sina mchango! kinachoangaliwa hapa ni maamuzi ya kijinga yanayofanywa na viongozi wetu, mfano lowasa na kikwete waliwahi kusema mikopo itolewe kwa wanafunzi waliopata form six division one na two only. je wao waliweza kuzipata izo wakati wao? mtoa mada hajakosea anajaribu kupima watu kwa kipimo walichokiweka wenyewe. ccm kusema kuwa mgombea wa urais awe amemaliza chuo kikuu, kipimo kinachofuata je kwa kiwango gani? haijalishi una diploma au degree bado unaweza kuwa kiongozi mzuri, ila ukianzaa kuboronga kama jk itabidi tukupime kwa kipimo chako unachostahili