Naomba kujua kuhusu mafao ya NSSF

Jan 6, 2012
31
4
Habari zenu wakubwa,
je kuna mtu yeyote ambaye amewahi kuchukua hela ya NSSF kabla ya miezi sita (6) kupita?

Kama yupo naomba anifahamishe sababu alizotumia kupata.
 
Kwa kifupi hii nchi imeshaoza, kama una vijisenti vingi kidogo basi basi wakatie mpunga kadhaa wanakuandalia cheki ndani ya wiki moja, lakini kama unataka ukauzu zaidi ya dagaa inabidi umuone daktari mnayefahamiana naye akuandalia Medical report kwamba huwezi tena kufanya kazi kutokana na afya yako
That's only way u can do, otherwise benchmark ni six month.
 
Habari zenu wakubwa,
je kuna mtu yeyote ambaye amewahi kuchukua hela ya NSSF kabla ya miezi sita (6) kupita?

Kama yupo naomba anifahamishe sababu alizotumia kupata.

Iko hivi- Industries ambazo ukiacha au kuachishwa kazi unaruhusiwa kufungua madai yako papo hapo na ndani ya siku 21 unavuta vyako ni (MINING) Ila kwingineko inabidi utulia kwanza mpaka ipite miezi sita ndo ufungue madai yako.Unatakiwa uwe na vielelezo vifuatavyo- kadi ya uanachama, Barua ya kuachishwa au kujiuzulu kazi, na form inayonyesha michango yako toka kwa mwijiri wako.
 
Mbona kwenye usajili hawatuambii subili miezi sita ndo uanze kuchangia?
Yaani ela yangu mumeizungusha weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee leo nataka ichukua mnanipa masharti na mbaya zaidi pamoja na kuizungusha kote uko ata faida sipati
 
na kadi pia inabidi ubadilishiwe upatiwe smart card kama unayo ya zamani,
jamaa kwa kweli ni matata sana, kabrasha zako zikiwa sawa unaambiwa urudi baada ya wiki mbili waverify hizo kabrasha zako kama zipo sawa unapewa siku 21 ndio uje kuchukua cheki yako,
mimi nimeacha kazi september mpaka leo nafatilia, nimesema rushwa sitoi ng'o
pesa yamgu washaifanyioa biashara halafu niwape na hongo hiyo GUMU sanaaa,
 
Kwa kifupi hii nchi imeshaoza, kama una vijisenti vingi kidogo basi basi wakatie mpunga kadhaa wanakuandalia cheki ndani ya wiki moja, lakini kama unataka ukauzu zaidi ya dagaa inabidi umuone daktari mnayefahamiana naye akuandalia Medical report kwamba huwezi tena kufanya kazi kutokana na afya yako
That's only way u can do, otherwise benchmark ni six month.

naomba kuuliza kama na mimi naweza kupata haki yangu kutoka nssf japo mimi nilifanya kazi zidi ya mwaka mmoja ila niliachakazi bila taarifa na kuondoka kazini japo ni muda mrefu sana tangu niache kazi.

inakuwaje hapa naweza kupata mafao yangu kipindi niko kazini.
 
Haki ya mtu haipotei ndugu yangu, huchelewa tuu. Nenda NSSF kachukue fom ya madai ila unatakiwa uwe na barua ya kuacha kazi na picha 5 za size ya pasport.
Barua waweza kuidraft tuu sio ishu.
then wakati wa kuipeleka ile fom kwenye kampuni uliyoacha kazi usiambatanishe na ile barua.
Wakikuzingua rudi NSSF kawaambie then wao wataandaa barua kwa mwajiri wako wa zamani kisha mwajiri wako atakujazia madai yako bila tatizo kwani ni kosa kubwa sana kwa mwajiri kutotoa ushirikiano kwenye madai ya mafao kwa mfanyakazi wake aliyeacha kazi kwake.
Baada ya hapo utavuta mkwanja wako.
I'm waiting for my 10%.
 
