Naomba msaada wa kisheria haraka

Kim Jong Un

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
496
258
Mimi nimezaa na Dada mmoja ambaye tulikuwa kwenye mahusiano ya muda baadae tukaachana, kwa saa kila mtu anaendelea na maisha yake.

shida iliyopo ni kuwa huyu mzazi mwenzangu hataki nimchukue mtoto hata kwa dakika, na mtoto anaishi na wazazi wa huyo dada na wzazi wake haniruhusu kumchukua, hawataki nimlipie karo shuleni, hawataki nimpe matumizi.

nataka msaada jinsi ya kuwa namchukua hata maramoja kwa week. na kumrudisha au kukaa naye. kushiriki kwenye kulipa karo ya mtoto. na vitu vingine.

mtoto ana miaka minne.
 
Kisheria, wazazi wanapotengana ama kuachana, mtoto ana haki zifutazo.

1. Kulelewa ama kuhudumiwa pamoja na kupata elimu kama ile aliyopata awali kabla ya wazazi kutengana azma kuachana.

2. Haki ya kuishi na mzazi( baba au mama) ambaye kwa mtazamo wa mahakama aweza kumhudumia kwa maslahi bora ya mtoto.

3.Mtoto ana haki ya kumtembelea na kuishi na mzazi wake wakati wowote anapohitaji, isipokuwa kama tu, itaingilia masomo ama mafunzo yake.

Sheria pia imeweka dhanio (presumption) ya kwamba kwa kuzingatia maslahi bora ya mtoto, kama ni mwenye umri chini ya miaka saba awe na mama yake ingawa dhana hii yaweza pingwa (rebuttabal presumption).

Hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 26(1) cha Sheria ya Mtoto mwaka 2009. Maelezo yako na mtazamo wa kisheria ni kwamba anachokifanya
mzazi mwenzako ni kinyume na sheria na kinamnyima haki mtoto na kufanya ww kushindwa kutekeleza wajibu wako kisheria
 
Ni ivi mtoto chini ya miaka saba sheria inasema atakaa na mama ake ila una haki kisheria ya kumsomesha na kumpa mahitaji yote muhim ikiwepo kumtembelea pia
 
Hapa amesema huyo mtoto anakaa kwa wazazi wa mama yake.
 
Kuna kitu kinaitwa walfare principle tunaangalia mtoto yupo kwenye mazingira bora ya malezi kama uko aliko anapata malezi bora kuliko akimchukua yy bas ataendelea kukaa uko ila mdau naona anataka kuwa anamtembelea mwanae iyo sheria ipo waz ana haki iyo
 
Nenda Mahakama ya Wilaya uombe Amri ya Matunzo ya Mtoto. Utaomba Mahakakama itoe amri ya kutoa matunzo kwa mtoto na haki ya kumuona mwanao. Akifika miaka saba unaweza kupewa kabisa kama mazingira ya nyumbani kwako ni salama kwa mtoto.
 
Amri itatekelezeka tu ikiwa huyo mama wa mtoto atakuwa mwelewa. Hata kama mahakama itatoa amri lakini ikiwa mama atakuwa akimficha mtoto pindi baba akienda kumtembelea unafikiri amri hiyo itakuwa na maana?
 
Ni ivi mtoto chini ya miaka saba sheria inasema atakaa na mama ake ila una haki kisheria ya kumsomesha na kumpa mahitaji yote muhim ikiwepo kumtembelea pia
Si lazma, sheria imeweka presumption ama dhanio ili kuhakikisha maslahi bora ya mtoto, kama hayo hayapo inaweza pingwa na hivyo kufanya mtoto chini ya umri wa miaka saba asiishi na mama yake...(it is a rebuttable presumption)
 
Yes nakubaliana na ww
 
Nilitaka kujua mmeishi kwa kipind gan? Kama ni zaid ya miak miwili sheria yandoa inatambua kwamba yule ndiye mkeo,, nirudi kwenye swari lako la msingi

Sheria ya ndoa au the law of marriage Act, 1971 Cap29 R:E 2002 imasema hvii kama baba na mama watatengana watoto wote waliopo chini ya miaka saba wataondoka na kwenda kuish na mama yao..

lakin
Mume inabdi atoe huduma zote zinazo stahili kwa wale watoto au mtoto hususan kama ulizo zitaja hapo Juu,, ila wewe kukuzuia usitoe huduma kwa yule mtoto wanfanya makosa,

Cha msing fanya yafuatayo

1. Ww inabd uihusishe Familia na watu mbalimbali wenye busara kifamilia

2.ww inabdi uend kweny vyombo vya dini kwa usuluhishi.

3.kwenda katika baraza LA usuluhishi la ndoa.

Ni hayo tu naomba niwasilishe
 
thanks guys hakika mmenipa unafuu wa moyo.

swali: yawezekana kuwa ninamchukua mtoto weekend na kumrudisha jpili jioni. maana natamani kuspend muda na yeye pia.
 
Nilitaka kujua mmeishi kwa kipind gan? Kama ni zaid ya miak miwili sheria yandoa inatambua kwamba yule ndiye mkeo,, nirudi kwenye swari lako la msingi

Sheria ya ndoa au the law of marriage Act, 1971 Cap29 R:E 2002 imasema hvii kama baba na mama watatengana watoto wote waliopo chini ya miaka saba wataondoka na kwenda kuish na mama yao..

lakin
Mume inabdi atoe huduma zote zinazo stahili kwa wale watoto au mtoto hususan kama ulizo zitaja hapo Juu,, ila wewe kukuzuia usitoe huduma kwa yule mtoto wanfanya makosa,

Cha msing fanya yafuatayo

1. Ww inabd uihusishe Familia na watu mbalimbali wenye busara kifamilia

2.ww inabdi uend kweny vyombo vya dini kwa usuluhishi.

3.kwenda katika baraza LA usuluhishi la ndoa.

Ni hayo tu naomba niwasilishe
Mkuu mm nna kesi km hii japo ni tofauti kidogo,mm tulitengana na mahakama iliamua mtoto miaka saba nikae nae maana mama siyo mtulivu,nyumba tulojenga itakuwa ya mtoto chini ya usimamizi wangu,shida ilotokea hapa ni mama haonekani kujali kujasor kumuona mtoto jambo ambalo halinipi shida,lkn wakati nakaa nae alikuta nnawatoto ambao wakati tunaoana na kujenga walikuwepo na kushiriki,lkn mahakama haijawatambua km warithi,sasa nafanyaje ili kufanya wahusishwe na nyumba nloambiwa niisimamie mm,la pili nnaweza kuchagua msimamizi tofauti na mama ake iwapo ntafariki wakati mtoto hajafikia kujitambua?,na tatu umri tambulika na mahakama wa kujitambua ni upi,samahani km nimetoka nje ya mada
 
Mimi nimezaa na Dada mmoja ambaye tulikuwa kwenye mahusiano ya muda baadae tukaachana, kwa saa kila mtu anaendelea na maisha yake.

shida iliyopo ni kuwa huyu mzazi mwenzangu hataki nimchukue mtoto hata kwa dakika, na mtoto anaishi na wazazi wa huyo dada na wzazi wake haniruhusu kumchukua, hawataki nimlipie karo shuleni, hawataki nimpe matumizi.

nataka msaada jinsi ya kuwa namchukua hata maramoja kwa week. na kumrudisha au kukaa naye. kushiriki kwenye kulipa karo ya mtoto. na vitu vingine.

mtoto ana miaka minne.
we ndo uliempa dada yetu mimba afu ukamtelekeza, wajomba zake tupo tutamcare hatutaki kuona pua yako hapa
 
Hata kama unataka msaada kisheria lakini unaonekana wewe ndo una makosa haiwezekani wakukatalie yote hayo kama ulifanya ujinga basi hiyo family inajiweza kaombe msamaha acha ujinga mtoto utampata tu

Back
Top Bottom