Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba Ushauri - Kilimo cha Nyanya

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Maamuma, Jan 13, 2011.

 1. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 841
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wapendwa wana JF, Happy New Year!
  Jamani nina interest ya kulima nyanya kibiashara. Naomba ushauri juu ya utunzaji wa shamba, mimea hadi matunda pamoja na challenges. Nina imani nyanya zinaweza kunitoa, kwa muono wangu,
  Wenye ujuzi naomba msaada.
  Thanks in advance.
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,817
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tumia mbegu aina ya (money maker or marglobe),
  Unataka kufanya kilimo katika ardhi za mkoa upi ili tukushauri, maana zao hilo lahitaji uangalifu sana hususan hali ya ukungu wakati wa kutengeneza matunda.
   
 3. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 841
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mpevu, asante kwa ushauri. Nitafanyia Kasulu, Kigoma. Kwakuwa niko maeneo hayo, nataka niwe karibu na project yangu maana nitaweza ku-monitor closely.
  Je kuna dawa za kukabiliana na hali hiyo? Gharama yake ikoje?
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,139
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Money maker ni nzuri kwa sababu unaweza kupata nyanya mpaka sabini ktk shina moja kama umepanda kitalaam, money maker inakuwa hadi mita moja na zaidi kama mmea utapata mbolea na maji vizuri, ni nzuri kwa biashara kwa sababu zinaweza kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika na ukasafirisha mbali.

  Marglobe ni nzuri kwa kula nyumbani, zina nyama nzuri ila hazizai sana ktk shina moja, usishangae mmea ukazaa nyanya tano tu,kama unauza kwenye soko la wajuba ni nzuri sana kwa sababu bei yake iko juu, ila mmea wake ni laini sana kwa ugonjwa wa ukungu. Kwa ufupi marglobe hazifai kwa kilimo cha biashara za faida kubwa kwa walalahoi. Zafaa kwa matumizi ya nyumbani zaidi. Kama una mtaji mkubwa waweza lima marglobe, ila kwa mtaji mdogo money maker the best.
   
 5. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 841
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu Malila, nashukuru sana. Kwa mtaji wangu mdogo I'll go for money maker.
  Again, thanks.
   
 6. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,637
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Pia jaribu Roma varieties (zipo nyingi) kama zile ambazo unaona zina spherical shape. Mimi huwa naona zinachelewa kuharibika. Muhimu, onana na wataalamu wa kilimo, ikiwa ni pamoja na mabwana/bibi shambas watakupa msaada mzuri tu.
   
 7. Gwaje

  Gwaje JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 256
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Najua tanya na tengeru, sijui iwapo money maker unaweza kuipata sokoni. Unaweza pia tafuta aina hizo nilizo kutajia.
  Kumbuka kilimo hakilipi kwa ukubwa wa eneo hasa cha bustani, kinalipa kwa idadi ya mimea kwa eneo.hakikisha unapanda kwa nafasi sahihi.
  Nitumie
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,139
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Baadhi ya vijiji wanaziita moyo,
  Ni nzuri kama ulivyosema, ni tamu sana hata kwa kuzila mbichi!!!!!! na zinazaa sana,zenyewe hazihitaji miti ya kuegeshea kwenda juu kama money maker na marglobe, zinakuwa chini chini hivi. Go for garden man.
   
 9. L

  Lady JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 277
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Malila your such a wonderful man, it seems you know everything kuhusu biashara na kilimo, BIG UP BROTHER, kwa sasa i have to keep quiet just to watch, one day nitakutafuta kwa ushauri.
   
 10. M

  Malila JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,139
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Asante dada,

  Kiasi ninachofahamu ni kidogo sana,ila njaa ndio imenifanya niyatafute na kuyajua haya mambo,ukiachia mbali kuwa elimu ya kilimo nilipata kidogo kwa vitendo. Pili huku ktk kilimo ushindani sio mkubwa kama ktk biashara nyingine. karibu.
   
 11. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 841
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Malila, japokuwa ulikuwa unamjibu Lady lakini nawiwa kusema tena asante for your encouraging posts. Kwa kweli napata uthubutu wa kuingia kwenye kilimo kwa maneno yako yenye kutia moyo. I can see my dream coming true. Ubarikiwe.
   
 12. M

  Malila JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,139
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu.
   
 13. n

  nyambiJr New Member

  #13
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 14. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,817
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na utambue kuwa kilimo cha nyanya chahitaji intensive care, nimewahi kufanya kazi hiyo sambamba na mzee wangu tukiwa Tabora & Mwanza. Tulilima nyanya, cabbage, carrots na onions.
  Kwa mbegu nzuri na ambazo zinavumilia hata soko likiwa baya huko kasulu ambapo unaweza hata kuzisafirisha mkoa mwingine kwa haraka na pasipo kuharibika ni moneymaker & roma, ukikuta soko zuri kwa Tabora huwa kwa tenga ni sh. 30,000/= mpaka 50,000/=
  Pale mwanza maeneo ya soko kuu am mwaloni ni kwa tenga (mnadani) ni sh.35,000 na hupanda mpaka kufikia 80,000 kwa tenga kulingana na msimu. Maradhi makuu ya zao hilo ni UKUNGU, hakikisha unaendana na viwango vya kitaalam ktk kupulizia dawa hususan kipindi cha kutunga maua/matunda.
   
 15. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 841
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wakuu NyambiJr na Mpevu, asanteni sana kwa michango yenu. Pamoja wakuu!
   
 16. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2012
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  je mkoa wa pwani nyanya zinastawi kwa kumwagilia?nina sehemu kuna bwawa maji hayakauki
   
 17. M

  Malila JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,139
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  2011 niliona nyanya nyingi ktk vibonde fulani kule Vianzi na Msorwa Mkuranga. Pili kule Ruvu juu wanalima nyanya pia. Sasa sijui ww uko Mkoa wa Pwani kipande kipi.
   
 18. C

  CLEMENCY JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Bagamoyo ya Kiwangwa unaweza kulima nyanya mkuu?
   
 19. M

  Malila JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,139
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Samahani mkuu,
  Sijapata nafasi ya kufika Kiwangwa, nimeishia Fukayosi, hilo si neno, nyanya zinahitaji maji mengi na udongo wenye nguvu, maji ya kutosha ni sifa muhimu kwa mazao yote ya muda mfupi hasa ya bustani. Sasa hapo kiwangwa kuna maji ya kutosha na manpower ipo?

  Nyanya zikikosa maji hazitakupa matokeo mazuri.
   
 20. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,163
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  ahsante wakuu kwa michango yenu!
  Binafsi napenda kujua kuhusu kilimo cha nyanya.......ila kwa mliyoyachangia hapa yanatosha,napenda tuu kuongezea swali dogo juu ya soko la nyanya,jee ni msimu wa kuanzia mwezi gani unafaa kwa kilimo cha nyanya?ili wakati wa mavuno uvunie ktk bei nzuri?na bei ya wakati huo huwa number bei gani kwa kilo ya nyanya(moneymaker)na vipi soko la hoho lipo?
   
Loading...