Naomba mawazo yenu

Hapo inabidi turudi katika hulka ya mtu binafsi, vitu vikubwa vinavyo muathiri mtu ni kabila na Elimu! amini husiamini kidogo dini pia huwa uleta utata lakini hivyo viwili vya ongoza.

Elimu ni nambali moja. Sisi Waafrica/Tanzania tumejengeka katika mambo ya kificho, hii ni tabia mbaya sana maana kila tunalofanya katika medali ya mapenzi tunafanya kwa kificho, hata yeye anaamini anamsema Mmewe kwa kificho! wanakuwa na wapenzi watatu wana-amini wanafanya kwa kificho! wanaotembea nje ya ndoa wana-amini wanafanya kwa kificho! wanakuwa na wapenzi wao wazuri pia wanashindwa kuwapereka nyumbani maana ni kificho! utamwambia vipi Baba na Mama! wakati ni Dunia ya kificho! Haya mambo ya kificho katika nchni kama zetu zimeperekea hata watu kuoa na kuolewa na watu ambao sio wapenzi wao, huo ni wakati wa kutimiza wajibu, unaolewa na mtu ambaye humpendi au unaowa mtu ambaye humpendi, unajifanya unampenda kwa kificho. Matokeo ndio hayo, hapo hamna mapenzi.

Mi naamini kificho ni rafiki wa giza, na giza ni rafiki wa Shetani!
 
Back
Top Bottom