Naomba mawazo yenu

Aisha Adam

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
460
103
Kuna mdada mmoja mfanyakazi mwenzang kaolewa ana mme na mtoto mmoja, kinachoniuma ni kwamba huyu mdada anakipato kikubwa kumzidi mmewe sasa akikorofishana na mmewe anaanza kuwaambia wafanyakazi wao kuwa mmewe hana kitu chochote ndani hata nyumba hajaweka hata mfuko cement so asiwababaishe.
Nimshauri nn huyu mdada ili aachane na tabia hiì make weng hawajaipenda
 
huyo ni mshenzi wa tabia
tena ni mshamba na hizo pesa kazishika ukubwani
we utamuanikaje mume wako mbele za watu eboo
kaniudhi sana..
we mwambie aache hiyo tabia watu wanamchora..
ni wajibu wake pia kujihusisha na maswala ya nyumbani, kama mume hajaweka hata mfuko wa cement kwani tatizo ni nini?
si aliapa katika shida na raha..mxiiiiiiiiiiiii binadamu wengine ovyoo ushamba huo wa kushika pesa ukubwani
mbona wanaume wakijihusisha 100% hawatangazii ulimwenguu..aache utoto huyo

tafuta lugha nzuri ya kumwambia ila ujumbe ndo huo.
 
...mwambie aache ulimbukeni. Hamvunjii heshima mumewe pekee, hata ndoa yao anaivua nguo!
Maisha hayana Guarantee kwamba kila siku yeye ndio atakuwa juu kwa kipato.
Abadilike haraka iwezekanavyo.
 
Limbukeni tu huyo bi mdada. Aache ushamba. Mwambie kuwa kuna wenye hela zaidi yake na hawana dharau za kijinga kama zake. Hizo hela zinaweza kupukutika muda wowote bila hata ya tahadhari.
 
Aache ushamba hela nini bwana
kuwa na pesa sio unakuwa na kila kitu katika dunia hii
awe makini na ndoa yake isijevunjika
ipo siku mumewe atakuwa na hela zaidi ya zake
asubiri kusimangwa pia
 
Kuna mdada mmoja mfanyakazi mwenzang kaolewa ana mme na mtoto mmoja, kinachoniuma ni kwamba huyu mdada anakipato kikubwa kumzidi mmewe sasa akikorofishana na mmewe anaanza kuwaambia wafanyakazi wao kuwa mmewe hana kitu chochote ndani hata nyumba hajaweka hata mfuko cement so asiwababaishe.
Nimshauri nn huyu mdada ili aachane na tabia hiì make weng hawajaipenda

Imekuwa ni tabia yake kumkejeli mume wake hapo ofisini kwasababu na hao anaoongea nao hawaonyeshi kuchukizwa na tabia hiyo. Hivyo unaweza kumuambia ila kama siyo mtu muelewa akabaki anaendelea kama kawaida. Kwaiyo mbali ya kumuambia yeye, jaribu kutumia hekima kuwasilisha jambo hili kwa wenzako na kuwauliza wao wanalionaje. Hapo utaweza kujuwa mtazamo wao kama wanalichukulia kuwa ni kawaida au na wao hawalipendi. Kama hawalipendi, shirikiana na wenzako kwa vitendo kumuonyesha kuwa hamuipendi tabia yake ikiwa ni pamoja na kumuambia.
 
Ulimbukeni tu huo unamsumbua....mshamba saaaaaaaaaaana huyo mfanyakazi mwenzako.kama maisha yanaenda vizuri yanini kuwafuata watu na kuwaeleza?ndoa inahitaji kutunziana siri....huyo mwanamke hajafundwa kabisa....yani anawahaibisha wanawake wenzake...mkemeeni huyo kwa tabia mbaya.
 
Aache ushamba hela nini bwana
kuwa na pesa sio unakuwa na kila kitu katika dunia hii
awe makini na ndoa yake isijevunjika
ipo siku mumewe atakuwa na hela zaidi ya zake
asubiri kusimangwa pia

Nadhani yeye ataachwa kabisa..
 
Hebu jaribu kuongea hayo mabaya anayowaambia mbele yake....wakati akiwa kwenye good time na mumewe.....
 
Huyo dada ana matatizo na wala hajajua maana ya ndoa. Unapokuwa ndani ya ndoa chochote kinachopatikana na "CHENU". Sasa anapowaambia hao wafanyakazi ili iweje? Huyo dada nadhani anahitaji maombi haraka sana kwani inaonesha upendo kwa mumewe umepungua kabisa, huwezi kumsema vibaya umpendaye.
 
Sa' bi Aisha kwanini usijali hamsini zako? we kwani ni shahidi wa mahsuiano yao?

Wewe una uhusiano naye kama nani?Sijui unataka kumshauri wewe ukiwa kama nani kwake?? kama anaweza kumsema mbovu mumewe mbele za watu, unafikiri wewe utasalimika?..
 
huyo ni mshenzi wa tabia
tena ni mshamba na hizo pesa kazishika ukubwani
we utamuanikaje mume wako mbele za watu eboo
kaniudhi sana..
we mwambie aache hiyo tabia watu wanamchora..
ni wajibu wake pia kujihusisha na maswala ya nyumbani, kama mume hajaweka hata mfuko wa cement kwani tatizo ni nini?
si aliapa katika shida na raha..mxiiiiiiiiiiiii binadamu wengine ovyoo ushamba huo wa kushika pesa ukubwani
mbona wanaume wakijihusisha 100% hawatangazii ulimwenguu..aache utoto huyo

tafuta lugha nzuri ya kumwambia ila ujumbe ndo huo.

Nyani haoni kundule mboa na sisi huwa tunawaanika wake zetu kuwa aah ni golikipa mara hana lolote mlinzi na yanapotokea kutoelewana ndo kwanza tunawasema vibaya eti aah mwanamke mwenyewe hana lolote hapa ndani hajachangia hata cement lkn si kakupa mawazo mazuri jamani!! tuache tu kusemana vibaya hizi kauli zinakera kwetu sote !!! la msingi tuondokane na tabia ya mawazo pungufu hata kama umemtoa mwenzio sio umwanike mara nyingi ni ushamba au kaonyeshwa kukerwa sana na tabia hiyo!!
 
Kuna mdada mmoja mfanyakazi mwenzang kaolewa ana mme na mtoto mmoja, kinachoniuma ni kwamba huyu mdada anakipato kikubwa kumzidi mmewe sasa akikorofishana na mmewe anaanza kuwaambia wafanyakazi wao kuwa mmewe hana kitu chochote ndani hata nyumba hajaweka hata mfuko cement so asiwababaishe.
Nimshauri nn huyu mdada ili aachane na tabia hiì make weng hawajaipenda

Huyo ukiangalia alikotoka ni kama hiyo avatar yangu sasa kapata kishasahau.
Mwambie kutafuta ni wajibu,
pesa ni matokeo tuu. Yeye leo
kesho mumewe Sweetdada punguza hasira.
 
mhhh sishangai dunia ina watu wa kila design. Mfuate mme usikie kwanza mawazo yake ikiwezekana umshauri mme jinsi ya kumwelemisha mkewe, ila wewe kumfuata huyo mama naona km una beep matusi yake.
 
Mwambie arudi kwa kungwi wake akamwambie hakuelewa topic ya Maana ya ndoa kungwi airudie. Na nyie kwa nini mnasikiliza huo ujinga? Si mumshushue tu!
 
khaaaaa
ndo tabia gani hiyo..
ye hajui maisha ni mzunguko..
ngoja siku ya geuke ndo ataimba haleluya
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom