Naomba ushauri wenu wana jf plz

frank lujaju

Member
Aug 21, 2011
58
4
Ni mwaka mmoja sasa tangu tuhitarifiane na mpenzi wangu wa awali ,sababu ya mimi na yeye kukwaruzana na kuachana ni pale nilipohitaji kujua ukweli wa jambo fulani baada ya kulisikia,lakini matokeo yake akaamua kunitext kwamba nimuache aendelee na masomo yake na she will not care about what I will think on her,na mm wala sikuchukua muda nikamwambia ok tanx,kwakuwa unataka concetration ktk masomo ok go.Lakini kiukweli sikuwa sawa kwa takribani mwezi mzima na kibaya zidi nililia mbele ya Mama,ambaye pia alimfahamu huyu binti coz hadi home alishafika,mama akaniambie muche utapata mwingine.Tulikuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miezi Minane she was da first to me.baada ya miezi kama miwili kanifuata kazini cku ya jmosi eti akiomba msamaha nikamwambie nimekusamehe but kiukweli nilikuwa sijamsamehe coz nilitaka tu aondoke fasta.Sikuwa tena na hamu naye sms zake ckutaka hata kuwa nazijibu,ikawa inamuuma sana akagundua kuwa msamaha wangu ulikuwa fake,basi mwaka huu nikaamua kuchukua hamsini zangu na kutafuta penzi lingine na sasa niko kwenye mahusiano mapya kwa takribani miezi minane na nusu na mtu mwingine.Kilicho nishangaza tena mwezi ulio pita mpenz wa zamani karudi tena mara ya pili kuniomba msamaha,na anajutia kosa na alinitumia sms ya mm na yy kuachana coz alipanic coz baba yake alikuwa mgonjwa na mm nikawa namchanganyia stori zisizo za ukweli,na anaomba tuwe marafiki mm nilikubali kutoka moyoni kwamba nimemsamehe ila hajui kama niko kwenye penzi jipya na sitaki kumuumiza mwenzangu,ila kumchana laivu namuurumia coz yuko mwishoni mwishoni mwa elimu yake naogopa ataharibu,mpenzi wangu mpya kila inshu kuhusu mpenzi wa zamani anazijua,sijuhi sasa nifanyeje kumuweka wazi huyu wa zamani,ushauri pliiiiiiiiiiiiiz,
 
Kama unataka afanye vizuri kwenye masomo yake, mridhishe kuwa umemsamehe, na akitaka ule mzigo powa kula. hawa wanawake huwa wanakuwa na maamuzi yanayotokana na future ya hapa isiyoona mbali na leo anajuta. Hakikisha unacheza kama pele kuwa hata huyo mpenzi wako mpya hata sanda kitu chochote. Na wewe inaonekana una kichwa chepesi. haukutakiwa kumtafuta mwingine haraka haraka.
Hata hivyo na wewe umefanya makosa, hukuwa mvumilivu pale mahusiano yalipovurugika ulitakiwa ucomfirm kuwa yule demu hakutaki. matokeo yake ukakurupuka kuchukua mtoto wa watu sasa unataka kumwumiza kwa kutokuwa mvumilivu.
Ilitakiwa ukae naye mezani ili mjadili mustakbali wa mahusiano yenu, kama haeleweki unamweleza wazi kuwa sasa mimi natafuta chombo kingine.
Kwa sasa itakuwia ngumu kuhakikisha kuwa hawatajuana. labda ucheze pele.
 
mmmmmh Asante MUNGI ni kweli uvumilivu ckuwa nao,ila cwez fanyakosa tena dis time,upele unatakiwa ila duuu kazi kweli kweli
 
Ulimwaga machozi mbele ya mama!!!!Aisee!Any way,,tambua kwamba ukweli ni silaha muhimu kuliko hata bomu la maangamizi.Ukweli ndio utakaowaweka kwenye mstari wa salama na amani wote,yaani wewe,mpya na wazamani.Tafuta wakati mwafaka umwambie ukweli huyo wa zamani ili ajue kwamba kwa sasa ni TOO LATE.Kesi ndogo sana hiyo.
 
Kila kinachoendelea baina yangu na wa zamani ni lazima nikiweke wazi kwa mpya sitaki unekani play boy
 
Sa na wewe mbaba mzima unadate na vitoto vya secondary mkuu,dah!!ila nakushauri ucmwambie chochote kwa sasa hadi amelize mtihan wake.
 
mapenzi uanzia mbali na kikubwa malengo bac na kuangalia mbele,ok kikubwa ushauri wako,nimekusoma
 
Ukimwambia huwezi kua nae sababu una mpenzi mngine ataumia, ila ukimficha na aje agundue mwenyewe ataumia zaidi. Bora umwambie mapema, utakua umemtendea haki hata huyo mpenzi wako wa sasa, who should be your priority.
 
kwanza nimependa avatar yako,bila shaka ni wewe na pia jina ni lako,u-mkweli kiaina!mpe msamaha feki halafu akimaliza masomo yake mchane laivu,ndio akome as long as huyo ulie nae mnaenda bila shida na umeridhika nae!
 
Kila kinachoendelea baina yangu na wa zamani ni lazima nikiweke wazi kwa mpya sitaki unekani play boy

Huyo mpya kama utamweleza kuhusu mawasiliano yako na yule wa zamani huoni kuwa utaingia kwenye matatizo? There will be a very big impact believe me. Huyo mpya unaweza kumweleza kila kitu kuhusu huyo, na hujui atakavyopokea. Matokeo yake ni kwamba huyo mpya anaweza kutafuta means ya kumtafuta huyo wa zamani mambo yakawa hadharani, akaja kujua una mwingine. Utakuwa hujamsaidia kwa masomo yake. Na wewe acha kufanya ngono na watoto wa sec.
 
we mwmbie tu ukweli,alipokuwa anakuacha alikuwa hajui inakuuma?inawezekana kaachwa halafu anakuja tena kwako.
halafu nina mashaka maana hutaki kusema kwanini alikuacha,inaonekana labda we ndo una makosa
 
ok nikweli juu ya ulisemalo,lakini huyu mpya nampenda sana dats y namueleza kila kitu kuhusu wa zamani ila baadae isionekana nilikuwa namzunguka.Ebwana MUNGU sikuwa kingono kwa huyo wa zamani nilikuwa na malengo naye,hatukuwahi kusex kwa kipindi chote tulipo kuwa kwenye mahusiano,licha ya kwamba nilikuwa nikimgusia na anatoa nje,coz nilikuwa na malengo naye nikawa napotezea,kwao nilienda na kwetu kaja u daaaaaah inauma lakini muda alionipotezea jamani na mambo niliyomfanyia aisee
 
Back
Top Bottom