naomba kukazia maneno sahihi ya kiswahili na matumizi yake

Ms Judith

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
2,563
918
mazoea yanaweza kufanya maneno fulani yaonekane kuwa yanatumika kwa usahihi, lakini ukweli ni kinyume chake. mfano haya yafuatayo"

1. siyo, sahihi ni sio
2. ndiyo, sahihi ni ndio
3. ndio yeye, sahihi ni ndiye yeye
4. ndio wewe, shihi ni ndiwe wewe
5. ndio mimi, sahihi ni ndimi mimi
6. hichi, sahihi ni hiki
7. liwalo lote, sahihi ni lolote liwalo
8. onyesha, sahihi ni onesha
9. maonyesho, sahihi ni maonesho,
10. aidha... au..., sahihi ni aidha,..../......au......
11. siyo... wala...., sahihi ni si.... wala.....
12. kufariki, sahihi ni kufa
13. (fulani) anachechemea, sahihi ni (fulani) anachehechema/anachechemeka
14. shuka juu, sahihi ni shuka chini
15. toka nje, sahihi ni tokea nje/toka ndani
16. ukweli, sahihi ni kweli
17. uoga, sahihi ni woga
18. nk.

wengine mwaweza kuongeza ama kusahihisha.
wapendwa tukienzi kiswahili.

Glory to God
 
Asante miss Judith. Umenikumbusa kua swahili yangu iko mbofu. Inabidi mimi rekebisa.
 
Miss Judith nashukuru umeleta huu mjadala mzuri kabisa. Pamoja na uzuri wa mjadala nina mashaka na usahii wa maana na matumizi ya baadhi ya maneno uliyoyaleta hapo juu.
Mimi nafahamu kwamba neno kama NDIMI tayari liko nafsi ya kwanza umoja. Linatokana na muungano wa kivumishi kitenzi-nomino thibitishi: NDIO na kiwakilishi nafsi MIMI
NDIO+WEWE = NDIWE
NDIO+HII/HIYO = NDIYO
Neno UKWELI liko sahii, na wingi wake ni KWELI. Maana inategemea sana
Nitarudi hapa jamvini kuendeleza uchambuzi na kuleta vielelezo na vyanzo vya maelezo yangu.
 
Kwa mtizamo wangu, "naomba kukazia..." nadhani ungeandika "naomba kusisitiza..."; mana'ake nilipoanza kusoma kichwa cha habari nilipata mshtuko na msisimko kwa wakati mmoja. Otherwise, asante kwa changamoto!
 
Onyesho na Onesho yote yapo sahihi neno ONYESHO=Ni hali ya kumpa mtu Onyo kuhusu jambo fulani.na neno ONESHO=hutumika kama vile band zinapotumbuiza jukwaani,hili huitwa Onesho
 
ndimi mimi.............nadhani mimi haitakiwi kuwepo tena hapo inakuwa marudio ya maneno .

Nashukuru kwa kutumbusha
 
suala na swala...suala hili; swala hili....kule visiwani wanatumia sana suala na sisi Tanganyika naona tunatumia sana swala. Hebu tusaidie hapa Dada Judy.
 
Acha kuchanganya watu wewe. Neno la kwanza tu umechemsha, na hayo mengine je?
Huwezi kusema 'ndio yenyewe', unasema 'ndiyo yenyewe'.
Kapitie upya 'Ngeli' za Kiswahili ujikumbushe.
 
Miss Judith nashukuru umeleta huu mjadala mzuri kabisa. Pamoja na uzuri wa mjadala nina mashaka na usahii wa maana na matumizi ya baadhi ya maneno uliyoyaleta hapo juu.
Mimi nafahamu kwamba neno kama NDIMI tayari liko nafsi ya kwanza umoja. Linatokana na muungano wa kivumishi kitenzi-nomino thibitishi: NDIO na kiwakilishi nafsi MIMI
NDIO+WEWE = NDIWE
NDIO+HII/HIYO = NDIYO
Neno UKWELI liko sahii, na wingi wake ni KWELI. Maana inategemea sana
Nitarudi hapa jamvini kuendeleza uchambuzi na kuleta vielelezo na vyanzo vya maelezo yangu.

nakubaliana nawe mpendwa, katika kiswahili kuna mikazo/misisitizo hutumiwa mara nyingi na huwa katika mtindo wa kurudia mfano mtu akisema "nyumba hihi hii", eneo hilihili, mtu huyu huyu, nk. neno hii linarudiwa kuonesha mkazo au msisitizo. hata unaposema "ndimi", ingetosha tu ila unapotaka kuongeza msisitizo kwa kurudia hilo neno ndio matumizi yake sahihi yapaswa kuwa ndimi mimi na sio "ndio mimi". vivyo hivyo katika ndiwe wewe

nashukuru umafafanua "ndio hii"= ndiyo

tuko pamoja katika kuboresha matumizi ya kiswahili.

Glory to God
 
Onyesho na Onesho yote yapo sahihi neno ONYESHO=Ni hali ya kumpa mtu Onyo kuhusu jambo fulani.na neno ONESHO=hutumika kama vile band zinapotumbuiza jukwaani,hili huitwa Onesho

umesema sawa kabisa mpendwa. tatizo watu hutumia onyesho wakimaanisha onesho, maonyesho wakimaanisha maonesho.

