naomba msaada wenu nimwache huyu binti

mkulimamwema

Senior Member
Apr 14, 2011
153
18
Watanzania mimi ni mwanaume niliye na mchumba ninayemjali sana,nilimwamini na kumtambulisha kwa ndugu zangu lakini ghafla amebadilika anazima simu na kuwa na visingizio vingi.Leo ilifikia hatua ya kunikatia simu na nilipompigia hakupokea pamoja na kumpigia mara nyingi ingawa alijaribu baadae kunipigia nilishindwa kupokea kwani nilikuwa bado nina hasira.
Huyu bibie amegundua kuwa nampenda sana hata akikosa si mwepesi kuomba msamaha mpaka nimkumbushe,nimevumilia sana lakini kwa kuwa sijamwoa naona bora nichague mwingine lakini kabla ya kuamua sipo peke yako nina ndugu zangu kwenye familia yetu ya jammii forum naomba ushauri wenu nichanganye na wa mbayuwayu
 
Alivyokupigia simu si ungepokea na kumuuliza kulikoni, kwa kutokupokea kwako na yeye anaweza akajenga tafsiri yake, lkn chunguza hayo mabadiliko ya ghafla
 
kiufupi dm wako anajisikia sana kama vp mpotezee madem wengi wanatafta wa kuwaoa yy anakuzingua bado hujachelewa huyo dm ana mambo mengi
 
Back
Top Bottom