Naomba Ridhaa

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Ndugu wanajamii,
Katika moja ya post za jamii forums kuliwahi kuwa na picha niliyoiweka kwenye attachment. Jumatatu nitakuwa na conference na watu fulani wa huko nchini Uholanzi kuhusu changamoto za elimu nchini Tanzania, na namna ambavyo tanzania inaweza kupanua wigo wa ushirikiano na nchi za magharibi katika suala la elimu. Na wameniomba baadhi ya picha za mfano, na nimeona picha hii pamoja na nyinginezo ambazo tayari nimeshapata ridhaa ya kuzitumia, zinaweza kufaa. Actually nimechukua shule zenye hali duni kabisa na zile zilizo katika class ya juu kabisa ili kujaribu kuonyesha tofauti. So moderator, author wa hii picha and other members naomba ridhaa yenu.
 
Attachments

  • _shulembuyuuuuu.pdf
    31.9 KB · Views: 153
nimejaribu kufungua hazionyeshi kwahiyo mimi bado sijakupa ridhaa yangu mpaka nizione unless mimi sio mmiliki wa picha hizo, kwani jamaa wanakulipa shilingi ngapi?
 
E bwna nimeona hiyo picha lakini kabla ya kukupa ridhaa , nijuze hiyo conference ni ndani ya tza au n'je?
 
nimejaribu kufungua hazionyeshi kwahiyo mimi bado sijakupa ridhaa yangu mpaka nizione unless mimi sio mmiliki wa picha hizo, kwani jamaa wanakulipa shilingi ngapi?

nimeona picha ni ile ya watoto wanasoma chini ya mti na mwalimu anatoa taaluma ubao umetundikwa mtini,
 
Yah, nashukuru sana kama umefanikiwa kuiona, nilikuwa busy kutafuta namna nyingine ya kuipost. Actually nipo nje ya nchi, na tulikuwa tunapiga story na hawa jamaa kuhusu hali ya elimu kwao ukilinganisha na kwetu. So wakaomba tuwe na media conference japo kujadili changamoto zetu katika elimu yetu na namna ambavyo western countries zinaweza kushirikiana na nchi za Africa katika mambo ya education. Siyo rasmi sana but kwakuwa kutakuwepo na media, nina wasiwasi kwamba wanaweza kuomba wazichapishe kwenye gazeti, ndo maaana nimeomba ridhaa yenu.
Kiujumla hakuna malipo yoyote, ni kama sehemu ya kubadilishana tu mawazo. Naamini kutakuwa na majadiliano mazuri, na nitawaleteeni hapa sebuleni matokeao ya majadiliano hayo.
Regards
 
Ee bwana ee hapa kwetu tuna utamaduni wa kitu kidogo(tip). Hapa hata kura haitolewi bila kwanza kupataniwa bei ndo maana unaona watu wa kwetu wanathubutu kuivunja hata bank kuu kuiba pesa za kununua kura. Sasa to cut short story sema utatoa bei gani tukupe ridhaa ya kuzitumia? Hata downpayment tunapokea!!
 
Lakini picha hii ni kutoka sehemu gani ya Tanzania? Hiyo shule inaitwaje?
Nauliza kwa sababu picha za Afrika nyingi zinafanana, inawezekana mtu kaiona hiyo picha sehemu nyingine kaamua kuipost halafu sisi tukadhani ni ya kwetu. Ili uweze kupresent kitu kama picha lazima ujue imepigwa wapi na lini na ikiwezekana ujue nani kapiga. Ni muhimu sana kujua location ya shule yenyewe maana watu wanaweza kutaka kuitembelea na ni hapo sasa utakapoonekana useless or baseless for info you provided.
 
Kwa maelezo yaliyokuwa kwenye picha, ilionyesha kwamba hiyo picha impigwa huko Chunya Mbeya. Though haikusemwa kwamba ni shule gani hasa. Pia ilionyesha kwamba imepigwa hivi karibuni. Nadhani presentation yake ilikuwa sambamba na ile ya kigoma.
Na wewe Kiby wa kitu kidogo, down payment ndo inalipwaje?
Nitakuripoti PCB. Take care!
 
Back
Top Bottom