Glory to God
 
ndimi mimi.............nadhani mimi haitakiwi kuwepo tena hapo inakuwa marudio ya maneno .

Nashukuru kwa kutumbusha

sawa mpendwa, angalia nilivyojibu kwa omukuru. thanks

glory to God
 
suala na swala...suala hili; swala hili....kule visiwani wanatumia sana suala na sisi Tanganyika naona tunatumia sana swala. Hebu tusaidie hapa Dada Judy.

ndugu yangu BAK yote ni sahihi na yana maana tofauti. swala linatokana na mambo ya ibada hasa ya kiislamu, kwa ibada za kikristu wanatumia sala zaidi lakini yote yana maana sawa au inayokaribiana na prayer/worship kwa kingereza. ila hilo la pili la "suala" linamaanisha " an isshue" kwa kiingereza na wingi wake ni masuala yaani issues. huo ndio usahihi wake na yapaswa kutumika hivyo kote bara na visiwani.

Glory to God
 
Acha kuchanganya watu wewe. Neno la kwanza tu umechemsha, na hayo mengine je?
Huwezi kusema 'ndio yenyewe', unasema 'ndiyo yenyewe'.
Kapitie upya 'Ngeli' za Kiswahili ujikumbushe.

asante ndugu, siwezi hata siku moja kufungua JF ili kudanganya watu. kama nimekosea mahali, nielimishe tu yatosha na mimi nipate kujifunza.

kuhusu mchango wako, anagalia nilivyojibu kwa omukuru kuhusu ndio+hii= ndiyo, kwa hiyo ndio+yenyewe= ndiyo. ila ukitaka kuongeza msisitizo ndo unasema "ndiyo yenyewe" ubarikiwe sana

Glory to God
 
Asante sana Judith umenikumbusha darasa la 3 kwenye kutunga sentensi, ila kiswahili changu kinahitaji urekebishi!
 
asante ndugu, siwezi hata siku moja kufungua JF ili kudanganya watu. kama nimekosea mahali, nielimishe tu yatosha na mimi nipate kujifunza.

kuhusu mchango wako, anagalia nilivyojibu kwa omukuru kuhusu ndio+hii= ndiyo, kwa hiyo ndio+yenyewe= ndiyo. ila ukitaka kuongeza msisitizo ndo unasema "ndiyo yenyewe" ubarikiwe sana

Glory to God

Kule visiwani pia wenzetu wanasema suali na sisi bara tunasema swali. Mfano: "sikulielewa suali lako" na "sikulielewa swali lako" neno lipi kati ya haya mawili ni sahihi.
 
Mnajitahidi lakini, mnhhh, kiswahili cha mtowa mada na anavyo-shajihisha inaonesha anajitahidi lakini bado ana kazi ndefu ya yeye mwenyemewe kujifunda.

Mfano; si swala, ni swalaa au kama watumiavyo wengi iwe waIslaam au si waIslaam, Sala

Swala = mnyama.
 
Swalaa- dini,
Swala - Mnyama wa porini mwenye uwezo wa kukimbia mwendo wa kasi
Suala - Jambo fulani
Kwenye red nadhani ulitaka kumaanisha "an issue" - Miss vipi tena mamito mtaalam wa kiswahili kama wewe unachanganya kiswahili/kingereza?

ndugu yangu BAK yote ni sahihi na yana maana tofauti. swala linatokana na mambo ya ibada hasa ya kiislamu, kwa ibada za kikristu wanatumia sala zaidi lakini yote yana maana sawa au inayokaribiana na prayer/worship kwa kingereza. ila hilo la pili la "suala" linamaanisha " an isshue" kwa kiingereza na wingi wake ni masuala yaani issues. huo ndio usahihi wake na yapaswa kutumika hivyo kote bara na visiwani.

Glory to God
 
Mnajitahidi lakini, mnhhh, kiswahili cha mtowa mada na anavyo-shajihisha inaonesha anajitahidi lakini bado ana kazi ndefu ya yeye mwenyemewe kujifunda.

Mfano; si swala, ni swalaa au kama watumiavyo wengi iwe waIslaam au si waIslaam, Sala

Swala = mnyama.

kwenye keyboard hapa huwezi ku-explore kila kitu. nakushukuru kuwakilisha na umesomeka mkuu. pamoja sana
 
Swalaa- dini,
Swala - Mnyama wa porini mwenye uwezo wa kukimbia mwendo wa kasi
Suala - Jambo fulani
Kwenye red nadhani ulitaka kumaanisha "an issue" - Miss vipi tena mamito mtaalam wa kiswahili kama wewe unachanganya kiswahili/kingeeza?

haha, hapo kwenye red is just a slip of a pen/finger wala si kuchanganya liugha mpendwa na kwa kweli sijafikia kiwang cha kuitwa mtaalam wa kiswahili, hapa najitutumua tu ndugu yangu, wataalam wenyewe wapo si unaona hata wengine wameishaanza kunitolea uvivu?

Glory to God
 
Kule visiwani pia wenzetu wanasema suali na sisi bara tunasema swali. Mfano: "sikulielewa suali lako" na "sikulielewa swali lako" neno lipi kati ya haya mawili ni sahihi.

BAK leo naona watu wa visiwani unao, huwaachii wakapumua!

mimi niaminivyo ni kuwa kusema swali ndio sahihi, sasa sijui wataalam wenyewe wakija itakuwaje. lets wait they are comming
 
Back
Top Bottom