naomba ushauri wa sheria

Ballot

Member
Jan 4, 2012
39
12
mimi ni mtanzania ninaishi botswana'serikali ya nchi hii imeamua kutoa sheria kali kwa wageni wanaofanya kazi na biashara'nina kampuni lakini wamenipa masharti magumu kabisa ya kupata leseni'suluhu ya tatizo hili nimeamua kumkabidhi mwenyeji kampuni yangu kwa kuwa sheria haibani wazawa'
Nimebadilisha share certificate na kila kitu kuhusu kampuni kuwa kwenye jina la huyu mzawa'bank signatory tunasaini wawili'lakini tunaenda kwa mwanasheria wake kufanya makubaliano ya kwamba kampuni ni mali yake ila mimi kuwepo pale ni kwa ajili ya kujenga kampuni na faida yoyote itakayopatikana tunagawana 50/50'naombeni ushauri je
Naweza kuja kudhulumiwa huko mbele?
Je yule mwanasheria anaweza kuandika vitu nisivyojua ili baadaye nishindwe?
 
Umeliwa....RUDI NYUMBANI haraka!!!
Hakuna mkataba halali unaoingiwa kwa udanganyifu ili kuvunja sheria za nchi halafu ukaweza kutambuliwa.
Hii ni sawa na Mzungu mmoja alikuja Tz akanunua ardhi kwa vile sheria hairuhusu mgeni kumiliki ardhi
akaandikisha jina la kimada wake mtanzania na walikubaliana kuwa ardhi hiyo ingebaki kuwa mali ya mgeni japo
jina ni la m bongo. Hata hivyo wakati Mzungu anaondoka alishindwa kuuza ardhi hiyo kwani mahakama ilisema
ardhi hiyo ni mali ya M-bongo hivyo akawa amedhulumiwa....
 
Mia Mkuu

Back
Top Bottom