Kubota
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 532
- 1,089
MKuu Ohotaite Kintu, nashukuru kwa ufafanuzi wako. Nami ninauzoefu sana na Kilimo cha nyanya za majira haya! Kwa uzoefu wangu kutokana na maelezo yako hapo juu nakusihi hivi sasa pamoja na kutafuta bei nzuri usikatae bei inayopatikana hapo shambani! Umefanya vema kuomba msaada jukwaani ila usikatae kidogo kitakachofika shamba! Mkuu katika majira haya ya nyanya nyingi watu tumewahi kutoka kapa! Anakuja mnunuzi anakuta umechanganyikiwa anakuambia umuuzie mali kauli atakulipa mzigo ukifika sokoni, mkifika sokoni wanasema mzigo umefurika hakuna mnunuzi, unaanza kukumbuka 2000 ulizokataa shamba, maana ukiangalia pesa ya kulipia nauli ya gari huna unaamua kutoroka sokoni kimya kimya kurudi shamba. Mkuu endelea kutafuta soko lakini usiache kupokea hicho kinachokuja shamba hata kidogo pokea, nyanya za majira haya Kilosa wanaita "Nyanya ninyanyue nyanya ninyanyase".