Naomba kujua kiasi kilichopatikana jana kwenye harambee ya CHADEMA

Tangu lini michango ikawa siri wakuu? Mbona wakati wa kuchangia watoaji wanatamka wazi kila mtu anasikia? Leo iweje ikisha kusanywa ndo iwe siri ya chama? Hapo kutakuwa kunafanyika uchakachuaji.

JK naona avatar yako unatuonyesha chama chako ccm kinavotafuna na kuharibu maisha ya wananchi. Kuhusu kuchakachua nafikiri umesahau michango ni ya CDM sio ccm kunakofanyika uchakachuaji baada ya mafisadi kuchangishwa pesa. Si unajua tena ngoma droo mafisadi wanaibia serikali ya ccm. Wakichanga pesa mafisadi ccm inawaibia tena fedha walizochanga. Yaani ni nyumba ya panya wote wezi; mtoto, mjomba, mamamkwe, mzee wa mji, watoto, shangazi, mjukuu kama wewe hadi na wageni nao wezi.
 
Waliotoa majibu humu sio wasemaji wa chama,sasa kwa nini muanze kuonyesha gadhabu juu ya chama?

Watu wanakurupuka tu. Jibu linatolewa na kibaraka wa ccm anayejifanya kuisemea CDM bila kutafakari watu wanaingia kichwa kichwa wakifikiri ndio majibu ya CDM.
 
Tangu lini michango ikawa siri wakuu? Mbona wakati wa kuchangia watoaji wanatamka wazi kila mtu anasikia? Leo iweje ikisha kusanywa ndo iwe siri ya chama? Hapo kutakuwa kunafanyika uchakachuaji.

Haihitaji kuwa na elimu ya degree kufahamu kwamba wewe ni mlalamishi yani hata siku mbili hazijapita unalalamika hujatangaziwa kilichopatikana,CDM hawawezi kuwa na upeo finyu kiasi hicho washindwe kutambua kuwa wananchi wanahitaji kujua walichokichangia tusubiri
 
fedha......njia mojawapo ya kibomoa chama! mmechagua fungu la kujibomoa vizuri
 
Kinchotakiwa ni " latest available figure". wangeweza kusema mpaka jana jumapili ni kiasi hiki kipepatikana na watu wanendelea kuchangia. kimya kinaleta sura mbaya. tuwe wakweli tuache unafiki
 
Haya ni maajabu, michango tutoe wengine, halafu ufuatiliaji na uchangiaji wa hoja unafanywa na watu wa magamba ambao walitoa povu wiki nzima kujaribu kututisha tusichangie. Mbona nyie magamba kuna watu tuliambiwa wamepita kwa wahindi kukusanya hela lakini hatujaambiwa kiwango kilichopatikana wiki ya pili sasa??
 
We have managed to collect a total of Tshs 200m and thus Magwandraa would like to thank you all for your unmatched generosity. Two-thirds of this money will be allocated for Club Billicanas repairs while the remaining amount will be designated for Mr. Mbowe's private house maintenance and Mrs Mbowe's Easter shoppings. Also be informed the next fundraiser, which has wholly been dedicated to Dr. Slaa's new bungalow construction, is due to take place early April in Dodoma.

another gamba using masaburi for thinking.
 
Chadema viongozi wangu mnataka kutia doa imani ya wananchi kwenu.
au ndo 2nazidi kuwa vipofu
toeni amount watu tuzidi kuwaamini.
KIPIMO CHA UONGOZI NI SAMBAMBA NA U-SHARP KTK MAMBO YA FEDHA.

LOVE YOU CHADEMA.
 
We have managed to collect a total of Tshs 200m and thus Magwandraa would like to thank you all for your unmatched generosity. Two-thirds of this money will be allocated for Club Billicanas repairs while the remaining amount will be designated for Mr. Mbowe's private house maintenance and Mrs Mbowe's Easter shoppings. Also be informed the next fundraiser, which has wholly been dedicated to Dr. Slaa's new bungalow construction, is due to take place early April in Dodoma.

mtu aliyerogwa na kulaaniwa huwa hana pointi na badala yake huwa anaropoka tu as hajui anachokifanya!
 
Chadema kila kikiendelea kinatutisha, kinatufanya tufikiri mara mbili kuwa chama hiki kinaweza kushika mamlaka na nchi kuwa kwenye amani

chadema kimekuwa ni chama kinachopingana na misingi ya uwazi na demokrasia, nnashangaa sana kuona chama mabacho niliamini kuwa huenda kitatuvusha hapa tulipo, kikiwa na sera za kibabe na kufikicha demokrasia.

nnawaomba wanachadema kuanzia juu hadi chini kuchukua hatua za haraka kurudi kwenye mstari.

nimeshangazwa kuona Ndugu Zitto kabwe alipoamua kutoa mawazo yake, watu wametukana na kumwita kibaraka. hivi hiki si ndio chama ambacho tuliamini kuwa kiko tofauti na CCM ? kuna uhuru wa kujieleza?

kuhusu masuali ya pesa chama makini kinatakiwa kiwe wazi ili kila mtu aamini kweli hiki chama kina uwazi na kina mipango thabiti, na hili litawasaidia kushawishika kukipa kura kuongoza nchi

kinyume chake wananchi mtaendelea kuwatisha na kuamini hiki ni chama hatari na cha kuogopwa

kama mtu umekosa pesa ya matumiz na mkavurumishana na mkeo bora ukae uwanjani kuliko kutuletea huu uchafu huu!
 
Back
Top Bottom