Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

High Vampire

JF-Expert Member
Nov 17, 2012
2,915
2,083
Naona watu siku hizi magari haya ya Nissani Extrail wananunua sana.

Je, wanajua kuwa ni mabovu na spea zake ghari au hawaambiwi na watu.

1593174620473.png



BAADHI YA MAWAZO YALIYOTOLEWA NA WADAU KUHUSU GARI HII
Sababu za Brand za magari kama NISSAN, MITSUBISHI na Zinginezo kuonekana ni tatizo.

Utalamu wa mafundi wetu na kujua mahitaji ya magari husika upo chini. Haya magari hayataki mafundi ambao ukimpelekea gari anaanza kupiga ramli kujua tatizo linaanzia wapi.

Anaanza kusearch kichwani mwake kwa kutumia akili yake binafsi na sio utaalamu wa kujua mfumo wa gari husika. Hizi gari kwa miaka mingi zimetibiwa magonjwa yake kwa kufanyiwa modification na sio kuadress shida kuu.

Mfano kama mimi niliwahi kuhangaika na Mitsubishi Pajero IO zile ndogo. Kila unapokwenda gereji kila fundi anakuja na ugonjwa wake, ikafikia m'moja akasema kwa gari hiyo nitoe hiyo engine niweke ya Noah, of which ni modification inayowezekana but sikuwa comfortable. So nikapunguza nayo matumizi nikisubiria suluhu hadi nilipowasiliana na jamaa kutoka Japan na akanieleza why hizo gari zikifika nchi za dunia ya tatu kama india na African zinakuwa zinazingua.

Akasema gari ni system.... Na system huwa inakuwa na standard requirements. Na zisipokuwa met basi hiyo gari itaanza leta shida. Akanishauri gari nipate fundi mwenye diagnosis machine, ambayo itaelezea shida gani kwenye mfumo automatically kupitia computer chip iliyo katika gari.

Kwa mfano, kwa hii gari, kwenye mfumo wake wa engine inataka sana mafuta ya premium level. Yaani mafuta ya zile Petrol stations kama Puma, Victoria, Engine, Total na wengineo ambayo hayo mafuta huwa yanasaidia katika uchomaji kwenye engine na kuipa nguvu inayotaka.... Badala ya kuweka haya ya ordinary kama ya Camel, oilcom, na kwengineko.

Kimsingi gari kupitia mfumo wake ikiditect kuna shida kwenye mfumo wake automatically inatengeneza fault ili kuzuia madhara yasisambae. Sasa kwa mbongo wa kawaida akiona gari limejizima tu anasema hizi gari ni mbovu, anapeleka kwa fundi ambaye hazijui anafanya kuotea tu tatizo na mwisho wa siku akiifungua kuna vitu harudishii sawa au anavidisturb kwakusema hiki tukitoe maana ndicho kinazuia gari isirespond kuwaka. Kumbe unatoa kitu ambacho ni muhimu katika kutoa taarifa fulani kwenye sytem ya gari. Sometimes unakuta ni sensors tu zimefeli na inatakiwa kipatikane kile kifaa cha diagnostic kitoe jibu la fasta bila kuhangaika kupiga ramli.

So kwa ushauri wangu ukiwa na magari kama, Nissan Xtrail, Nissan Navara, Pajero zote ndogo na kubwa, Ford, Descovery, BMW, Mercedes, Volkswagen, na kadhalika wewe nenda kwa fundi ambae atafanya diagnosis kupitia kifaa na sio ramli ya kichwa watakuharibia gari na kukuaminisha gari ni mbovu kumbe ni wabovu kwenye kudeal na technology ya magari ya kisasa ambayo mifumo yao inakuwa inarespond pale ikiharibiwa.


Kuna magari ukishaanza kuyaweka mafuta ambayo sio premium utaona linaanza kusumbua kuwaka kumbe system imeshadetect mafuta ya kuchakachua na hivyo inatuma warning signal gari isiendelee kutumika itauwa fuel pump..... So kuweni makini sana na maswala ya modification.

Na kuhusu spear.... Spear zilikuwa ni shida kupata zamani before internet haijawa kila kitu..... Ila kwasasa hiyo shida hakuna tena.... Internet imerahisisha mambo, kwasasa unaweza kufanya manunuzi ya spare kwa kuweka to Serial namba ya spear ya gari yako mzigo ukaletwa ukakufikia na unapata kitu genuine.... Shida ni kwamba wabongo ni waoga wa maisha na tunaishi kwa mazoea.....

Sent using Jamii Forums mobile app
---
Sio kweli.

CHA KWANZA KABISA UMJUE FUNDI ANAEJUA KUTENGENEZA NISSAN XTRAIL NA SIO TAPELI. FUNDI MWENYE UJUZI NA MUELEWA NA SIO MWENYE TAMAA!

Mimi fundi wangu miaka yote ni fundi mmoja anaitwa Deo yuko pale Mwenge alifundishwa na Nissan Wenyewe, yuko karibu na Maryland Bar opposite ITV.

Gari la kwangu nilinunua 2013 na mpaka leo ninalo na nimetembea nalo mikoa mingi sana nchi hii. Tayari tangu nimenunua nimetembea Kilometre 134,000 (nilizotumia mimi) Hili hapa:

Nimetumia magari mengi tangu ninunue gari la kwanza 1998. Nissan X-Trail haijawahi kuni-disapoint hata siku moja! Ni gari durable na comfortable hata ukiwa off road na stable barabarani sana. Nissan X-Trail spare zake ni ghali kidogo na sio kiasi kikubwa kama watu wanavyosema, ila bush, na stabiliser links ambazo ndio unabadilisha zaidi kama ni mtu wa pori kama mimi ukifunga ni mwaka. Spare zake karibu zote ni original. Vitu vikubwa vinavyokufaga na ni mara moja kwa mwaka ni sensors ambazo magari mengi ya siku hizi yanazo, usipoibadili ukaipuuzia basi unaweza kuharibu gari, gari ikaheat au tatizo lingine. Sensor moja inaweza kuwa laki mbili, ila sensor kama ya air filter mara nyingine huhitaji kusafishwa tu na spray maalum.

Muhimu usipitilize service milage, hakikisha unaweka collant na sio maji yako ya Dawasco, engene yake ni high efficient na moderm na ukiona tatizo lolote lile, peleka kwenye computer wa diagnose full stop. Iwe ni miss au engene ina mngurumo wa ajabu. Taa yoyote isiyo ya kawaida ikiwaka kwenye dashboard ni Computer tu ndio itakwambia.

Ujinga wa sisi Waafrika wengi tunataka gari ambalo hata usipofanya servie litakwenda tu na fundi yoyote ukimpa atategeneza. Ukimsikia fundi anakwambia hizi gari mbaya sana kama wanavyosema siku hizi gari za VVTI au D4 ujue huyo mbulula hana shule na hajui kulitengeneza. na ukimwachia atakuharibia gari.

Nissan X-trail haikuwahi kukwama katika tope, sio chini ya mara moja nimeziacha Rav 4, Suzuki Escudor na Hiluz Double cabin porini mimi nikapasua katika tope, vumbi na vichaka na sikupata shida yoyote. Pia clearance yake chini ni nzuri na sio rahisi kugonga.

Zingatia service yake, na ukifunga spare ni mkataba mwaka sio kama Toyota spare bei rahisi lakini utabibadili tu mara kwa mara na hutakumbuka mwisho wa mwaka umeingia gharama kiasi gani.

---
Ndugu nissan xtrail haina shida hata kidogo...hii gari inahitaji kufuata masharti yake elekezi....hii gari inatumia oil ya nissan extrail tu...hivyo watu wengi wanapofanya service huwa wanatumia oil ambayo not recommended kwa xtrail.

But mtu ukitumia oil yake utaifurahia sana hii gari....ni gari nzuri....ni gari ya safari. Tatizo letu Watanzania tunapenda kufanya maamuzi kwa kutumia maneno matupu ya watu. Changamoto ninayoiona kwa extrail ni bei ghari ya vipuli....but vipuli vyake ni imara na original na hudumu muda mrefu
---
Ni kweli, xtrail haziko reliable kabisa kama Toyota. Inaweza kukuharibikia ghafla ukashindwa kujua cha kufanya, na spea zake ni chache sababu nyingi haziingiliani na gari nyingine.

Kimeo kingine ni Nissan Murano. Kama umeshafanya utafiti kidogo wa bei zake kwenye used, zimeshuka saana, sasa hivi ni affordable kwa watu wengi. Ila haziko reliable hasa kwa barabara zetu na mafundi wetu
---
Nimesoma huu Uzi naona kila mmoja anatoa story asieijua. Kwa taarifa yenu hakuna Gari nzuri kama Nissan xtrail. Nimekaa nayo five years, Nina ndugu zangu wanne hazijasumbua.

Kuhusu AC zipo vzr sana kama gx 110 spear so ghali kama watu wanavyotaka kutuaminisha no za kawaida sana. Engine complete used 700 laki sijui kwa mini watu wanapotosha. Kwa safari nni Gari nzuri sana.

Ulaji was Mafuta in mzuri ukilinganishana na SUV nyingine ambazo ni 4WD. Ukitaka detail ya kila spear na being uliza sio kukurupuka na kudanganya umma. Ukiwa na RAV4 kwa mwaka garana za service na Mafuta no kubwa kuliko Xtrail, ninao ushahidi kwa hili

Kuagiza extrail no cheap kuliko RAV4 lakini ushuru was Xtrail no mkubwa kuliko rav4 n.k
---
Nimekaa nayo muda mrefu sana na sijapata tatizo lolote. Nimepiga safari za nje ya nchi kama safari sita kwenda Uganda na Mara nane Congo. Sijapata tatizo lolote. Sasa mtu anapokuja na story nyingine namshangaa.

Oil ya gearboc ni Dx4 smbayo nayo mnaibadilisha kwa makosa. Inabadilishwa baada ya km 130000. Ball joint zipo imara sana zijabadili kiasi kwamba ningekuwa na Toyota ningeisha badili kama mara saba. Ni gari zuri sana.
---
Kiujumla gari za kisasa ambazo sio toyota ni ishu sana. Gari moja ya aina ya Escudo 2006, taa moja ya nyuma ni 900,000 kwa seti! Kama nadanganya aje mtu abishe hapa.

Tuwe makini tu ikiwa huna haja ya fasheni km ww ni 'bora usafiri' tununue ist, starlet,rav4 (<2003) ni magari mengi mno mjini ingawa hayana hadhi kwa sababu ya kuwa km uniform
---
Ukisikiliza sana Watanzania hutanunua hata baiskeli...

Ninashindwa kuelewa kabisa watu wanaegemea wapi..

Watakuambia X trail ni mbovu,

Ukija kwenye Toyota utasikia injini D4 kimeo,

Nilichogundua sisi watanzania hatupendi kubadilika...tunapenda kuwa conservative, kutishana na kuigana.....kwa mfano angalia GX 100 zilivyoingia, watu waliigana wakakimbilia huko karibu wote, Angalia ujio wa IST ,Sasa hivi ni Athletes Crown ndiyo watu wamekimbilia huko...

Point yangu ni nini..?
Hakuna gari bovu (in general conclusion)
Kwa sababu gari linapotengenezwa kiwandani linapitia standards nyingi sana za kimataifa ili kuku balike kuendesheka popote duniani...

Cha ajabu hawa Watanzania wanaosema Nissan X trail na Toyota za D4 engine ni mbovu, watanzania hawa hawa hawana hata technolojia ya kuyengeneza bulbu tu ya gari....kiwanda cha matairi kule Arusha kimewashinda kimekufa....Sijaelewa wanatoa wapi ubavu wa kuikosoa technology ya mjapan...

Ingelikuwa X trail ni mbovu kama madai ya watanzania yanavyodai, nadhani Nissan Motor Cop wangesitisha uzalishaji wa haya magari...

Lakini leo hii X trail ipo generation ya tatu...Ina maana generation ya kwanza ilifanya vizuri, wakaja na generation ya pili ikafanya vizuri, na sasa wapo generation ya tatu....

Watanzania tuna kile kitu cha sizitaki mbichi hizi...

Why x trail na Toyota D4 ni mbovu kwa wabongo tu na siyo huko duniani..?

Majibu..
1...Umasikini.....hali zetu za umasikini hazikidhi sisi kumiliki hayo magari na kuyafurahia...Kipato cha kuunga unga unataka ukae ndani ya x trail au Toyota yenye d4, lazima tu utasingizia hizi gari hazifai kwa sababu huna hela za kufanya service inayokidhi viwango na spea genuine.....Mtu wa namna hii kaa kimya ndani ya starlet, carina, vitz, funcargo, corrola na nyinginezo za jamii hizo.

2..Ufundi...
Nchi yetu bado ina majanga makubwa sana kwa upande wa mafundi waliobobea kwenye brands nje ya Toyota....hawa mafundi ndiyo wamekuwa wapotoshaji wakubwa kuwa Nissan, Mitsubish,Mazda,Subaru, BMW,Aud,Benzi B na Toyota zenye injini ya D4 hazitengenezeki, hazina spea, spea ni ghali(hili nakubaliana nalo lakini ukifunga unasahau..)
Unakuta fundi hajui kuandika jina lake vizuri anaikosoa technology ya mjapani...
Watanzania wengi wamekuwa wakiishi kwa ushauri wa mafundi wa chini ya mwembe mwisho wanapotea..

3..Baadhi ya watu wanapenda kushikiwa akili zao na mafundi wao...

Kwa mfano Nina Nissan ambayo ina bush flan ya wishbone...hii bush inaingiliana na kwenye Nissan March....kuna jamaa nilimkuta kwa fundi kachongesha hii bush, nikamuuliza WHy, akanijibu fundi wangu kasema spea za Nissan hazipatikani na ukipata ni ghali sana....nikambishia kwa sababu huwa ninanunua hizo bush kwa 15000/ kwa moja na zimajaa tele...jamaa yeye alishikilia msimamo wa fundi wake..The hell with him...

Kwa hiyo, tunapojadili magari fulani fulani, kagua mfuko wako, mafundi wako na aina ya service unayofanya...

Usije ukataka kuleta Service ya starlet kwenye X trail, halafu ufikiri X Trail itakuchekea...

Sent using Jamii Forums mobile app
---
Ukisikiliza sana Watanzania hutanunua hata baiskeli...

Ninashindwa kuelewa kabisa watu wanaegemea wapi..

Watakuambia X trail ni mbovu,

Ukija kwenye Toyota utasikia injini D4 kimeo,

Nilichogundua sisi watanzania hatupendi kubadilika...tunapenda kuwa conservative, kutishana na kuigana.....kwa mfano angalia GX 100 zilivyoingia, watu waliigana wakakimbilia huko karibu wote, Angalia ujio wa IST ,Sasa hivi ni Athletes Crown ndiyo watu wamekimbilia huko...

Point yangu ni nini..?
Hakuna gari bovu (in general conclusion)
Kwa sababu gari linapotengenezwa kiwandani linapitia standards nyingi sana za kimataifa ili kuku balike kuendesheka popote duniani...

Cha ajabu hawa Watanzania wanaosema Nissan X trail na Toyota za D4 engine ni mbovu, watanzania hawa hawa hawana hata technolojia ya kuyengeneza bulbu tu ya gari....kiwanda cha matairi kule Arusha kimewashinda kimekufa....Sijaelewa wanatoa wapi ubavu wa kuikosoa technology ya mjapan...

Ingelikuwa X trail ni mbovu kama madai ya watanzania yanavyodai, nadhani Nissan Motor Cop wangesitisha uzalishaji wa haya magari...

Lakini leo hii X trail ipo generation ya tatu...Ina maana generation ya kwanza ilifanya vizuri, wakaja na generation ya pili ikafanya vizuri, na sasa wapo generation ya tatu....

Watanzania tuna kile kitu cha sizitaki mbichi hizi...

Why x trail na Toyota D4 ni mbovu kwa wabongo tu na siyo huko duniani..?

Majibu..
1. Umasikini

hali zetu za umasikini hazikidhi sisi kumiliki hayo magari na kuyafurahia...Kipato cha kuunga unga unataka ukae ndani ya x trail au Toyota yenye d4, lazima tu utasingizia hizi gari hazifai kwa sababu huna hela za kufanya service inayokidhi viwango na spea genuine.....Mtu wa namna hii kaa kimya ndani ya starlet, carina, vitz, funcargo, corrola na nyinginezo za jamii hizo.

2. Ufundi
Nchi yetu bado ina majanga makubwa sana kwa upande wa mafundi waliobobea kwenye brands nje ya Toyota....hawa mafundi ndiyo wamekuwa wapotoshaji wakubwa kuwa Nissan, Mitsubish,Mazda,Subaru, BMW,Aud,Benzi B na Toyota zenye injini ya D4 azitengenezeki, hazina spea, spea ni ghali(hili nakubaliana nalo lakini ukifunga unasahau)
Unakuta fundi hajui kuandika jina lake vizuri anaikosoa technology ya mjapani. Watanzania wengi wamekuwa wakiishi kwa ushauri wa mafundi wa chini ya mwembe mwisho wanapotea.

3. Baadhi ya watu wanapenda kushikiwa akili zao na mafundi wao
Kwa mfano Nina Nissan ambayo ina bush flan ya wishbone...hii bush inaingiliana na kwenye Nissan March....kuna jamaa nilimkuta kwa fundi kachongesha hii bush, nikamuuliza WHy, akanijibu fundi wangu kasema spea za Nissan hazipatikani na ukipata ni ghali sana....nikambishia kwa sababu huwa ninanunua hizo bush kwa 15000/ kwa moja na zimajaa tele...jamaa yeye alishikilia msimamo wa fundi wake..The hell with him...

Kwa hiyo, tunapojadili magari fulani fulani, kagua mfuko wako, mafundi wako na aina ya service unayofanya...

Usije ukataka kuleta Service ya starlet kwenye X trail, halafu ufikiri X Trail itakuchekea...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona watu siku hizi magari haya ya nissani extrail wananunua sana je wanajua kuwa ni mabovu na spea zake ghari au hawaambiwi na watu

Asante High Vampire kwa uzi mzuri.
Naomba nijue ubovu wa hz nissan x-trial.

Binafsi nazipenda coz naona ni gari yenye nafasi sana na je kwa ushauri wako kama nataka kuagiza nikiagiza Voxy au Noah ntakuwa nimecheza vema na opportunity cost (kwa ku forgone xtrial)

Asante.
 
Last edited by a moderator:
Asante High Vampire kwa uzi mzuri.
Naomba nijue ubovu wa hz nissan x-trial.

Binafsi nazipenda coz naona ni gari yenye nafasi sana na je kwa ushauri wako kama nataka kuagiza nikiagiza Voxy au Noah ntakuwa nimecheza vema na opportunity cost (kwa ku forgone xtrial)

Asante.

Kama una hela nunua tu ukiambiwa uagize nairobi unatoa tu ila kama hela za mawenge nunua kampuni ya toyota
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe mkuu haziko vizuri,hata nje wameshusha sana bei ili zitoke ndiyo maana watu wengi wananunua pasipo kujua kuwa ni bei promo..

Hapa mwanza yawekuwa mengi mno najiuliza au spea zimeshuka bei au ndio kutojua tu hatari sana kama hela za kuunga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom