Naomba msaada wenu wakuu

R Mbuna

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,278
5,319
Habari za wakati huu wana jamvi.
Ni matumaini yangu mnaendelea vizuri na majukumu ya kulisaka tonge.
Nisiwachoshe sana nikachelewa kupata msaada ninaouhitaji kw ajili ya porojo zangu.
Ijumaa ya wiki iliyopita nilipata ajali ya pikipiki nikapasuka usoni na kupata michubuko kwenye mkono wangu wa kulia . Nikaenda hospitali yetu kubwa hapa kwetu Mbagala Zakiem nikashonwa nyuzi nne na kupata tiba zingine . Ila nilikosa sindano ya tetanus ,nimejitahidi kuulizia sana wapi ninaweza pata hii sindano ili niweze kuepuka madhara ya hapo mbeleni.

Wakuu kama kuna hospitali au zahanati unaijua inatoa hiyo huduma kwa hapa Dar es salaam naomba muongozo wenu ili nipate hii tiba,.

Ahsanteni

R Mbuna
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom