Naomba ushauri;Mke wa mtu anataka nimpe mimba

RPC wa MWANZA ni tukio lilitokea hapa TZ au nchi jirani? Hata redio mkulima huna ukapashwa habari? Inzi anafuata kidonda daima,si kidondo kifuate Inzi.kaa vizuri.
 
lakini haya mambo yapo, yalikuwepo na yatakuwepo! sema tu hapo mtu unakosa uhakika wa ukweli wa jambo la huyo mdada, bt hizi paa zinafunika mengi sana, kuna jamaa pale kijichi ana maisha mazuri sana (nyumba ya kisasa, miradi, mshahara mkubwa, magari) bt wana miaka 18 kwenye ndoa sasa bila kid, tetesi ni kwamba prblm ni mme.
 
Habari zenu wakuu,huyu dada tulifahamiana tukiwa safarini, alinionekana kuwa mcheshi na mkarimu sana kwangu kumbe alikuwa analake,kwakuwa tulikuwa tumekaa siti moja sikusita kuongea nae mawili matatu,baada ya maongezi mengi aliniambia ameolewa ila mpaka sasa hawaja barikiwa mtoto ingawa wameshaangaika hospitalini na kwa waganga wa jadi...Kwa maelezo yake mumewe ndio anatatizo na hospitali ndivyo walivyo ambiwa.
Sasa yeye anasema anahitaji mtoto na amechoka kuishi bila mtoto na Kubwa zaidi anataka kutest kama kweli yeye hanatatizo,Ingawa nimeshauri aendelee kuwa na subra kwan ipo siku Mungu atatenda,ila anasema kama kuvumilia amevumilia sana ila kwa sasa basi....anachotaka yeye ni mimba tu na jumatano hii anakutakuja Dar kwa ajili ya kutekeleza swala hili.
Binafsi mimi nina miaka 26..
Naombeni ushauri wenu je nimtekekezee swala lake ama nimshauri vipi?
hapo pagumu. mimba maana yake ni pekupeku hiyo, sasa sijui.....
Au akija Dar hana pakufikia, anatafuta sehemu ambayo atakula bure na atalala bure na ku-save pesa ya kulala gesti. Style hii ilitumiwa na wamama wa mkoa fulani waliokuwa wanaenda kufanya biashara Uganda, ku-save kwao hela ya ya kula na ya kulala gesti kukasababisha wakarudi na UKIMWI.
Kuwa makini.
 
Wewe una mtoto? Una uhakika gani kama unazaa? Kwa nini asimtafute mtu ambaye angalau ana watoto na ana 30's yrs kwa ajili ya uhakika wa yeye kupewa hiyo mimba? Mfanya biashara amekosa kabisa wafanya biashara wenzie na huko kote anakozunguka?? Mmeshauriana mkapime kwanza?? Kama yeye hana tatizo basi wewe ndo utakuwa una tatizo, maana kwa namna ulivyoliweka ni kama yeye ndo anakuomba, jifikirie kwani kawaomba wangapi wamzalishe?. Mshauri akamtafute mkomavu mwenzie huko. Jistukie then chukua hatua.
 
Mdogo wangu huo ni Mkenge! kisingizio cha Mimba ni gea ya kutaka umtafune peku ili akuachie kale kamdudu! "TAFAKARI, CHUKUA HATUA!"
 
Wewe roho yako inakutuma nn?Kama inakutuma kufanya jst do t,bt kama inakutuma kutofanya leave run away .Mind u ni jaribu ilo.
 
Kati ya watu niliowahi kuwadharau sana, wewe ni number mbili. Can't be serious kuongelea hilo mbele ya watu wenye akili timamu. Is you, yourself and yoursoul kufanyanya maamuzi. Sema jingine acha hizo laana.
 
Hii ni fundisho kwa wanaume wote mlio na wake.
Watimizieni wake zenu vitu wanavyoitaji ipasavyo.
Kuna mdada aliombwa kumegwa nje kwa sababu tuu mme wake hampi kitu kinachopaswa katika sita kwa sita.
 
we dont learn from others mistakes, thats our problem!! udhaifu ume mea sasa!
 
Mke wa mtu ni sumu, katumika weee afu ndo anakutaka wewe,at your age,kuna mdau hapo juu kasema usizoe magundu njiani.kuwa makini na heshimu maisha yako
 
mkuu bado we mdogo sana,una safari ndefu mbele yako,huyo dada kama alichagua kwa makosa mwache alipe deni lake mwenyewe asikuhusishe wewe,fungua macho mjomba
 
Utajisikiaje mtoto wako akilelewa na baba mwingine huku huwezi kusema ni wako wala kumsalimia na isitoshe hata kumuona itakuwa tabu na pia inaweza ikawa chanzo cha yule dada kuachika kwa mume wake na ujue akiachwa anahamishia majeshi kwa baba wa mtoto ambae ni wewe, hivyo sikushauri na hivyo ukifanya jiandae kwa haya yote.
 
Back
Top Bottom