Naomba mnieleweshe hapa kiswahili sahihi ni ipi maana inanichanganya

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
ukisoma kwenye magazeti au majarida utaona waandishi wanatofautina kuelezea hili sentensi,sentensi ipi ni sahihi hapa chini?


1. Shirika la benki la taifa.
2. Shirika la taifa la benki
 
Askari nashukuru,kwa hiyo ile 'la' pale kati nayo ni kosa?
 
1.Shirika la benki la taifa.
2. Shirika la taifa la benki

Mie nadhani kwa ufahamu wangu sentesi hizi mbili zinabeba maana mbili tofauti,
unaposema Shirika la Benki ya Taifa hapa unataka kuonyesha kwamba, shirika hili ni la Benki yaani unataka kutoa utambulisho kwamba, hili shirika ni la benki na linahusiana na masuala ya benki na . Sentesni ya pili ya Shirika la taifa la benki, hii ni fasili na maana ya kwamba, shirika hili ni la taifa kwa maana kwamba, hili ni shirika la taifa yaani sio la binafsi na kadhalika, kwa hiyo unatoa utambulisho juu ya shirika la taifa ambalo linahusiana na masuala ya Benki.
 
Back
Top Bottom