Naomba nichangie hoja ya January Makamba

Plato

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
420
94
Wakuu nimeikuta hii kule mjengwablog

Ndugu yangu January,

Naelewa unavyokerwa na hali iliyopo. Unachozungumzia ni uozo wa kimaadili- a moral decay ambayo pia ni rushwa kuu- Ni kansa.

Naomba niendelee..

Miaka ya mwisho ya uhai wake Mwalimu amesema sana kuhusu hatari ya rushwa kuliangamiza taifa. Akaandika pia kitabu kile muhimu- Uongozi wetu na hatma ya Tanzania.

Niseme ukweli wangu; Adui mkubwa namba moja anayetuangamiza Watanzania ni HOFU. Ni hofu inayoturudisha nyuma Watanzania. Ni hofu inayotufanya tubaki watumwa.

Nakubaliana na Dixon Mpemba, na nimeandika sana hili; kuwa Tuanze na Katiba. Mfumo wetu wa uchaguzi unachangia kutuletea viongozi ambao baadhi yao hawakupaswa hata kuongoza vilabu vya wacheza bao, lakini, kwa vile wana fedha, wananunua uongozi.

Hatuna Tume Huru ya Uchaguzi na nahofia haitakuwepo kwenye rasimu ya Katiba ijayo, sababu? Hofu ya CCM ya wapinzani kuingia madarakani. Ndugu yangu January, nahofia kukwambia, kuwa mkakati wako wa mwezi Juni unaweza kuwa umeshindwa hata kabla ya kuuanza.

Tunakumbuka Jaji Warioba alikuwa na TUME yake kuhusiana na rushwa na ripoti yake hadi hii leo inakusanya vumbi kwenye makabati. Tuendelee na juhudi hizi za kuvunja ukimya, kuondoa hofu na kukemea maovu kwa uwazi. Lakini, tuwekeze zaidi kwenye Katiba ijayo na tusiruhusu fikra zetu zifunikwe na wingu la HOFU. Ni hayo tu.

Maggid Mjengwa
 
HOFU ILIKUWEPO SIKU ZA NYUMA LAKINI SASA ISHAWATOKA WATANZANIA....Labda Kama bado ni mfuasi wa magamba kwani ndio kundi la kwanza kujazwa hizo hofu na wakatumika kuzisambaza kwa wananchi wa kawaida wakiijikita zaidi vijijini na kwa akina mama na wazee kwani kiuhalisia ndio makundi na maeneo yenye udhaifu kulinganisha na vijana & mijini.
 
HOFU ILIKUWEPO SIKU ZA NYUMA LAKINI SASA ISHAWATOKA WATANZANIA....Labda Kama bado ni mfuasi wa magamba kwani ndio kundi la kwanza kujazwa hizo hofu na wakatumika kuzisambaza kwa wananchi wa kawaida wakiijikita zaidi vijijini na kwa akina mama na wazee kwani kiuhalisia ndio makundi na maeneo yenye udhaifu kulinganisha na vijana&mijini.

hujaelewa, wenye hofu ni magamba aka ccm na sio wananchi. Magamba wanaogopa kupigwa chini. Makamba anaogopa hoja ya cdm ikipita na ikafanikiwa basi ccm watakuwa wamepigwa bao.
 
Back
Top Bottom