Kbd
JF-Expert Member
- Oct 9, 2009
- 1,260
- 447
Habari za mchana wana MMU! Mchana huu nimeshirikishwa jamba na kaka yangu (tunafanya kazi wote) ili nimshauri na mimi nikaona kabla sijamshauri chochote ngoja nipate mawazo ya wapendwa wangu hapa MMU, maana palipo na wengi hapaharibiki neno.
Alivyonisimulia ni kwamba, yeye enzi za ujana wake karibu miaka 20 imepita akiwa kwenye ndoa aliwahi kutembea na mwanamke nje ya ndoa na kwa bahati yule mdada akapata mimba. Na alivyoona hivyo akamweleza huyu kaka ila huyu kaka alimkatalia kata kata na uhusiano ukaishia hapo. Naomba ifahamike kuwa huyu kaka yuko kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 31 sasa.
Sasa wiki iliyopita huyu kaka kapigiwa simu na baada ya salamu binti akajitambulisha kuwa mi mwanao, ulizaa na fulani miaka hiyo sasa ninakutafuta nikuone. Binti amemaliza form 6 na anafanya kazi na pia anaishi mkoani. Huyu kaka akampigia simu yule mwanamke aliyezaa naye na kumuuliza kulikoni akajibiwa ndio hivyo na nilikwambia ukakataa........sasa mtoto amekuwa akinisumbua kila siku nimwambie baba yake yuko wapi au kama amekufa pia nimwambie...... na mimi nikaona haina maana kumdanya mtoto kwanza ni mkubwa na anamaisha yake hivyo nikaona nimwambie ukweli.
Sasa huyu kaka yangu anajiuliza kwanza akikutana na binti yake atajitetea vipi na pili atamwambia nini mkewe ambaye kweli jambo hilo la mtoto wa nje hataki kusikia kabisa, ila yeye binafsi anatamani kumfahamu mwanae na amtambulishe pia kwa watoto wake na ndugu zake kwa ujumla.
Nasubiri mawazo yenu.