Naomba Kuuliza:.....CONCERN FOR THE ELDRLY (COEL) TANZANIA Ni kina nani....?

Mh SAMBALA

Member
May 29, 2011
43
2
Naomba Kuuliza..

CONCERN FOR THE ELDRLY (COEL)
TANZANIA.

Ni kina nani hasa hawa...?

Leo amefika mgeni Ofisini kwangu toka
NGO ya COEL (DICKSON ISRAEL SWAI)

Kijana huyu anadai kutumwa na NGO hiyo kuja kutoa elimu kwa wananchi wangu.
Juu ya haki ya Vikongwe.

Na pia amekuja na barua ya DC ,RC na
WIZARA inayomtambisha kwetu. Barua kum/ADGB/193/225/01/74 ya tarehe
23/3/2007. Inaliruhusu Shirika hilo kutoa elimu ya
mafunzo mtambuka.

Kwa madarasa ya
MEMKWA. Pia barua kumb Na. DA 25/122/01/
TEMP/19 Iliyotolewa 4 Oct
2011.Inamtambulisha mwezeshaji na
kumruhusu afanye kazi zake kwa jamii.

Na pia OFISI YA DC Kondoa nayo imempa barua Kumb AB. 233/374/01/153 ya tarehe
13. Feb, 2012 ya kumtambulisha.

Maswali ya kujiuliza je kwa nini kila
mwananchi anayehitajiwa kupatiwa elimu
anashurutishwa kulipia kiasi cha 25,000/=..?

Na je Ofisi zilizompa barua ndo wamekubaliana atoze watu kiasi hiki...?

Na pia katika msongo wa uongozi
wanaonyesha kuwa na Viongozi mpaka
ngazi ya
Shina
Kitongoji,
Kijiji, Kata,
Taarafa. Na wameahidi kutoa ajira kwa hao
watakaopatiwa mafunzo.

Je wanauwezo wa fedha kiasi hicho...
Kumudu waajiriwa hawa...?

Na kwa watu wa mwanza tunaomba
mtupe taarifa za kina juu ya hawa COEL
manake wamejitambulisha kuwa na Ofisi
kuu Mwanza.

Na sanduku lao la barua ni 2345 Mwanza.

Tahadhari, mwaka 2008 lilikuja shirika
kama hili TAADE. TANZANIA ADULT EDUCATION.

Hawa baada ya kukusanya fedha za watu waliishia mitini na kwa kondoa walishakusanya zaidi ya mln 30/= Wakiwa na mbinu kama hizi..

Na mpaka leo hakuna anayewajua wako wapi hao TAADE.

NAWAOMBA WANA JF WENYE
KUWAJUA VYEMA WATUELIMISHE NA
KUTJUZA ZAIDI. KARIBUNI KWA MAJADALA.

(chanzo TANURI LA FIKRA)
 
Issue yenyewe umeitoa FaceBook mi nilizani kisanga kimekupata? Kama chanzo ni FB wapelekee hao watoto wa FB Tanuru la Fikra watakusaidia! Kama mmeliwa kubalini tu kwani ndiyo mfumo wa ajira binafsi!
 
Nimesema ofisi yangu mimi mwenyewe leo na kesho nafanya wdc ktoa maamuzi....
 
Ni shirika lililo chini ya rais mstaafu Ally H. Mwinyi
S.L.P 9173
SIMU: 2700040
(ndo mlezi mkuu) WAWEZA KUFANYA MAULIZO KWA MAWASILIANO HAYO.

WALEZI NA WAKURUGENZI
1. Hon Judge Mark Bomani- mshauri mkuu COEL-TAIFA

2. Mr. Leonard Derefa (huyu ni mlezi wa kanda ya zíwa)

3. Mr. Steven Mashishanga mlez kanda ya kati

4. Mr. Valley Mwanisongole na

5. Mr. George Gambuna Koya

hawa ni wakurugenzi wa shirika.

VIONGOZI WA SHIRIKA KAMATI KUU NI

1. Mr. Jamathon Magodi -Mwenyekiti Mtendaji wa COEL

2. Mrs. Zamoyoni Bakari -m/mkíti

3. Mrs. Zena Shaban Boimanda -katibu mkuu

4. Mr. Philip W. Mwakagile -Mkurugenzi na

5. Mr. Leonard Kulwa- Mhazini

COEL imesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya 19540 Cap 337 tarehe 2.6.2000 na kupewa hati namba So. No. 10448.

Na baada ya kufanya vizuri COEL imepata usajili wa pili tarehe 12.02.2007 chini ya sheria ya NGO'S Act 2002 na kupewa cheti cha kukubaliana na utendaji kazi za shirika (certificate of compliance) No. 1765 ya tar 12.02.2007


nímechoka kuandika nashauri ni PM ili nikupf namba ya simu tuongee au nikupe mobile namba ya mmoja kati ya hao hapo juu.

IFAHAMU COEL, IJUE COEL.
 
Back
Top Bottom