naomba ushauri juu ya haya...

lilly petet

Senior Member
Feb 20, 2013
144
22
habari wana jamii forum mm ni mdada mwenye umri wa kati, naishi na mwanaume kama mume wangu ana tabia ambazo kwa kweli sizielewi kabisaaa! kwanza kwetu hajatoa chochote, pia yanayonikera ni haya mambo ya ndani, kwanza ni mtu wa kununa bila sababu yoyote, anakunywa pombe kitu ambaho mm sipend pia anakula ugoro ...naomben ushaur wana jf
 
anakula ugoro.....? sasa mnakiss aje........? uwiiiiiii......kama vipi tembea mdo mdo......hajakuoa halafu kero ndio hizo......akhaaa.......tafuta mwingine mwenye ustaarabu.........
 
mmmh hapo kazi sasa milianzaje ishi wote hata kwenu hajatoa chochote, hapo ni shida kama moyo wako haujalizika bora muachane tu usijilazimishe
habari wana jamii forum mm ni mdada mwenye umri wa kati, naishi na mwanaume kama mume wangu ana tabia ambazo kwa kweli sizielewi kabisaaa! kwanza kwetu hajatoa chochote, pia yanayonikera ni haya mambo ya ndani, kwanza ni mtu wa kununa bila sababu yoyote, anakunywa pombe kitu ambaho mm sipend pia anakula ugoro ...naomben ushaur wana jf
 
Lily... Kuna mambo ambayo yakikukuta, unamshukuru Mungu na kusonga mbele. Kwa maneno yako hayo machache inaonesha wazi kuwa huyo mwanaume hakustahili.

Amini kuwa kuna watu wakikusoma hapa wanatamani kuwa na situation kama yako. Ila hawana ujanja huo sababu walishafunga ndoa ndio anakuta mtu wake ni kimeo na hawaendani hata chembe na kuwafanya waishi kama wanadimba dimba.

Follow your heart na angalia instict zako zinakupelekea maamuzi yepi. Na tambua ukweli kuwa kama mapema hivi anafanya hivyo basi ndio alivyo na hawezi badilika. Kila la kheri...
 
habari wana jamii forum mm ni mdada mwenye umri wa kati, naishi na mwanaume kama mume wangu ana tabia ambazo kwa kweli sizielewi kabisaaa! kwanza kwetu hajatoa chochote, pia yanayonikera ni haya mambo ya ndani, kwanza ni mtu wa kununa bila sababu yoyote, anakunywa pombe kitu ambaho mm sipend pia anakula ugoro ...naomben ushaur wana jf

Kwani umeshikiwa kwa 'supagluu' hapo!? Chapa lapa...
 
habari wana jamii forum
mm ni mdada mwenye umri wa kati, naishi na mwanaume kama mume wangu ana
tabia ambazo kwa kweli sizielewi kabisaaa! kwanza kwetu hajatoa
chochote, pia yanayonikera ni haya mambo ya ndani, kwanza ni mtu wa
kununa bila sababu yoyote, anakunywa pombe kitu ambaho mm sipend pia
anakula ugoro ...naomben ushaur wana jf

Bora umejua kabla hamja funga ndoa hivyo bado unayo nafasi ya kuachana naye
 
Kama umri unaruhusu kwa nini kujiendekeza na mla ugoro na mnunaji??...
Tafuta mtu atakayekupa raha ya maisha bana...
 
habari wana jamii forum mm ni mdada mwenye umri wa kati, naishi na mwanaume kama mume wangu ana tabia ambazo kwa kweli sizielewi kabisaaa! kwanza kwetu hajatoa chochote, pia yanayonikera ni haya mambo ya ndani, kwanza ni mtu wa kununa bila sababu yoyote, anakunywa pombe kitu ambaho mm sipend pia anakula ugoro ...naomben ushaur wana jf

Mimi nadhani ulijimilikisha bila kumjua vizuri, sasa kwa sababu unamjua waweza fanya maamuzi sahihi ya kuendelea nae au kuachana nae! Angali ni mangapi mazuri ankutendea na mangapi mabaya, katika mabaya je anaweza kujirekebisha (inabidi uongee nae) na kama hawezi kujirekebisha je unaweza kuyavumilia?
 
kwanza unadai kwenu hajatoa chochote wewe si umejipeleka mwenyewe bure? uliitwa ? acha uipate fresh wewe kutongozwa siku mbili tatu unahamia? tena unasema unaishi nae kama mumeo ,ndo maana anakununia
mimi hata nigonge 50 siamii kwa mtu kihuni asilani ,acha iwe mbaya
kwa nini nikose mbingu kisa dushe?
atakula hata bange na kinyesi hapo?
tulizana mtoto wa kike
 
Tukushauri ufanyeje?
Tabia zake uzizoee?
Aache tabia zake?
Akatoe kitu kwenu?
Umuache au usimuache?

Majibu yote unayo mwenyewe.
 
1. Unawezaje kumuita mwanaume mumeo ilihali hajakutolea mahari??, nadhani nahitaji kutafuta kamusi ya Kiswahili.

2. Nina kila sababu ya kuamini kuwa "akili yako haina akili", unawezaje kuishi na mtu usiyempenda halafu bado uwe na kiu ya kuhitaji ushauri kutoka kwetu?

3. Jifunze kuwa na maamuzi magumu.
 
here we go again...mwanamke mwenyewe anajirahisisha alafu anakuja lalamika hapa. sii uondoke tuu au dushelele yake tamu sana?
 
Yaani kwa ubongo wa huyu dada, hayo maswali ni kama paper ya NECTA last year...lazima achezee division ya mwisho....

Tukushauri ufanyeje?
Tabia zake uzizoee?
Aache tabia zake?
Akatoe kitu kwenu?
Umuache au usimuache?

Majibu yote unayo mwenyewe.
 
lilly petet..ukipenda boga penda na maua yake. Kutotoa chochote kwenu ni makubaliano yenu. Swala la kununa ni juu yako kumbadilisha(play your role as woman).. Pombe na hayo mengine naamini hajaanza leo wala jana. Kama yupo addicted hawezi kuacha mara 1, mweleze kwa upole namna ambavyo hufurahishwi na hiyo tabia..
Btw umesema wewe ni "kama mke" which means sio mke.. Hayo mahari sijui utalipiwa kivp kama hamjadhamiria kuoana.
. . . . . . .
Mke mwema ni tunu bora . . . humfurahisha mumewe . . . kifuani mwake humwia uso wa kuchangamka!!
 
Last edited by a moderator:
ugoro tena hiyo kali ingekuwa sigara ningekuambia vumilia ugoro duh shika njia nenda zako
 
Huo ugoro tu jamani.. Kaaaaa ni mmasai ??

Afu hii tabia ya kununa nuna watu huwa wanaipendea nini???

Nachukia sana hii tabia yani sanaaaa.. Kama umekwazika au una jambo kwanini usiongeee?? Gubu gubu afu ukishanuna ndo umesolve??

Wenye nayo jirekebisheni kwa kweli,.. Haijengi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Maji uliyoyavulia nguo sharti uyaoge!kumbuka pia ukipenda boga penda na maua yake!!kama uliamua kuhama kwenu ukaishi na huyo "mumeo" basi mvumilie!!
 
tukushauri ufanyeje?
Tabia zake uzizoee?
Aache tabia zake?
Akatoe kitu kwenu?
Umuache au usimuache?

Majibu yote unayo mwenyewe.
ahivi dada hii tabia ya mabinti kuhamia kwa wapenzi wao inasababishwa na nini?
Ni kupanic au?
Maana ndoa ni kitu simpe tu kufunga sio lazima sherehe kama mtu anakupenda kweli kukuoa kwa utaratibu ni jambo gumu kiivo kweli hadi muishi miaka mkizini? Si bora uzini kidogo mtaani tu teh! Unakubali mtu anakutumia daily anakuchakaza akuuuuuuuuu!
 
Back
Top Bottom