Bwana Njowepo nimependa sana coment yako mim pia nimeajiriwa ila naumia sana unachangia hela halafu baada ya miaka 20 unapewa hela ileile bila interest.where is value for money Watanzania tumelala sana mim na wewe tunatakiwa tuamke tupinge hili Pole sana mhandisi wa umeme hii ndo Tzania yetu!!
 
na kadi pia inabidi ubadilishiwe upatiwe smart card kama unayo ya zamani,
jamaa kwa kweli ni matata sana, kabrasha zako zikiwa sawa unaambiwa urudi baada ya wiki mbili waverify hizo kabrasha zako kama zipo sawa unapewa siku 21 ndio uje kuchukua cheki yako,
mimi nimeacha kazi september mpaka leo nafatilia, nimesema rushwa sitoi ng'o
pesa yamgu washaifanyioa biashara halafu niwape na hongo hiyo GUMU sanaaa,

Du yan tupo pamoja, niliacha kazi august, ila ile kadi ya zaman nikawa nimeipoteza, nikaenda kuomba nyingine tangu january nimeipata Juzi!!! Yani hawa jamaa nimesema siwapi hata centi moja rushwa na pesa yangu watanipa! NSSF Morogoro imeoza, sijui ni kote au zipi? Yan nawaonea huruma wanaoingia NSSF sahivi!

Kurudi kwa swali lako la msingi, kuna njia mbili za kupata pesa zako fasta

1. report ya daktari kama mjumbe mmoja alivyoeleza
2. Form za kujiunga na shule (Chuo) kama unaenda kusoma unapewa pesa zako fasta coz utasema ndo ada yenyewe hiyo
 
Jamani NSSf mpoooo!
 
Habari zenu wakubwa,
je kuna mtu yeyote ambaye amewahi kuchukua hela ya NSSF kabla ya miezi sita (6) kupita?

Kama yupo naomba anifahamishe sababu alizotumia kupata.

ni nje ya utaratibu, labda uende na cheti cha daktari akionesha we ni mgonjwa na unahitaji matibabu nje ya nchi au ndani e.g. AIDS, figo, e.t.c
 
Jamani wana jf nimesoma maoni yenu yote kwa ujumla Nadhan tuna experience tofauti tofauti kwa wale mlojitoa NSSF na kudai haki zenu poleni kwa ma usumbufu..Ki msingi vijana wenzangu Najue wengi wetu hatuja elimishwa vya kutosha kuhusu Maana hasa ya Social Security..Lengo na madhumuni ni kwa ajili ya kujiwekea akiba pindi unapo pata majanga kama ya Uzee,Kumia kazini,Matibabu na kadhalika.Wa kuu swala la kujitoa uanachama ni risk kwako mchangiaji.In ma opinion Jamani vijana Tutumie fursa ya mifuko ya jamii kwa malengo ya mifuko hiyo kwa sababu wengi wetu tunao kimbilia hizo pesa zilizoko Nssf hatuzifanyii cha maana zaidi badae tunajuta najua wapo watakaosema"Pesa si zetu"yah ni zako but tuna mifano mingi watu wakuja kujuta badae...Na pia kumbuka mwajIri wako anakuchangia 10% na mwajiriwa 10% Vipi kama uakuja kujitoa Ulipwe 10% yako ulochangia?Acheni kuwa selfish Kama huta pata mafao yako wategemezi wako watapata...Mi nacho washauri Tuchangamkie Fursa za mifumo ya social security iliopo ili tuweze kujikinga na majanga na kwa ambae Tayari yupo Nssf ahakikishe anapata na kujiandikisha kwenye Fao la matibabu ili Atibiwe bure yeye na Familia yake....Mwisho mafao ni Haki yako its not a privilege Hivyo huna haja ya kutoa kitu chochote ili upate haki hiyo na kama utatoa basi umejizulumu....
 
Huu wangu ni ushauri tu kwa vijana wenzangu ambao bado tuna muda mrefu siku za usoni kuweza kufanya kazi/kuajiriwa!! Assume hivi sasa umeacha au kufukuzwa kazi au kitu chochote sawa na hayo! And, kwa sasa ni member wa NSSF huku ukisotea mafao yako na hujui utayapata lini.......!! In short, ktk hali ya kawaida, fao la kujitoa NSSF unaanza ku-claim after six months! So, kama utapata ajira sehemu nyingine, then fikiria haya yafuatayo:

1. Salary yako kwenye ajira mpya!
Hili ni muhimu sana kuangalia ili kufanya uamuzi wa busara ujiunge na mfuko gani. Kama mshahara wenyewe ndio hii mishahara yetu mingi ambayo, inapotokea kufukuzwa au kuacha kazi tu; basi on the same month unakua katika hali mbaya; basi ogopa NSSF kama ukoma! Unakuta mtu anapata basic ya TZS 600,000/=! Mtu kama huyu simtarajii kama anaweza kufanya savings ya kutosha itakayomwezesha ku-survive for six more months bila kazi. So, mtu kama huyu anapofukuzwa kazi ama mkataba wake kwisha, then kuna uwezekano mkubwa hayo yakamkuta wakati hata laki tano hana kwenye akiba yake!! Na unapoenda NSSF kuchukua chako, utaambiwa usubiri miezi sita wakati akiba uliyonayo ni ya kukuwezesha ku-survive mwezi mmoja! Na kumbuka, hiyo miezi sita ni kwa ajili ya kufungua madai, so cash money itaingia mkononi mwako at least seven months tangu utoke kazini! Kwahiyo, katika mazingira kama hayo basi iogope NSSF kama ukoma!
In contrast, kama salary yako inaweza kukuwezesha ku-save amount ya kutosha; kwamba at any given month, basi unaweza uka-save angalau TZS 300,000/=, then NSSF is best for you! WHY? In short ni kwamba, pale mkataba wako unapoisha au kufukuzwa basi kuna uwezekano ukawa umejiwekea akiba ya kutosha kidogo kukuwezesha ku-survive kwa miezi sita zaidi! Kuna uwezekano ukaja kupata mpunga wako wakati ndo unaanza kutaka ku-collapse na hivyo kuwa na additional months za kuweza ku-survive wakati unatafuta mchongo mwingine! Unless kama u've entrepreneurial ability, kujiunga mifuko inayotoa mafao mapema si busara endapo mshahara wako ni mzuri!! Sizani kama nimeeleweka....!! Assume mshahara wako ni mzuri to the point kwamba mkataba wako unaisha huku una akiba ya angalau TZS 2,000,000/= in your bank account. Na good enough, upo kwenye mfuko ambao unatoa mafao ya kujitoa kwa haraka zaidi; say within 3 months! Hii maana yake ni nini? Ni kwamba utalipwa mafao yako wakati bado una akiba ya kutosha. Ama kwa lugha nyepesi, badala ya mafao yako kuanza kuingia kwenye mkondo wa matumizi seven months after kuacha kazi(from NSSF), sasa mafao hayo yataingia kwenye mkondo wa matumizi only after three months! Hapo ni kwamba, hata kama ni kuashiwa basi utaishiwa mapema zaidi kwavile umechukua mpunga mapema zaidi!

BUT, kwavile mishahara mingi ni midogo sana, basi jambo la maana ni kuigopa NSSF!
 
Du yan tupo pamoja, niliacha kazi august, ila ile kadi ya zaman nikawa nimeipoteza, nikaenda kuomba nyingine tangu january nimeipata Juzi!!! Yani hawa jamaa nimesema siwapi hata centi moja rushwa na pesa yangu watanipa! NSSF Morogoro imeoza, sijui ni kote au zipi? Yan nawaonea huruma wanaoingia NSSF sahivi!

Kurudi kwa swali lako la msingi, kuna njia mbili za kupata pesa zako fasta

1. report ya daktari kama mjumbe mmoja alivyoeleza
2. Form za kujiunga na shule (Chuo) kama unaenda kusoma unapewa pesa zako fasta coz utasema ndo ada yenyewe hiyo

daaah mkuu umesema kweli, hapo NSSF moro kumeoza kabisaaaaa, kuna shemeji yangu anafuatilia mafao ya mumewe toka mwaka 2009 mpaka leo bado hajapewa mwezi huu ameenda ameambiwa form zimepotea aanze tena upya, pumbaafu, yani wanakera kweli
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom