Naomba kujua historia ya Urusi

Safi sana mkuu.pata soda kwa mangi hapo ntakuja kulipa...lol hapa elimu tosha kabisa,naona na Magufuli wetu anajaribu ku apply baadhi ya mambo aliyofanya Roosevelt ya new deal....
Cant wait for the next episode
 
Phase hii umenikumbusha vitu vingi hususan new deal niliisoma ten years past

Kumbuka kaka swali langu la uchumi wa kichina na ubepari nawakwti n nchi ya kisoshalisti?
Uchumi uliomfanya mwalimu ang'atuke Larkin wao walikope vip mwalimu asindwe na wakat n marafiki
 
Phase hii umenikumbusha vitu vingi hususan new deal niliisoma ten years past

Kumbuka kaka swali langu la uchumi wa kichina na ubepari nawakwti n nchi ya kisoshalisti?
Uchumi uliomfanya mwalimu ang'atuke Larkin wao walikope vip mwalimu asindwe na wakat n marafiki
Mtaalaam yuko chimbo anafukua nondo labda naweza anza kidogo kisha atamalizia. Kwa uchina wana sera wanaita “socialism with Chinese characteristics ” yaani watawala waliamua “kuchanganya” mifumo ya ubepari na ujamaa. Siasa za nchi ni za kijamaa kwamaana ya hakuna vyama vingi kila kitu kinapangwa na serikali lakini uchumi ni wa kibepari uliochanganywa na vionjo vya kichina. Viwanda muhimu “strategic industries” mathalani viwanda vya kijeshi viwanda vya IT (huawei na vingine) viwanda vya solar viwanda vya ndege za kijeshi na za kiraia nk vyote viliwekwa chini ya Jeshi ama chini ya makampuni ya china. Pia wawekezaji wa nje wanaonzisha viwanda wanatakiwa kuingia ubia na makampuni ya china kama sehemu ya kutransfa ujuzi na technolojia. Kifupi sehemu kubwa ya uchumi wa china unamilikiwa na serikali(jeshi). Mkuu emperor atakuja malizia
 
Aisee very interesting.....especially hii NEW DEAL....nadhani mh. Magu angepitia hii "new deal program" yapo mambo mengi sana tunaweza kuyakopi na yangeweza kutusaidia...mfano TVA na Agriculture Adjustment Act...kwa nchi yetu hii yenye rutuba ya kutosha basi nadhani Africa kusingekua na njaa.
Mkuu @The Emperor nathamini sana kazi yako mkuu.....endelea kutupa darasa, elimu ni bahari
 
Hivi we kupe una skili kweli...eti russia haiko kwenye nchi tajiri 15 ..kwakweli wewe ni mjinga wa mwisho..
Hebu nenda google uandike G8 alafu uone russia ni ya ngapi??

Yaani wewe unaanduka kitu kutoka kichwa chako kinsvyokutuma unazani huku labda watu hatujui kutafuta data??
Hata nchi zinazoongoza kwa tecnolojia ya juu kabisa duniani Urusi imejzidi china, Uingereza na Ufaransa.
Duuh heb kajifunze kudanganya ndo urudu humu..
Nimevumilia maneno yako . Pia nimetafuta na ku google sana lakini bado siioni russia katika nchi 10 tajiri duniani. Pia siioni katika nchi kumi zilizo na strong economy duniani. Hebu nisaidie notice zako unazitoa wapi
 
Nimevumilia maneno yako . Pia nimetafuta na ku google sana lakini bado siioni russia katika nchi 10 tajiri duniani. Pia siioni katika nchi kumi zilizo na strong economy duniani. Hebu nisaidie notice zako unazitoa wapi
Acha uongo bana we umegoogle wapi? Ile nimeandika g8 countries zikaja,ufaransa,ujerumani,canada,uk,usa,rusia,japan and italy,acha uvivu
 
New deal inahitaji mapato ya kutosha na viwanda wezeshi

Wamarekan walikuwa na kila kitu ila soko likakosekana na pia alikuwa na wataalamu wa kutosha pia kipindi hicho hakukuwa na umoja imara wa kuyumbisha nchi kama sasa bali lilikuwa taifa moja n lingine

Magu akianza inabidi aipunguze nguvu na ushawishi wa upinzani then atende haki kwa wabadhirifu wa mali na awape nafasi washiriki kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji

Pia new deal lazim ifunge watu wa nje katika uwekezaji hata kuwapunguzia share je itawezekana?

Nchi kandamizi zinatabu si mchezo
 
Nimevumilia maneno yako . Pia nimetafuta na ku google sana lakini bado siioni russia katika nchi 10 tajiri duniani. Pia siioni katika nchi kumi zilizo na strong economy duniani. Hebu nisaidie notice zako unazitoa wapi

mkuu embu angalia hii link ya CIA "WORLD FACT BOOK" : The World Factbook
lakini pia lazima ujue hawa wakubwa wana vigezo tofauti tofauti vya kupima "maendeleo".ukiangalia hii fact book kuna avigezo tofauti katika kigezo kimojawapo inaonekana urusi ipo kwenye top ten. Wajuzi zaidi wa hivi vigezo labda wajazie nyama. Alichokuwa anasema huyo muheshimiwa uliyemkoti ni kuwa urusi ipo katika list ya nchi nane zilizoendelea zaidi kiviwanda na hii si longo longo ni fact mkuu. Angalia hizi link mbili zifatazo hapa utapata kitu:
1. The Group of Eight (G8) Industrialized Nations
2.WorldRichestCountries.com

karibu tujadiliane
 
Daaaah Mkuu Emperor umetisha.
Baada ya kumaliza kuisoma hii episode nikasema leo mbona umeandika epsod fupi hivi nikaanza kuscowl kurudi juu, heeeh kumbe ndefu, mim niliiona fupi kama salama ya 'mambo'. Laiti kama maandiko haya yangekuwa kwenye likitabu likubwa kama 'BS' au dictionary ya Oxford basi usiku huu lingeisha.
Big up Mkuu.

Nimeangalia profile yako upo kwenye senior member. Ombi langu kwa invisible akupendelee uwe expert member maana wew ni muhim kama Ensten kwenye bom la atomic.
Wew ni moja kati ya watu wachache sana wanaojitolea kwa mamufaa ya wengine paspo wew kubenift directly.
Rai kwa wandishi uchwala makala hizi ni electronic signatured Emperor through JF kwa matumizi mengine yeyote yale tafadhali pata kibari cha Emperor.
Ubarikiwe
 
Heshima kwako kaka, URUSI ni moja kati ya nchi zenye historia kubwa saana ya kufurahisha.Kwanza urusi zamani iliitwa Russian Empire haikuwa na eneo kubwa kama unavyoliona sasa.Urusi ilitawaliwa kwa zaidi ya miaka 300 na familia ya RAMANOV ambayo utawala wake ulifikia kikomo mwaka 1917 baada ya mapinduzi makubwa ya wakomunisti...kihistoria mfalme anayekumbukwa kuipanua urusi kuwa kubwa mara mbili anaitwa Czar Peter the great au St.Peter.Urusi ilikuwa na nguvu kwa miaka mingi kijeshi kwasababu ya ukubwa wake,rasilimali nyingi na hali yake ya kijeografia ambapo ni baridi sana utoweza kuruhusu wageni kuvamia kirahisi mfano mzuri ni pale ambapo mfalme Napoleon Bournaparte wa Ufaransa alivyoivamia na jeshi la watu kama laki sita hivi mnamo miaka ya 1800's na kupigwa vibaya na mfalme Alexander wa Urusi ambapo aliiamuru miji yote ichomwe moto na kisiachwe chakula ili wafaransa wakija wapigwe na baridi kali ili wafe na kwa bahati nzuri ilitokea hivyo.kadiri miaka ilivyoendelea Urusi ikaanza kuwa dhaifu kwasababu ya mfumo wa Feudalism ambao uliruhusu rushwa na utawala wa watu wachache juu ya wengi walio maskini,kumbuka urusi ni moja ya rainbow states since ina multiple ethnical groups,kama Caucasian,jews,mongols etc.Urusi ilijiingiza kwenye struggle for power mnamo miaka ya 1800's hadi 1900's na matifa ambayo ni madogo kuliko yeye lakini yalikuwa tayari yamesha fanya mabadiliko ya kiviwanda kuliko yeye hivyo kupelekea kushindwa vita hata na kitaifa kama Japani na Uturuki.Mnamo miaka ya 1914 ilitokea vita ya dunia ambapo mfalme wa Urusi bila kufikiria aliliingiza taifa la Urusi vitani kisa kulinda tu heshima yake,wakati huu Urusi ilikuwa haina silaha za kutosha na za kisasa kama automated rifles,aircrafts,tanks and submarines hivyo alitegemea sana silaha kutoka kwa Muingereza,..Mrusi alijiunga na muingereza na Mfaransa kuwapiga adui na majirani zake Germany Empire,Uturuki kipindi hicho ni Ottoman Empire na Austria.Warusi wengi kama 4million walikufa hivyo kuifanya Urusi kuwa Taifa maskini sana na chovu kuliko yotee ulaya.

Mnamo mwaka 1917 mfalme wa Urusi alianza kuua wanaharakati ambao walitaka asitishe vita na kufanya mabadiliko ya kimfumo,watu kama Vladmir Lenin walikuwa exiled ambapo alirudi mwaka 1917 kuendesha mapinduzi makubwa ya kikomunisti ambayo yalipelekea Civil war hadi mwaka 1919 ambapo mataifa mengi dunian hayakupenda ukomunisti hivyo yakasupport wapinzani wa Lennin ila walishindwa.hii ni historia ndogo tuu.

Urusi chini ya Lenin na ukomnisti iliweza kuunda nchi inayoitwa USSR au The UNION OF THE SOVIET SOCIALIST REPUBLICS au CCCP,ambayo iliweza kuanzisha ujamaa ambao kwanza uliwaunganisha warusi wote kwasababu walikuwa na uchumi sawa na hali sawa,pili iliwekeza sana kwenye elimu na pia mwisho jeshi la Urusi lilikuwa linaanza kufundisha watoto wakiwa na umri wa miaka 6.Lenin aliunda mifumo ya kipelelezi iliyoitwa Cheka,NKVD na GRU hivi ndivyo vyombo vilivyoifanya urusi iwe leo unavyoiona.Mwaka 1924 Lenin alifariki akaingia raisi anayeitwa Stalin ambaye alikuwa ni dikteta mbaya ambaye alivitumia vyombo hivyo kuua maadui wa Urusi na kuiba technolojia ya mataifa ya magharibi na kuiletea urusi.1939 dunia iliingia vitani tena ambapo urusi ilionyesha umahiri mkubwa saana kijeshi baaada kumshinda Hitler alipoivamia hapa napo walifanya tena kama kwa Napoleon walikimbia kuelekea Red Square ili wajerumani wadhani kwamba warusi hawana nguvu kumbe walikuwa wanasubiri winter ianze ili baridi iwasaidie.ndaendele kesho:smile-big:

