Naomba kufahamu kuhusu Vyura wa Kihansi

Nenda Chuo kikuu UDSM kwenye captive breeding facility jirani na jengo la Molecular biology (?) utawaona hao vyura.

ikiwa wewe ni mpenda mazingira it is worth your time utapata kujifunza mengi.
 
Stupid government.Najuta kuwa mwananchi wa nchi hii.Vitu adimu duniani ati wanawapeleka marekani.Sasa mtalii atakuja kufanya nini Tanzania kama vyura hao wako America?Wanyama wa kila aina wameibiwa bila kumeasure impact.Watalii watakuja kufanya nini endapo vitu adimu kama hivyo vinapelekwa nje?Unazuia vitu wizi wa vyura huu.Hati miliki ikoje??Na mbaya zaidi sio wizi pia ni kwa namna gani afya yao haiwezi kuwa intoxicated na hata kumaliza hiyo spicy kabisa??Watu wangapi wanakosa ajira endapo watalii na kuja kuwatazama watapungua??Inaathiri vipi pato la mtu mmoja mmoja,familia na taifa??Tanzania ina laana maana hata vitabu vinasema natural resources can be curse or blessung.For us it is a curse.
 
Kama umesoma historia ya nchi hii Wazungu walichukua mmea wenye jina la "busy lizzie" ambao ni ornamental (wa mapambo). Walipochukuwa haukuwa na thamani yo yote katika Milima ya Usambara lakini leo huko Ulaya mmea ule ni biashara ya maelfu ya madola na maeuro. Na Tanzania kama nchi imeambulia nini? Zeeeeeeeero. Angalia na vipepeo vya hapo hapo kwenye milima ya Usambara leo ni biashara kubwa sana na miaka michache tu nyuma havikuwa na thamani yo yote. Angalau kwenye vipepeo kidogo watu walikuwa wameamka na ndio tunapata kamgao kadogo.

Kama Mwenyezi Mungu ameamua kumuweka chura huyu wa kipekee duniani hapo Kihansi lazima anazo sababu zake, kwa nini sisi binadamu ndiyo tuwe mstari wa mbele kuwamaliza? Leo tukimmaliza chura huyo, kesho Sanje mangabay (kima wa kipekee kwenye milima ile) na keshokutwa mwengine na mwengine......... hatimae tutakuwa weupeeeeee

Lazima tuhifadhi bioanuwai aliyotujaalia Mungu
Lazima tuhifadhi mazingira na hasa yale yenye viumbe adimu duniani. Siku moja kama sio sisi basi hata wajukuu zetu watakuja kuona faida zake. Na tukiharibu watakuja kutulaani.

Umeandika ya kumliza mtu kwa kweli. Kwa wanaopenda raslimali ya nchi yetu na vivutio, hivi tutakuwa wajinga miaka yote? Zamani mababu walibadilisha taa kwa almasi leo wanabeba kila kitu, hayo maua ya busy Lizzie ni kama 7000 ya tz kwa bunch bora hata tungekuwa tunatuma mauwa badala yake ulaya siku hizi kila mtu anapanda ingawa mbegu zake ni ngumu kuota wanalazimisha tu.
 
Ndugu wanajukwaa tafadhali sana naomba mnijuze kama wale vyura wetu wa rangi ya kijani waliochukuliwa kutoka Kihansi na kupelekwa Marekani kwa ajili ya uchunguzi washarudishwa hapa nchini au bado wapo marekani wanaendelea kufanyiwa utafiti. Maana mkuu wa kaya aliyeruhusu wapelekwe huko karibu anaachia kaya (ikulu) hivyo nimeona ni vyema kufuatilia na kumkumbusha kuhusu hizo rasilimali zetu mapema kabla hajang'atuka! NAWASILISHA HOJA!
 
Ndugu wanajukwaa tafadhali sana naomba mnijuze kama wale vyura wetu wa rangi ya kijani waliochukuliwa kutoka Kihansi na kupelekwa Marekani kwa ajili ya uchunguzi washarudishwa hapa nchini au bado wapo marekani wanaendelea kufanyiwa utafiti. Maana mkuu wa kaya aliyeruhusu wapelekwe huko karibu anaachia kaya (ikulu) hivyo nimeona ni vyema kufuatilia na kumkumbusha kuhusu hizo rasilimali zetu mapema kabla hajang'atuka! NAWASILISHA HOJA!

washazamia usifanye mzaha na kwenda ng'ambo
 
Njowepo na Bona, sikujua kama kweli kuna watu katika JF ambao hawajui maana ya kutunza mazingira na viumbe wake katika karine hii. Kusema kweli kama mwana ecolojia ni meshangaa sana kuona hamjui faida ya kuwatunza vyura hao. Mngekuwa mmetembea kidogo nchi kama Misri naona mngesgaa kuona jiwe la picha ya Sphinx ambalo japo limemomonyoka lakini linatunzwa kama lulu. Na watu wana miminika duniani kuja kuliangalia na nchi ya Misri inapata watalii wengi sana. Ushauri wangu ni kwamba muende shule ili mjue maana ya utunzaji mazingira. Kama ni umaskini unaletwa na mambo mengine lakini sio vyura vya kihansi.

Mkuu hasante umejitaidi sana kupangua hoja zao kwa fact.....yaani kuendeleza kitu eti ni kuleta umasikini jamani!!!
 
Je baada ya vyura wa kihansi kurudishwa TANZANIA, unadhani bado wataendelea kuwa vyura wanaopatikana TANZANIA pekee?


"Vyura wa Kihansi wamerudishwa katika makazi yao ya awali. :Source TBC1 Habari 07th May 2018"

kihansi.jpg
images.jpg
 
Waliwachukua makusudi ili wakazalishwe wengi
Yaani kama wanaweza kuibiana technology watatuachia wanyama wetu salama.
Wameiba sana jamani na kuna watu wanawasaidia kuwachukua kabisa
Wewe weka nyani nyumbani uone msala wake lakini wao watatoa mpaka cloned
 
Je baada ya vyura wa kihansi kurudishwa TANZANIA, unadhani bado wataendelea kuwa vyura wanaopatikana TANZANIA pekee?


"Vyura wa Kijansi wamerudishwa katika makazi yao ya awali. :Source TBC1 Habari 07th May 2018"

View attachment 769546View attachment 769547
Japo haielezwi ila ukweli ni kuwa vyura hao waligoma kuzaliana ugenini. Hiyo ndiyo sababu ya kuwarudisha. Kwa hiyo usiwe na shaka kwamba watapakaa huko ughaibuni.
 
Mkuu hao VYURA ni kweli WANA RANGI YA NJANO ? au unamaanisha VYURA FC? isije ikawa unaleta LUGHA YA PICHA ,,,NA tafakari KICHWANI kwako
 
Back
Top Bottom