanachemka, tia viungo [(h)iliki, mdalasini, tangawizi -- angalia maelezo hapa chini]. Acha viungo vichanganyike na maji yachemkayo kwa km dkk 10-15. Sasa unaweza kuweka sukari ukipenda. Tia majani ya chai kidogo na acha yachanganyike na maji yachemkayo kwa km dkk 10 -- usiwache majani yachemkie kwa muda mrefu; chai inaweza kuwa chungu. Chai yako iko tayari kunywewa.

Chai ya maziwa: Ni vema kuanza kwa maji kiasi kidogo, km ktk chai ya rangi. Tia maziwa baada ya viungo kuchemkia ktk maji. Hatua nyingine ni km ktk chai ya rangi hapo juu.

Maelezo Khs Viungo:

(h)iliki - Menya maganda. Weka mbegu ktk kipande cha karatasi/kitambaa safi kisha zitwange.

tangawizi - Mbichi ni bora kuliko ya unga. Isafishe tangawizi, menya maganda kwa wembamba au para kwa kisu. Isage tangawizi ktk kiparuzio (grater). Kiasi cha tangawizi unachoweka ktk maji yachemkayo kinategemea kiasi cha ukali unachokihitaji -- kiasi kikubwa, ukali zaidi. Kumbuka pia, muda mrefu wa kuchemkia tangawizi huchangia kuongeza ukali.

mdalasini - Ni vema kuutwanga kuliko kuuweka mzima mzima. Mdalasini mzima ni bora kuliko wa uliokwishatwangwa -- Ni vema uutwange wewe mwenyewe.

Nasubiri feedback.
 
kumbe chai naho inautalam wacha nijaribu kumpikia my wife kesho.
jf ni kilakitu nizaidi ya darasa.mia
 
But angalia asije akazoea tu ila kumsaidia ni poa sana na sisi wanaume tukipika tu ujue utasifiwa miaka mia..
 
Chemsha maji yapate moto kisha weka kwenye kikombe halafu chukua majani ya pakti tia ndani ya kikombe chako chenye maji moto, ongeza sukari saizi yako kisha koroga..
Kwisha.....
 
Umenichekesha kwa hiyo "Kwisha". Hii ni chai ya maofisini.
 
Usiweke viungo kwenye chai wakati ipo jikoni harufu inapungua, fanya hivi.....
Twanga viungo vyako, inaweza kuwa iliki na mdalasini, vitwange vizuri kisha viweke kwenye chupa ya chai, chai ikichemka weka kwenye chupa funika.... Aseee inanukia hatareee
 
Asante kwa elimu, mimi huweka mwanzo nikidhani vitanukia sana, nimejifunza
 
Twanga viungo vyako, inaweza kuwa iliki na mdalasini, vitwange vizuri kisha viweke kwenye chupa ya chai, chai ikichemka weka kwenye chupa funika.... Aseee inanukia hatareee
Hii nitafanyia kazi kuanzia leo!!
1667356014303.png

=
Chai ni kinywaji bora zaiddi kwangu.
 
Usiweke viungo kwenye chai wakati ipo jikoni harufu inapungua, fanya hivi.....
Twanga viungo vyako, inaweza kuwa iliki na mdalasini, vitwange vizuri kisha viweke kwenye chupa ya chai, chai ikichemka weka kwenye chupa funika.... Aseee inanukia hatareee
Wengine hatutumii majani ya chai, kwahiyo hapo unachemsha maji tu, si ndio?
 
Kama ni chai tu tafuta majani ya chai chemsha maji yatie humo ,utapata chai , ila kama ni mapishi ya vifungua vinywa vingne kama tangawiz kahawa na nk utapata wataalamu apa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom