Naomba kujua ukweli kuhusu 'kiama'

Ni siku ya khasara.Ni siku ya hukumu.Ni siku ya majuto.Ni siku iliyo kuu.Ni siku ya malipo.Ni siku ya hesabu.Ni balaa kubwa.Ni siku ya mkusanyiko.Ni tukio la haki.Ni tukio la uhakika kabisa.Ni siku ufufuo.HIYO NDIO SIKU YA KIAMA.
Ni siku ambayo haitamfaa mtu mali yake wala watoto wake.Ni siku ambayo wanafamilia watakimbiana.Ni siku ambayo washirika watakataana.Ni siku ambayo siri zote zitafichuka.
Ole wao wale wanaokanusha siku hiyo!
 
Free ideas
Unaye mama/baba? Baba yako anaye baba?
Unaamini Babu ya mababu zako alikuwa ni nyani au binadamu/mtu?

Kuwa nyani kivipi!?,we ni mmoja wa wale mnachanganya,neno "Look like" na ""To be"!,.

Hawakuwa manyani bali they were "cousins of"
Je wewe ni moja ya wale wanaoamini kwamba mtu wa kwanza kuina ziwa victoria alikuwa white man!?.Ukiambiwa changanya na zako!

Inaonekana hauijui Evolution vizuri
 
Kwanini story zote za kumuhusu shetani(kama yupo) zinatoka kwenye biblia(au vitabu vya dini), je nae hakupata nafasi kujielezea, je, alinyimwa uhuru wa kujieleza kama bunge lilivyominywa? Ndo maana vitabu vilivyopo anaelezewa kama mpinga Mungu.

Kama alitupwa kuzimu, na Yesu akamfata, akamfungia kuzimu na kuchukua funguo(hawezi kuja duniani mpaka kiama), mbona bado inasemekana "anawapitia" watu na bado wanatenda dhambi.
Kwanini unapotaka kimjua Mungu kupitia uhalisia(ukihoji uwepo wake) unapata vitisho kwamba, utakufa, utapata mabalaa, Mungu hahojiwi nk.

"Sisi wanaadam hatuhitaji DINI ili tuwe na MAADILI, kama hujui kutofautisha ZURI na BAYA, basi tatizo lako ni UELEWA"
 
kuna watu wanatoa shuhuda ati walifika jehanamu na mbinguni kisha wakarudi duniani kuwakumbusha watu habari ya siku ya kiama i karibu kuja
 
Pitia jukwaa la jamii intelligence,kule angalau utapata majibu kwa kiasi.

Ila usiache kuutafuta ukweli kupitia google,youtube nk

Kaanze kutafuta hii makitu reincarnation.
una uamini kwa kiasi gani ukweli uliopo kwenye youtube na google mkuu?
 
Kuwa nyani kivipi!?,we ni mmoja wa wale mnachanganya,neno "Look like" na ""To be"!,.

Hawakuwa manyani bali they were "cousins of"
Je wewe ni moja ya wale wanaoamini kwamba mtu wa kwanza kuina ziwa victoria alikuwa white man!?.Ukiambiwa changanya na zako!

Inaonekana hauijui Evolution vizuri
Unasema nini?
Babu ya babu zako zilikuwa ni cousins of nyani(manyani)?
Au babu zako look like Manyani?
Babu zako ni manyani?

Nieleweshe vizuri hapa, Evolution ipi hiyo unayozungumzia hapa ndugu?




Za kwako ushazichanganya au umechanganyikiwa?
 
Unasema nini?
Babu ya babu zako zilikuwa ni cousins of nyani(manyani)?
Au babu zako look like Manyani?
Babu zako ni manyani?

Nieleweshe vizuri hapa, Evolution ipi hiyo unayozungumzia hapa ndugu?




Za kwako ushazichanganya au umechanganyikiwa?


Inaonekana hata hujui maana ya "cousin" Jitahidi kuelewa hoja!
 
Naomba nianze kukujibu kirahisi. Kwanza kiama ni kufufuka Kwa watu wote tangu Nuhu. Na baada ya kiama ni huku ya ulimwengu siku hiyo ulimwengu huu utakuwa ndo mwisho wake. Labda nikujuze gharika ya kwanza iliangamiza dunia ya kwanza ikaiacha Nchi ukiwa na utupu. Hii ili kuwa hukumu ila haikumhusu Ibilisi. Gharika ya Nuhu iliivunjavunja Dunia na kuacha watu 8 tu. Watu hao wakaishi dunia nyingine sio ile ya Adam. Niseme hivi gharika ya kwanza haikuwa na viumbe kama sisi. Sisi Mungu ametuthamini kuliko viumbe vyote na ndio mungu alipotaka kuangamiza na kufuta kizazi hiki nuhu akapata Neema. Mungu akapunguza umri na akaweka siku atakayo mhukumu shetana na watu watakao mfuata ibilisi hii nikuanzia watu nane ambao mpaka sasa wanatumikia adhabu kupunguziwa umri na kuwa miaka 120. Kiama ni kufufuka watu wote kwenda siku ya hukumu kuu ambao ndo siku ambayo Ibilisi na wafuasi wake wata lipizwa kisasi na Mungu Kwa uharibifu na usumbufu tangu kabla ya mwanzo wa ulimwengu huu hadi siku hiyo. Jibu Kwa Mungu hakusubiri kiama Kwa vizazi vingine ili kuwa ni mifano kwetu kuonesha hasira zake kumbuka Mungu amehukumu Kwa garika Mara 2 lakini hukumu hiyo haikumuhusu Ibilisi hata moto wa sodoma ili kuwa ni mfano tu na ndiyo maana hakudumu milele ila Moto huo wa Milele ndio adhabu ya Mwisho ya Mungu na kukiondoa kabisa kiumbe Shetani.
 
Kasome kitabu cha ufunuo wa Yohana ukikimaliza utaelewa kiama ni nini??
 
Inaonekana hata hujui maana ya "cousin" Jitahidi kuelewa hoja!
Free ideas huonekani kujibu maswali unayoulizwa wala kutoa ufafanuzi wa unayoyaandika.
Vipi utasaidiwa kufuta ujinga na kuongeza maaarifa?

Rudia michango ya nyuma na kama una maelezo au majibu, yaweke ili ueleweke.
 
Iyo ni imani yatupasa kuamini ivo ili tutende Yale ya kumpendeza mungu

23dae6b3657d58d87c59072973a789d2.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom