Naomba ushauri wenu ndugu zanguni

unlucky

Senior Member
Aug 9, 2011
199
56
mimi nina mume wangu niko nae leo miaka sita na nimezaa nae watoto watatu lakini tatizo ni kwamba mume ananitesa sana ananipiga hata nikiwa na mimba ya miezi 8,na pili ni malaya sana anaenda nje kila siku anabadilisha wanawake analala nje siku zingine ndani hakai hata kukaa na mimi kuongea hana mda yeye anakuja humu ndani kama gesti analala masaa 4 tu nakuondoka ananiambia mie mfanyakazi tu wa kulea watoto wakiwa wakubwa atawachukua na mie kuniacha,naomba mnipe ushauri nifanyeje niendelee kuvumilia mateso au...??
 
kweli wewe ndio unlucky,..yaani mumeo umezaa nae watoto watatu wakati hakupendi na mateso juu,....anyway piga moyo konde siku yataisha_ingawa ni ngumu kumeza
 
Unaweza kupoteza maisha kwa hyo ndoa ndugu.je umeshajaribu kufanya jitihada zozote za kujaribu kumfanya arudi ktk hali yake ya awali mlipoanza mahusiano?ni hatua gani ulifanya?
 
vunja ndoa?
, au ni handsome sana, au ana hela sana?
, au hujawahi kusikia kuwa kuna ndoa ziliwahi kuvunjika?
, au unaogopa malezi ya watu?
, au hujui kuwa mungu yuko na wewe?
 
Hapana usiendelee kuvumilia mateso ya namna hiyo labda kuwe na sababu ya msingi inayomfanya akuadhibu mara kwa mara sawa. Lakini kama anakunyanyasa bila sababu ni bora ukae naye chini na jaribuni kuzungumza namna ya kumaliza tatizo hili. Ikishindikana waweza chukua hatua ya kwenda mbele zaidi kuomba ushauri mfano kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.
 
endelea kuishi na huyo mumeo mpaka akuvunje kiuno ndo utaijua njia ya kwenu. msiwe waoga wa maisha simama tetea uhai wako kwa ajili ya wanao. move on kahangaike na maisha na ukimtanguliza MUNGU utafanyikiwa.
 
Nakushauri akikupiga bila sababu mpeleke polisi, huu anaofanya ni unyanyasaji mkubwa!
Au waambie kaka zako waje kumshushia kichapo cha nguvu then una achana nae na mali zote mlizochuma mtagawana kwa mujibu wa mahakama!
Usikubalh kuteseka kiasi hicho the anakuita mfanyakaz wa kule watoto!
 
Hv kweli kama ndiivo hvo muda wote wangojea nini jehanamu au Musa afufuke kutoka kwa wafu ndo uondoke kwenda nchi ya ahadi? Wewe timuuuuuuua sasa !!
 
Hii hadithi imefanan na ya dadangu kipenzi (RIP).
Aliolewa na mwanaume asiyejua thamani ya mke, akamtesa kwa vipigo, akaleta wanawake hadi ndani, dada alivumilia yote. But guess what, mwisho wa siku alimuua.

Fundisho, mateso hayavumiliki, jaribu kujipenda ndio umpende mwenzio, ndo maana hata maandiko yanasema mpende jirani kama unavyojipenda. sasa wewe naona hujipendi. Take action mapema kabla haujuuawa na kuwaacha wanao wakiteseka
 
id yako inakuwakilisha...kwanza pole sana na chukua tahadhari mapema..anakuja kwa sababu kuna mfanyakazi nyumbani, siku akija akakukosa(mfanyakazi) ndo atajua umuhimu wa kuwa na mfanyakazi kama wewe kama anavyokuita. hana huruma huyo mwanaume na hafai kwenye jamii.
 
duh!!polee...huyo mwanaume wako inaonekana una mpenda kupitilizaa,yani wee kakuzalishaa watatu,kichapoo ana kupaa,nyumbanii halalii,tenaa kichechee mweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.ungekuwaa dadaa angu ninge kushushia kichapo nikurudishe home na wajombaa zangu nileee.ukionaa vipi mkorongeee sumuuuu afe
 
Kuna majirani zangu walikuwa na dada yao wa pekee. Dada kaolewa na wakajenga nyumba si mbali na kwao. Mumewe (anatokea kabila linalosifiwa kwa kutoa kichapo) alikuwa anampiga now and then. Kaka zake(mashemejize) kuna siku walimtolea uvivu walimtandika kijana mpaka naolewa sikuwahi kusikia tena jamaa kampiga mkewe. Maana ilikuwa akianza kumpiga majirani mtasema kuna msiba. Huyu mumeo anahitaji kichapo tu huna kaka wewe???
 
Kuna majirani zangu walikuwa na dada yao wa pekee.&nbsp; Dada kaolewa na wakajenga nyumba si mbali na kwao.&nbsp; Mumewe (anatokea kabila linalosifiwa kwa kutoa kichapo) alikuwa anampiga now and then.&nbsp; Kaka zake(mashemejize) kuna siku walimtolea uvivu walimtandika kijana mpaka naolewa sikuwahi kusikia tena jamaa kampiga mkewe.&nbsp; Maana ilikuwa akianza kumpiga majirani mtasema kuna msiba.&nbsp; Huyu mumeo anahitaji kichapo tu huna kaka wewe???&nbsp; <BR>
 
1.Siku nyingine akikupiga mpeleke polisi,hakika hatarudia tena.
2.Kuhusu watoto mwache awachukue kwani wew utaendelea kuwa mama yao tu.
3.Jiamini kwamba wewe una thamani kubwa hapa duniani kama yeye hakupendi basi Mungu anakupenda na kukuthamini sana.
 
........kama ni kweli, unasubiri nini kuondoka? Kapime ngoma kwanza, kama upo fresh kimbia haraka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom