Naomba kujua.

JACADUOGO2.

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
930
217
Naomba nifahamishwe kwamba diwani akijiuzulu udiwani, kwa kawaida uchaguzi wa diwani mwingine badala yake unatakiwa ufanyike baada ya muda gani tangu kujiuzulu kwa yule diwani?
Kwa mfano, katika jimbo la Rorya kuna madiwani watatu wa kata tatu tofauti walijiuzulu kuanzia Desemba 2010 lakini mpaka leo Julai 2011 hamna dalili yoyote ya uchaguzi ndani ya zile kata tatu katika jimbo la Rorya! Madiwani waliojiuzulu wote walikuwa wa CCM ambao ni Ongujo Wakibara wa kata ya Mkoma, Mr. Ambogo kata ya Nyahongo na Okeya Ogigo.
Hawa madiwani walijiuzulu kutokana na manyanyaso ya mbunge wa jimbo la Rorya Lameck Airo hasa katika mchakato wa kumchagua mwenyekiti wa halmashauri ya Rorya ambapo Mh. Lameck alitumia ubabe kumpachika ndugu Ochelle katika hiyo nafasi bila ya maridhio ya baadhi ya madiwani.
Naombeni mnisaidie!
 
Back
Top Bottom