Naomba msaada wenu wa mawazo, natamani kudanganya

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Habari zenu wadau
Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa mkoa fulani kikazi, maeneo niliokuwa nakaa kuna mdada mmoja mzuri alikuwa amenizoea sana, nilikuwa naonana nae mara kwa mara wakati nikienda kula au nikitoka na jamaa zangu, hawa jamaa zangu kama mnavyojua ujana wakawa wananiambia uyu madada mbona unamuachia wakati kashakaa kwenye reli. Nikaona isiwe shida ngoja nicheze mechi ya kirafiki ugenini na kweli wala sikupata shida kumseti.
Sasa tukiwa chumbani nishamtoa nguo mdada akabadilika kapandisha mashetani ,ananiuliza tena sauti tofauti na ile yake mbona unataka mapenzi hujaomba ruhusa kwa kiti? wewe ni nani? tena akaanza kupandisha sauti kwakweli jasho nilikuwa linatoka huku nikiomba ardhi ipasuke niingie ndani maana kuna maneno mengine nilikuwa sielewi anaongea nini. Sasa katika harakati za kumtuliza akaning'ata maeneo ya bega kuelekea kifuani hata maumivu sikusikia. Ilichukua kama lisaa akatulia nikamtoa akaondoka zake na namba nikafuta.
Nilienda kuchoma shindano ya tetenasi japo hakukua na kidonda chochote ni alama tu ya meno.
Sasa tangu nimerudi kwangu siku chache zilizopita nimekuwa namkwepa mpenzi wangu ili nisongeze siku ili alama hii ipotee lakini na yenyewe wala haonyeshi dalili ya kupotea maana kila siku najiangalia.
Kiukweli uyu mpenzi wangu ananipenda sana na wala sitaki aanze kunitilia mashaka wala kuingia kwenye migogoro, nimerudi nimekuta kwangu amepafanyia usafi na zawadi kaninunulia.
Kiukweli hata sijui nitampa maelezo gani akanielewa na hii alama.
Waungwana msaada wenu wa mawazo na sio mnatoa hukumu
majanga yamemkuta jamaa yangu anaomba mawazo ya kujinasua
 
usimwambie ukweli hayo mambo yanauma sana kama vp mdanganye chochote tu...!!!
ukimwambia ukweli uaminifu ataupunguza kwako japo hatakuambia..!!!
assume umeambiwa wewe sasa na msichana wako ungeendelea kumwamini..!!!!
 
Maelezo umeeleza vema ni wewe then conclusion ikawa ni ya jamaa yako acha uongo na hata ushauri utakuja wa uongo.
 
Maelezo umeeleza vema ni wewe then conclusion ikawa ni ya jamaa yako acha uongo na hata ushauri utakuja wa uongo.

Alafu kweli aseee, labda ndo mana anataka pia ajue namna ya kudanganya mana ye mwenyewe muongo
 
Sema x wako alikuvamia na kukulazimisha ku sex ukakataa...
case closed
 
Maelezo umeeleza vema ni wewe then conclusion ikawa ni ya jamaa yako acha uongo na hata ushauri utakuja wa uongo.

mkuu mimi nimesumarize maelezo ndo maana unaona kama nimevaa uhusika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom