Naomba Tuungane kama Mko Tayari

Amanikwenu

Senior Member
Dec 1, 2009
187
0
Wakuu,

Kati ya shughuli ninazozipenda sana ni kupanda miti. Mwaka huu wa 2010 nina lengo la kupanda miti ya kivuli na matunda (hasa miembe ya asili) isiyopungua 100.

Kama Wana JF naomba tuanzishe kampeni ya kitaifa kwa Wana JF kama timu kupanda miti katika sehemu maalum hapa nchini ambazo tutazichagua hasa zile ambazo ziko sehemu ya vyanzo vya maji. Kampeni hii ihusishe pia shule zetu na taasisi nyingine za elimu.

Napendekeza tuwe na lengo la kupanda angalau miti 1,000 kwa mwaka huu kama Wana JF. Wakipatikana wana JF 50 na kila mmoja akapanda miti 20 tu tutakuwa tumevuka lengo.

Napendekeza ndoto yetu kitaifa iwe ni kuona kila mwanafunzi hapa nchini anapanda angalau mti mmoja kila mwaka.

Nchi yetu kwa sasa ina Wanafunzi katika ngazi mbalimbali za elimu wasiopungua milioni 10.

Naomba kuwasilisha.
 
KILIMO KWANZA...!

Wazo zuri sana, actually limekuja wakati muafaka, hii ndo masika yenyewe!

Tuliokuwapo enzi hizo tuliambiwa na Mwal. Nyerere kwamba...
"Mvua za kwanza ni za kupandia"

Iam available for that pal!
 
Asante sana PakaJimmy kwa utayari wako.

Unapendekeza chanzo kipi cha maji tuanze nacho hapa nchini?

Pia jaribu kuangalia kama unaweza kuchagua shule moja hapo ulipo na kuwahamasisha Wanafunzi na Walimu ili kila mmoja wao apande angalau mti mmoja mwaka huu.

Kwa upande wangu nitatembelea shule mbili za mkoa wa Pwani (moja ya msingi na nyingine ya sekondari) na kufanya huo uhamasishaji na ikiwezekana kuanzisha vitalu vya miti katika shule husika.
 
Amanikwenu nimekupa thanx hapo. Thanks yangu inakuja baada ya kuona nchi yetu inakuwa jangwa, miti yetu ya asili ambayo inaendana na uoto asilia wa nchi yetu inapotea, tunaletewa miti ya Ulaya ambayo mingine inasababisha jangwa na kukauka kwa vyanzo vya maji. inatumika nguvu nyingi sana ya kampeni ya kupandsa miti hii ya kisasa wakati ile ya asili kama miembe, mibuyu na miti mingine ya matunda asilia ikiwepo sehemu inakatwa. mwezi wa kumi na moja kama sikosei mwaka jana, wataalam walisema ile theluji ya kilimanjaro ili iweze kurudi, inabidi ipandwe miti asilia pembezoni mwa mlima na si hii ya kisasa ambayo inakausha vyanzo vya maji. hapo utaona jinsi gani tunacheza na nchi yetu. MKUU count on me, tupo pamoja
 
post no 4 ipi hiyo?ikwenu;750418]Asante sana Pearl. Naomba uangalie post namba 4 ili nawe uone nini unaweza kufanya kwa upande wako na kisha kututaarifu. Ubarikiwe sana.[/QUOTE]
 
Wakuu,

Kati ya shughuli ninazozipenda sana ni kupanda miti. Mwaka huu wa 2010 nina lengo la kupanda miti ya kivuli na matunda (hasa miembe ya asili) isiyopungua 100.

Kama Wana JF naomba tuanzishe kampeni ya kitaifa kwa Wana JF kama timu kupanda miti katika sehemu maalum hapa nchini ambazo tutazichagua hasa zile ambazo ziko sehemu ya vyanzo vya maji. Kampeni hii ihusishe pia shule zetu na taasisi nyingine za elimu.

Napendekeza tuwe na lengo la kupanda angalau miti 1,000 kwa mwaka huu kama Wana JF. Wakipatikana wana JF 50 na kila mmoja akapanda miti 20 tu tutakuwa tumevuka lengo.

Napendekeza ndoto yetu kitaifa iwe ni kuona kila mwanafunzi hapa nchini anapanda angalau mti mmoja kila mwaka.

Nchi yetu kwa sasa ina Wanafunzi katika ngazi mbalimbali za elimu wasiopungua milioni 10.

Naomba kuwasilisha.
concrete idea...!
nitaomba niwe kati ya hao 50
 
mmh ww hata sikuamini kwakweli,mchango ulisema unanipa mpaka now hujatokea wala nn,au mchango niliotaka kukupa wa harusi niweke huku ili ijumaa niwakilishe?
concrete idea...!
nitaomba niwe kati ya hao 50
 
Amanikwenu nimekupa thanx hapo. Thanks yangu inakuja baada ya kuona nchi yetu inakuwa jangwa, miti yetu ya asili ambayo inaendana na uoto asilia wa nchi yetu inapotea, tunaletewa miti ya Ulaya ambayo mingine inasababisha jangwa na kukauka kwa vyanzo vya maji. inatumika nguvu nyingi sana ya kampeni ya kupandsa miti hii ya kisasa wakati ile ya asili kama miembe, mibuyu na miti mingine ya matunda asilia ikiwepo sehemu inakatwa. mwezi wa kumi na moja kama sikosei mwaka jana, wataalam walisema ile theluji ya kilimanjaro ili iweze kurudi, inabidi ipandwe miti asilia pembezoni mwa mlima na si hii ya kisasa ambayo inakausha vyanzo vya maji. hapo utaona jinsi gani tunacheza na nchi yetu. MKUU count on me, tupo pamoja

Chimunguru na wengine,

Asanteni sana kwa kuwa tayari. Binafsi napendekeza njia mbili kama hatua za mwanzo katika kulitekeleza wazo hili kwa vitendo.

Njia ya Kwanza
Kila mmoja wetu achague shule moja ambayo ataitembelea na kuhamasisha upandaji miti katika eneo la shule na maeneo jirani. Lengo liwe kwa kila mwanafunzi na mwalimu katika shule husika kupanda angalau mti mmoja kwa mpangilio maalum na kuutunza. Kwa Mwana JF katika shule husika lengo liwe ni kupanda angalau miti 10 kila mwaka katika shule hiyo utakayokuwa umeichagua na kuwasiliana na uongozi wake.

Njia ya Pili
Kama Wana JF tujitose na kuanzisha kampeni ya kudumu ya kitaifa ya kupanda miti ya asili kuzunguka Mlima Kilimanjaro ili kurejesha Theluji yake tukirejea maelezo ya Chimunguru hapo juu. Katika hili tumuombe Chimunguru atupe taarifa zaidi kuhusu miti gani hasa inafaa kupandwa kunzunguka mlima kilimanjaro. kati ya hiyo miti inayofaa je Miarobaini imo? Naomba mnisaidie pia kujua mzunguko wa mlima Kilimanjaro ni kiasi gani.

Pearl, maelezo niliyoyaleza kwenye namba moja hapa ndiyo yako kwenye post namba 4 katika THREAD hii. Kwa upande wako Pearl shule ipi ndiyo chaguo lako na iko katika mkoa na wilaya ipi hapa nchini?

Fistlady1, Geoff, Bujibuji na wengine tutapenda kusikia toka kwenu pia.

mm niko wilaya ya temeke ngojanitafute xul zilizopo temeke kama kibasila na nyinginezo,lini tunatakiwa kuleta majibu coz for me mda naotoka job ni late sana so kama ni kwenda hapo xul maybe jmosi I can

Pearl,

Many thanks. Itakuwa vizuri kupata feedback ndani ya mwezi toka sasa kuhusu mwiitikio wa shule husika. Pia unaweza kupata rafiki au ndugu au jirani na mkashirikiana kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom