Naomba ushauri juu ya hili

Asanteeni sana kwa ushauri wenu wanaJF nitaufanyia kazi.
 
Mimi ni mwanamke wa aged 30 nina watoto watatu ambao umri wao ni 10, 8 and 10.
Tatizo lililosababisha mpaka kuamua kuandika hili ni kwamba niko njia panda katika mahusiano yangu na mzazi mwenzangu. Huyu mwanaume amekuwa akiyapuuza majukumu yake ya msingi hasa ya kutunza familia, mwanzoni tulipoana alikuwa anatunza familia kwa muda miaka mitatu hivi alibadilika na kuanza kurudi saa sita usiku, siku nyingine anarudi saa kumi asubuhi akiwa amelewa sana, nikajitahidi sana kumwomba aache hiyo tabia lakini hakuacha. Kipato tulichokuwa nacho kikaishia kwenye pombe mie nikabaki ninahangaika na biashara ndogo ndogo ya kuuza karanga na ubuyu nilichokipata watoto tunakula wote, akawa hashikiki akirudi nyumbani anasearch ndani akikuta kamtaji kangu anaondoka nako atapombeka mpaka kesho yake. Basi nikawambia familia yangu kuhusu huu mwanendo lakini niliambiwa vumilia, baadae nilipata hela kidogo kutokana na biashara yangu nikajiendeleza kusoma computer sikumaliza program zote hela ikaisha, basi ilipofika mwaka 2008 nikapata kibarua kwenye Company furahi (Jina sitataja) nikaimarisha maisha yetu pale nyumbani. Tatizo linalonishangaza ni kwamba huyu mwanaume kila nikimpa mtaji afenye biashara anakula, nimeshampa kama mara tatu hivi, watoto nawahudumia mm , JE NIKIMWACHA NITAKUWA NIMEFANYA VIBAYA? Kwa sababu hata nikiongela juu ya maisha yetu anasema mm niamue nitakavyo , yaani uamuzi ni juu yangu kuachana au kuendelea kuishi.

Achana naye huyo hana maana...mpe nafasi aendelee kupombeka na baada ya muda si mrefu atagundua umuhimu mkubwa wa kuwa nawe. Pole sana.
 
Pole,umevumilia vya kutosha ndugu mi ushauri wangu ni bora uishi peke yako kuliko kuishi na mtu asiye na msaada wa hali wala mali. JUST LET HIM GOOOOOO
 
usimwache kabisa hyu ni umeo na Mungu kasema alichokiunganisha mwanadamu asikitenganishe. cha msingi piga goti sali sana tena kama unaweza panda sadaka ya mbegu kwa Mungu, ili ambadilishe pia vunja roho zaulevi na umaskini na za kutokufanikiwa kwenye ndoa yako. mwambie Mungu unataka akufanyie nini juu ya huyo mume. nakwambia shetani anakutega tu manake anajua Mungu anamakusudi na wewe na hiyo ndoa yako. Atabadilika ma dia kama ukimtegemea mungu tu. usiangalie mazingira hapa na jua hii ni vita pigana na ushinde.
 
Back
Top Bottom