Now sasa the world war came to an end in 1945 ambapo the then Super power Great Britain alikuwa amechoka vibaya sana kiuchumi hivyo Marekani na USSR wakajikuta ndiyo mataifa yenye nguvu duniani kumbuka mrusi na marekani ndiyo walikuwa wa kwanza kuingia berlin walianza kufanya sabotage na assassinations za Nazi leaders lakinin kikubwa walichokifanya GRU ya Urusi ni kuwateka scientists wa nazi na kurudi nao urusi huku na marekani alikuwa akifanya vivyo hivyo.Marekani aliiba project kubwa sana ya ujerumani na kuipa jina la The Manhattan Project ambapo ilipomalizika we all know what happened to Hiroshima na Nagasaki.Mwaka 1945 raisi Franklin delano Roosevelt alifariki dunia na kumwachia madaraka makamu wake mwendawazimu aliyeitwa Harry S Truman ndiye aliyeruhusu mabomu ya atomic code Name FAT MAN na THE LITTLE BOY kuangushwa pale japan.USSR under Joseph Stalin hawakukupenda kile kitendo provided that Japan aliisha surrender na viongozi wake kama General Hedaki Tojo na Sugiyama walikuwa wamejiua.USSR alitumia mwanya wa vita ya pili kujitanua ambapo nchi kama poland,georgia,kazkhastan,ukraine,east germany na vijitaifa vya Eastern Europe vilimezwa kinguvu kitu ambacho kiliyaogopesha mataifa ya Magharibi kwamba nayo yataja mezwa.USSR ilikuwa ndiyo nchi kubwa sana duniani kuliko zote ambapo kijeografia ilikuwa inastretch almost Eleven time zones.Marekani kwa kuigopa urusi alishauri mataifa ya Ulaya ili kujilinda yatengeneze umoja wa NATO mwaka 1947,formation of Israel naton in the middle East mwaka 1948 kumbuka Israel ilitakiwa iwekwe hapa East Africa kwetu lakini walipima ni jinsi gani watzuia the Soviet advance(russian advance),Warusi walitumia mitandao yao kufinance vikundi vya kikomunisti vya Uchina hadi kupelekea mwaka 1949 kushinda na kuwaumiza Wamarekani kwa kiasi kikubwa saaaana kiuchumi.Mwaka 1949 mrusi aliishangaza dunia baada ya kurusha kombora la nuclear ambapo marekani alijua analo peke yake hivyo kupelekea mahusiano yao kudorora,Mrusi ndiye aliyekuwa anaongoza kuwa na sophisticated Rocket technology kuliko Marakani hivyo kufanya the red army kuogopwa saaana.Mnamo miaka ya 1949 hadi mwaka 1950's kulikuwa na kitu kinaitwa The Molotov Plan ambao ulikuwa mpango wa ku counter The Marshall plan ya Marekani ambao ulikuwa unatoa mikopo kwa mataifa yaliyoumizwa kiuchumi na vita ya pili.Warusi walikuja kufanya maajabu tena baada ya kuanza extensive innovation projects ambapo kalashnikov aligundua bunduki yenye nguvu saana aina ya AK47 au Avtomot Kalashnikov,tena miaka ya 60's mrusi ndiye aliyekuwa wa kwanza kurusha Artificial Sattelite kwenye Orbit na tena pia Mrusi ndiye aliyekuwa kwanza kupeleke mtu(cosmonaut)outer space nadhani alikuwa anaitwa Yiri Gargarian kama sijasahau.Mrusi alitumia mitandao ya upelelezi kama NKVD na GRU ambapo walipenyeza serikali za marekani na mataifa ya Nato ambapo walikuwa wanua viongozi wakubwa kwa poisoning na other tactics mfano mzuri waliweza kuunda kitu kinachoitwa THE RING OF FIVE pale Yale UNIVERSITY ambacho kilikuwa kinaua wanafunzi ambao wanaonekana ni future potential American leaders,umoja huu uliundwa na wnafunzi ambao walikuwa ni wamarekani.Urusi ilikuja kuugopesha dunuai mbapo mwaka 1961 walipeleka makombora ya Nuclear pale Cuba huku wakilenga miji mikubwa ya Marekani kama Chicago,Atlanta na newyork huku raisi wa Urusi wakati huo alikuwa anaitwa Nikita Krushchev alikuwa anawatishia Nato kwamba I WILL BURRY YOU,ilibaki kidogo ianze Nuclear War laikini wakubwa huwa wanaogopana yakamalizwa kwa diplomasia,lakini hata CIA wanakiri kwamba vita ingeanza wangeshindwa vibaya kwasababu wlijiamini na kujua kwamba vita haiji kuingia jirani na USA,they were wrong coz this time the bad omen was at their door step.Mrusi alikuwa na military bombers ambazo zilikuwa na uwezo wa kufanya mashambulizi makubwa saaana USA ukiangalia ujirani kati ya Cuba na USA.Mrusi alikuja kushikwa pabaya na USA kwenye the Six Days War ambapo mmoja wa mjasusi wake alikimbia Urusi kama alivyofanya Snowden na kuelekea Uingereza ambapo alitoa secret files za majina ya secret ghost agents wa Urusi ambao walikuwa wanaoperate middle east hivyo kupelekea wauawe na Israel kushinda vita,kushindwa huku kulipelekea Urusi chini ya rais mpya bwana Leonid Brezhnev kutengeneza the lethal weapon ambayo itaweza ku undermine all world intelligence agencies na kuirudisha Urusi katika hali yake,waliunda kitu kinachoitwa KGB.Trust me people even the Mossad feared the KGB,it was notoriuos,efficient killing machine,efficient tool for collecting information,tromendous tool in drafting national policies,masters of infiltration and good suppressors of internal dissidents.KGB itakumbukwa kwa kuifanya Urusi iwe the most feard country in the world hasa chini ya boss wake aliyeitwa Yuri Andropov ambaye alikuja kuwa rais wa Urusi baadae.KGB ilianza kupenyeza majasusi wake hadi kwenye jeshi la Marekani ambapo waliweza kumrecruit US NAVY chief ANthony Walker ambaye alifanya kazi kwa miaka 18 na kgb.Urusi na China walihusika saaana kuwaua Wamarekani kwenye Vietnam war,Urusi ndiyo waliilinda India mwaka 1971 ili USA wsiivamie na kweli USA alishindwa kuvamia India.Ije ikumbukwe Mrusi anakuwa na Nguvu saaana kwasababu huwa habetray allies wake kama USA,ambapo anawalinda NORTH KOREA,VIETNAM,SYRIA,IRAN na mataifa mengine washirika wake wakubwa.Urusi kailinda saaana Syria kwasababu kwanza ni nchi ambayo inavitega uchumi vikubwa saaaana vya mrusi kuna makampuni ya mafuta kama Tatneft,pia kampuni la mafuta la Syria linanua vifaa kama pipes kutoka Russia,pia Syrian Air and Marine companies vessels zake nyingi ni za Mrusi na pia mbali na south Asia soko kubwa la silaha liko Syria sasa.Mrusi hawezi ruhusu mataifa ya magharibi kuvamia kwasababu amewekeza saana Syria kwenye manufacturing industry,Urusi alizubaa libya kuna mikataba ambayo alisiani na Qaddafy ya matrilion ya Pesa ili aimalize mwaka 2011 lakini akazubaa uongozi ulivyoingia mpya dili la silaha akapewa mfaransa Urusi ikaumizwa na ndiyo maana sasa ailitishia vita NATO wakaogopa.Naomba niishie hapo.


CC:
Dotworld , maziku Masunga Jr , Bukyanagandi , MALCOM LUMUMBA
Ebana upo vizuri sana mkuu..umetisha mbaya..au wewe usalama wa taifa nini mana upo more than deep
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom