naomba kuuliza ili mtu apate lessen ya udereva wa gari anatakiwa awe na sifa zipi

kituro

Senior Member
Dec 25, 2010
176
15
Ndugu katika jf. naombeni kuelimishwa. ili mtu aweze kupewa lessen ya kuendesha gari TZ anatakiwa awe na sifa zipi. tafadhali naomba kujulishwa!
 
1) awe anazijua vizuri sheria za usalama barabarani (2) awe na akili timamu (3).....
 
Uwe mtanzania, umri uzidi miaka 45, mwanamke atapewa kipaumbele, uwe na gari

madereva wa daladala za mitaani kwetu asilimia kubwa hawajafikia umri huo hapo inakuwaje? ofisi nyingi watu huwa wanakwenda kuomba kazi ya udereva wakiwa wanaleseni tu wala hawana magari hapo unasemaje! ubaguzi wa aina yoyote ukiwemo ubaguzi wa kijinsia ni kosa kubwa na linakuwa linakiuka katiba unataka kunambia katiba ya hapa kwetu tanzania inajipinga kiasi hicho!. jambo la muhimu hapa ni kumsaidia muuliza swali, lakini siyo kuandika Frustration zetu hapa!

 
Miaka kuanzia 18
Akili timamu
physically fit(unakwenda hospital kupima kama unakizi vigezo vya kumudu kuendesha)
upitie mafunzo ya udereva

Mengineyo yatatokana na niliyoeleza
 
Ndugu katika jf. naombeni kuelimishwa. ili mtu aweze kupewa lessen ya kuendesha gari TZ anatakiwa awe na sifa zipi. tafadhali naomba kujulishwa!

Ukitaka leseni mpya ni sharti utimize mambo yafuatayo. Kwa leseni Class D, vigezo siyo vikali kuliko kuanzia class C.

  1. Unatakiwa uwe na TIN No. Kama huna utaenda TRA kufungua ni bure.
  2. Unatakiwa uwe na leseni aidha F (Lena) au ya za zamani ambayo utakuwa unaibadilisha.
  3. Tshs 40,000.00 kwa ajili ya malipo ya leseni hiyo.
  4. Vyeti vya chuo ulichosoma hasa kama unataka class C, maana ni lazima uende chuo cha usafirishaji au VETA.
Uwe tayari kufanyiwa majaribio hasa kama unataka Class C.

 
Back
Top Bottom