Kwa kuwa lengo la kwanza la CHADEMA wakiingia madarakani ni kuitisha mkutano wa Katiba sasa na kwa matazamo wangu nadhani kama hilo ni lengo wa kwanza basi CHADEMA haina sera kwa sasa. Kwa nini nasema hivyo, kwa mfano wananchi wakikataa mfumo wa majimbo kwenye katiba ni kivipi CHADEMA itatekeleza mfumo huo na kwa vile CHADEMA inaamini kuwa huo mfumo utatuletea maendeleo ya haraka sasa ni kivipi itatuletea maendeleo bila mfumo huo? Navyojua mimi sera za vyama vinatokana na katiba iliyopo. Kwenye sera ya utawala CHADEMA wamesema watapunguza mikoa kuwa 10 sasa kama katiba itakayoundwa itasema rais/chama hakitakuwa na mamlaka ya kugawa mikoa, je CHADEMA itakumia udikteta kuunda mikoa 10? Naomba muongozo.