SaidAlly
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 2,328
- 2,217
Ndugu wanaJF!
Nahitaji msaada wenu sana kuhusu tatizo la maumivu makali wakati wa hedhi anayopata mpenzi wangu.
Amekua akipata maumivu kwa muda wa karibu miaka 10 sasa, hatujapata mtoto bado na sehemu kubwa ya maoni tunayopewa ni kua atakapopata mtoto basi tatizo hilo litaisha ingawa bado hatujapanga kupata mtoto kwa hivi sasa, je hakuna namna inayoweza kumsaidia? Kwasasa ana umri wa miaka 34 na amekua akitumia tiba mbalimbali na kupata nafuu kwa muda tu, hiyo ikiwemo sindano, vidonge na hata dripu. Sasahivi hali imekua mbaya zaidi kwani ameanza juzi akameza vidonge lakini akazidiwa na maumivu ikabidi jana alazwe hospitali kwa muda akitundikiwa dripu na kupata nafuu kidogo na akapewa vidonge aendelee kumeza lakini jioni hii ya leo hali imekua mbaya zaidi tena na hata hatujui tuende wapi tena kupata msaada.
Nahitaji msaada wenu wanaJF tuondokane na tatizo hili kwani wakati wote unapofika muda wa MP amani huwa inatuishia hapa nyumbani na huzuni hutawala na kwangu mie huwa naumia zaidi kwa kushindwa kumsaidia pale anapozidiwa kwa maumivu.
Natoa shukrani zangu za awali nikiamini ntapata msaada wenu ndugu zangu.
Nawakilisha!