Naomba mnisaidie neno lipi ni sahihi?

Ndio na ndiyo
kwa mtizamo wangu maneno yote ni sahihi inategemea unataka kutumia wapi na kwa nani,
mfano neno NDIYO 2naweza kutmia hivi tamaa NDIYO iliyomponza,ndiyo nimekuelewa,ndiyo nimetekeleza.na
neno NDIO linaweza kutumika hivi hii ndio njia sahihi ya kufundishia.
 
watoto mmelewaaaaaa= ndiyoooooooooooooooooooooooo
hawa ndio watoto wangu!
 
Matumizi yote ni sahihi, lakin ni vizuri zaidi kutumia kama ifuatavyo:
1. Ikiwa nomino inayotajwa ni katika kundi la I-ZI kama vile, njia, barabara, kanzu, nazi, gari n.k. ni bora kutumia NDIYO. Mifano: Njia hii ndiyo uliyoichagua mwenyewe. Gari ile ndiyo iliyopata ajali
2. Ikiwa nomino inayotajwa ni katika kundi la A-WA na U-I, kama vile kijana, mfanyakazi, akinamama, mti n.k, ni bora kutumia NDIO. Mifano: Vijana uliotaka waje ndio waliofika. Mti uliokata ndio hasa niliokutuma. Akinamama ndio walioitwa hapa, wewe dume umekuja kufanya nini?
3. Kama unaandika neno moja tu, basi ni vizuri kuandika NDIO badala ya NDIYO. Mfano: Swali- Utakwenda Arusha kesho? Jawabu- Ndio.
4. Wakati tunapotamka, tukataka tusitake, tunatumia NDIYO kwa sababu itakuwa vichekesho kusema NDI-O.
 
Ndio:
Ndio interjection That is the way it is! Yes!, They are the ones!,
Ndio pronoun Yes,
ndio sababu conjunction for that reason, Therefore,


Ndiyo:
Ndiyo (Ndizo) pronoun Yes,
Ndiyo interjection Yes, That is the way it is! Yes!,
ndiyo maana conjunction that's why, yes it is so,
Ndiyo pronoun it is so,

-yo :
-yo verb relative That, Which,

Kwa ufupi zote sahihi.
 
Ningelipita kama alipopita MAMMAMIA...."ndio"
wote tungepita alipopita MAMMAMIA......"ndiyo"
ni msisitizo tu kwamba maelezo yako nayaunga mkono
 
nashukuru kwa maelezo yako lkn je ni sahihi kusema "Gari ile"? au ni "Gari lile"
 
nashukuru kwa maelezo yako lkn je ni sahihi kusema "Gari ile"? au ni "Gari lile"
Unayosema ni kweli, kwenye sarufi ya Kiswahili Sanifu gari iko katika "Noun class" li-ya na wala sio i-zi kama nilivyosema mimi. Kwa maana hiyo gari litakuwa halihusiki na ndio/ndiyo bali ndilo.
Asante sana kwa kunikumbusha, uelewa wangu wa Kiswahili sio mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom