Naomba msaada wa hii sentensi

Tom wa Arusha

Member
Jun 14, 2011
6
7
Kuna hii sentensi, sasa sina uhakika kama ina leta mantiki au la. ila ninependa kuwashirikisha nanyi wenzangu."Baba/mama mimi ni mwanao wa ngapi?" sasa kwa kiingereza sijui ita tamkwaje au kuandikwaje?
 
Baba, / mama, mimi katika kuzaliwa ni wangapi?

Baba,/mama, katika watoto wako mie ni wa ngapi kuzaliwa?
 
Kuna hii sentensi, sasa sina uhakika kama ina leta mantiki au la. ila ninependa kuwashirikisha nanyi wenzangu."Baba/mama mimi ni mwanao wa ngapi?" sasa kwa kiingereza sijui ita tamkwaje au kuandikwaje?
dah tom imekataa hiyo.
 
Kuna hii sentensi, sasa sina uhakika kama ina leta mantiki au la. ila ninependa kuwashirikisha nanyi wenzangu."Baba/mama mimi ni mwanao wa ngapi?" sasa kwa kiingereza sijui ita tamkwaje au kuandikwaje?

You could ask someone: "Where do u fall in your family's birth order"?- yaani kwenu wewe ni wangapi kuzaliwa?
Kwa hiyo: kwa sentensi yako unaweza kumuuliza baba/mama yako: "where do I fall in the/our family's birth order"?

Siku njema.
 
Tatizo ni kwamba watu wengi wanafikiri lugha ni kama hisabati....yaani 1 + 1 = 2 na pia 2 = 1 + 1. Lugha haipo hivyo jamani. Kingereza sio mirror image ya Kiswahili na wala Kiswahili sio mirror image ya kiingereza.

Sio kila neno au sentensi ya kiswahili inaweza kupatiwa kingereza chake cha moja kwa moja, na sio kila sentensi ya kingereza inaweza kupatiwa kiswahili chake cha moja kwa moja.

Kwa hiyo basi.....sentensi hiyo "Baba/mama mimi ni mwanao wa ngapi?" inaweza kutafsiriwa kwa njia nyingi kutegemea na nani anauliza na madhumuni ya kuuliza.....majibu mengi yaliyotolewa huko juu yapo sahihi.

Ila usitegemee kupata sentensi ya moja kwa moja....haitaleta maana.
 
Back
Top Bottom