Naomba kuuliza, cement huharibika baada ya muda gani?

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Kama ikihifadhiwa vizuri bila kufunguliwa, cement inaweza kuwa useful kwa mda gani? Naomba wataalamu wanijulishe..
 
Inategemea na mtengenezaji,jibu sahihi utalipata baada ya kusoma kwenye mfuko wa cement husika kwani ni lazima itaonyesha tarehe ya mwisho wa matumizi.........................kuharibika kwa cement sio kuganda tu,kwani inaweza ikawa haijaganda lakini isifae kwa matumizi kwani ubora wake utakuwa umepungua.............cement nyingi nadhani hudumu kwa miezi sita toka itengenezwe kama itahifadhiwa vizuri.
 
Kwa hali ya kawaida utafiti umeonyesha:
baada miezi 3 nguvu hupungua asilimia 20 hadi 30.8aada miezi 6 ni asilimia 30 hadi 40.Baada ya mwaka nguvu itapungua kwa asilimia 40 hadi 50.
Ni muhimu kuhifadhi saruji pasipo unyevu wa aina yeyote unaotoka sakafuni,ukatani,bati au kutoka kwenye hewa.Nguvu ya zege hutegemea mambo kadha pamoja na nguvu ya saraji./wingi wa saruji katika mchanganyiko,usafi na wingi wa maji,kiwango cha mchanga na kokoto,ukorogaji na umiminaji,ukuzaji(curing) baada ya kumimina
 
Back
Top Bottom