Naomba kufahamu kuhusu Vyura wa Kihansi

Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,323
18,793
Wadau naomba anaejua habari za hawa vyura anihabarishe, nikimaanaisha ni wa nini, faida zao na ni kwa nini wamekuwa maarufu hivyo...nimesikia wanazaa but sijajua haswa kama umaarufu wao ni shauri hiyo...jana nimewaona wakishuka kutoka kwenye KLM na escort ya kutosha wakitokea Marekani..je ilikuwa ni lazima waende Marekani?.....:A S-confused1:

=====

Unafahamika kama Mto Kihansi ambao unafanya maporomoko katika milima ya Udzungwa unaoanzia Mufindi na Kilolo mkoani Iringa. Mto huu humwaga maji yake katika Bonde la Kilombero, Morogoro.

Eneo hilo la milima lina sifa nyingi za uhifadhi, lakini kupatikana kwa vyura aina ya nectophrynoides asperginis mwaka 1996 ambao walipachikwa jina la vyura wa Kihansi, kumelifanya liwe la kipekee ulimwenguni.

Upekee huo unapambwa na ukweli kuwa vyura hao ni kati ya viumbe ambao wanapatikana Tanzania pekee na wapo katika orodha ya viumbehai walio katika hatari ya kutoweka.

Kutokana na hali hiyo Vyura wa Kihansi wapo katika orodha ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanyama na Mimea iliyo Hatarini Kutoweka (Cites), hivyo hivi sasa wanalindwa kisheria na ni mafuruku kuwauza sehemu yoyote duniani.

Sifa za kipekee

Awali haikufahamika vyura hao kuwapo katika eneo hilo mpaka mradi wa uzalishaji wa megawati 180 za umeme ulipoanza kutekelezwa katika bonde hilo mwaka 2006.

Viumbehai hao, wanaishi kwenye mazingira ya maji yanayotiririka na kutoa mvuke mwingi unaosababishwa na nguvu ya maji. Sifa yake kuu ni kutaga mayai na kukaa nayo kwenye kifuko kilichopo ndani yake hadi muda wa kuanguliwa unapofika.

Wakati ukifika vyura hao hutoa vitoto hai hali ambayo kisayansi hutafsiriwa kuwa ni kuzaa. Kutokana na ukweli kuwa hatagi mayai yakaonekana, ni dhahiri kuwa vyura wa jamii ni tofauti na jamii nyingine duniani ambao hutaga mayai yanayoonekana.

Vyura wa kawaida hutaga mayai na kuyaacha majini yakielea katika utando na kisha huanguliwa wakati unapowadia, lakini wa Kihansi huangulia tumboni.

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake zimeandaa mradi wa awamu ya pili wa miaka mitano ya utunzaji wa mazingira katika Bonde la Mto Kihansi ambao unasimamiwa na Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC).

Wadau wengine ni Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri), Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (Sua), Benki ya Dunia (WB) na mashirika wahisani lengo likiwa kurudisha uoto wa asili uliokuwepo ili kuwafanya vyura hao waishi katika eneo lao hilo la asili.

Kulingana na vyanzo mballimbali, vyura wa Kihansi alitangazwa rasmi kuwa ametoweka katika mazingira yao ya asili Novemba 2009 na chanzo kikuu kikitajwa kuwa ni ujenzi wa bwawa la umeme la Kihansi mwaka 1999/2000.

Matumizi ya maji

Bwawa hilo linaelezwa kutumia karibu asilimia 90% za maji yaliyokuwa yanapita ndani ya makazi ya vyura na Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa uhifadhi wa mazingira kama Wildlife Conservation Society na Benki ya Dunia ikafadhili mradi wa awali kuwanusuru vyura wa jamii hiyo.

Katika utekelezaji wa mpango huo, vyura wapatao 500 walipelekwa katika Chuo Kikuu cha Colorado nchini Marekani na jitihada zikifanyika kufufua makazi yake ya asili ambayo yaliathiriwa na utekelezaji wa mradi huo wa umeme. Mtafiti na mhitimu wa Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Hawaii cha Mareka, Devolent Mtui anasema mfumo bandia ulizalisha vyura zaidi ya 20,000 kutoka 1,200 waliokuwepo mwaka 2003.

Mtui ambaye alifanya kazi katika mradi wa awamu ya kwanza wa Usimamizi wa Maendeleo ya Maporomoko ya Kihansi ambao ulikoma 2011, anabainisha kuwa mwaka 2009 vyura hao ghafla walitoweka. Anasema taarifa za wataalamu zinataja sababu za kutoweka kwao kuwa huenda zinasababishwa na aina fulani ya fungus, waitwao chytrid au kemikali zinazotokana na mbolea zinazotumiwa na wakulima kwenye vyanzo vya maji yanayotiririka katika mto huo.

Anaongeza kuwa vyura waliopelekwa Marekani wameendelea kuzaana na kwa mujibu wa mkurugenzi wa mipango na utafiti wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), Fadhila Khatibu hadi sasa vyura 3,000 wamerudishwa.

Khatibu anasema baadhi ya vyura hao wamehifadhiwa Chuo Kikuu Dar es Salaam na wengine walirudishwa kwa awamu wapo katika makazi yao ya asili.

Anaongeza kuwa awamu ya pili ya mradi huo wa miaka mitano kuanzia sasa hadi Desemba 2018, utagharimu kiasi cha Sh5.98 bilioni na umelenga kukabiliana na changamoto za awali ambazo ni pamoja na elimu kwa wakazi wanaozunguka mradi.

Anasema: “Wakazi wa vijiji 30 vilivyopo katika wilaya tatu zinazozunguka mradi huo ambazo ni Mufindi, Kilolo na Kilombero wataelimishwa umuhimu wa kutunza mazingira ili kuwanusuru viumbe hao.”

Anasema elimu itahusu kupunguza matumizi ya maji kwa ajili ya shughuli za kilimo, kuzuia ukataji miti, utunzaji na uhifadhi wa mazingira ya eneo hilo na kuhakikisha maji hayo hayachafuliwi kwa shughuli za binadamu.

“Tunataka kupunguza matumizi ya maji kwa ajili ya shughuli za kilimo kwani mbolea na takataka nyingine zina athari kwa vyura hao na viumbe wengine wanaotegemea mto huo,” anasema na kuongeza kuwa kutakuwa na mashamba darasa pia.

Anasema mashamba hayo, ambayo yatasimamiwa na wataalamu wa masuala ya kilimo, yatatumika kuwafundisha wakulima wa maeneo hayo namna nzuri ya ulimaji ambayo haichafui uoto wa asili wa eneo hilo.

Meneja mwandamizi wa utafiti na mazingira wa Shirika la Umeme (Tanesco), Aaron Nanyaro anasema ingawa shirika lake linachohitaji ni kufua umeme kwa ajili ya shughuli za maendeleo, linatambua kuwepo kwa viumbe hao na kwamba linasaidia katika utunzaji wa mazingira.

Anasema kutokana na hali hiyo, shirika lake limepunguza mita za ujazo 1.5 ambazo zingeweza kuzalisha kiasi cha megawati 7 za umeme, ili kiasi hicho cha maji kiende kwa vyura hao, pia kuna mashine za kisasa za kutawanya maji hadi katika makazi ya vyura hao.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Utafiti wa Wanyamapori (Tafiri), Simon Mduma anasema anasema Serikali imeingia mikataba mingi ya kimataifa ya uhifadhi na kuhakikisha uwepo wa viumbe walio hatarini kutoweka, lakini mafungu kwa ajili ya utafiti ni tatizo.

Anasema awali walipewa jukumu la utafiti wa kuwepo kwa vyura hao, kuwezesha wawepo, uhifadhi wa Kihansi, kiwango cha maji, utafiti wa viumbe wengine wanaopatikana Kihansi na utafiti wa upunguzaji wa kiasi cha dawa zinazotumika shambani.

Mduma anasema hata hivyo kiasi cha Sh. 250 Milioni walizoomba kwa kazi hiyo toka Serikalini, walipata pungufu hali ambayo iliwafanya wajikite katika eneo moja la kuwezesha kuwepo kwa vyura hao pekee.

Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira (Nemc), Boniventure Baya anasema kuzinduliwa kwa mpango wa awamu ya pili wa miaka mitano wa uhifadhi wa bonde hilo, umelenga kuwahakikishia vyura wapatao 5,000, wanapata sehemu salama ya kuishi.

Anasema uhai wa vyura hao unategemea ushirikiano na wadau ambao watafikiwa na mradi huo wakiwemo wakulima ambao matumizi yao ya maji na viwango vya viuatilifu wanavyotumia, ndivyo vitu vya msingi ambayo vitawanusuru vyura hao.
 
Vyura wa Kihansi wanapatikana Kihansi tu duniani kote. Kihansi iko Iringa kwenye milima ya Udzungwa.

Walipelekwa USA baada ya kujenga ule mtambo wa umeme wa Kihansi. Hvi majuzi ndio wamerejeshwa kwa vile wamepotea kule kwenye makao yake ya asili Kihansi.

Vyura hawa wadogo huwa wanazaa vijitoto na sio kutaga mayai kama vyura wengine.

Inawezekana tusijue faida yao kwa sasa lakini hivi karibuni kuna aina fulani ya vyura ambao wanafanyiwa utafiti wa dawa fulani.
 
Hawa vyura kama wana manufaa na binadamu wangeachwa Marekani nchi hii ni masikini na nilisikia serikali ilikuwa inalipa zaidi ya dola laki mbili kila mwaka kuwatunza huko hela ambazo zingetumika kwenye afya ya kina mama wajawazito hapa kwetu.
 
hapo ndio nashindwa kuelewa kwa nini wana gharama namna hiyo
 
Vyura wa Kihansi wanapatikana Kihansi tu duniani kote. Kihansi iko Iringa kwenye milima ya Udzungwa.

Walipelekwa USA baada ya kujenga ule mtambo wa umeme wa Kihansi. Hvi majuzi ndio wamerejeshwa kwa vile wamepotea kule kwenye makao yake ya asili Kihansi.

Vyura hawa wadogo huwa wanazaa vijitoto na sio kutaga mayai kama vyura wengine.

Inawezekana tusijue faida yao kwa sasa lakini hivi karibuni kuna aina fulani ya vyura ambao wanafanyiwa utafiti wa dawa fulani.
mbona unanichanganya??? ina maana hata huko walipohifadhiwa marekani nako hawapatikani??
 
Wadau naomba anaejua habari za hawa vyura anihabarishe, nikimaanaisha ni wa nini, faida zao na ni kwa nini wamekuwa maarufu hivyo...nimesikia wanazaa but sijajua haswa kama umaarufu wao ni shauri hiyo...jana nimewaona wakishuka kutoka kwenye KLM na escort ya kutosha wakitokea Marekani..je ilikuwa ni lazima waende Marekani?.....:A S-confused1:

Preta hili la Kihansi ni funzo lakini Watanzania tumeshasahau na sasa tunataka kuleta madhara mengine Serengeti kwa ujenzi wa highway.
Ni hivi wale vyura ni endemic kwa Tanganyika (wanapatikana kwa asili Kihansi tu!). Kipindi kile tulipolazimishwa HOJA ZA NGUVU na wanasiasa nchi yetu iliingia mkenge kujenga hydro power plant pale Kihansi. Wana-ikolojia walijaribu kutoa sababu kwa nini zoezi hilo linaweza kuleta madhara lakini wenye mamlaka waligoma kusikia. Sasa kilichotokea ni kuwa watafiti wakaomba baadhi wa vyura hao wapelekwe Marekani kutunzwa katika modified environment inayofanana na Kihansi. Hivyo shehena ya vyura ilipelekwa Marekani kuhifadhiwa na kufanyiwa utafiti zaidi.

Huku nyumbani baada ya lile bwawa kujengwa haikupita muda tatizo likajitokeza. Kutokana na maji yale kusimama kwenye bwawa ilisababisha kuzuka au kuongezeka wa aina fulani ya fungi. Hawa fungi wakasababisha aina fulani ya magonjwa ambayo iliwashambulia wale vyura almost wote wakafa. Kwa hivyo mpaka sasa hakuna vyura wale tena katika eneo la Kihansi (i stand to be corrected!). Majaribio yakafanyika kuwarudisha wale vyura Kihansi lakini hayakuwa successful kwa vile wale fungi waliendelea kusababisha madhara.

Sasa basi kinachofanyika sasa ni kuwarudisha stagewise kwa kumodify habitat i.e. vyura walioko kwenye modified environment ya awali huko Marekani wanabadilishiwa mazingira kwa mpangalio maalumu ili kuwaongezea immunity na pia resilience kwa wale fungi. Hivyo wakionekana kustahimili kuishi bila madhara then ndio wanaletwa Tanzania.

Kwa hivyo Preta kwa kifupi hiyo ndio historia ya vyura wa Kihansi (wanasiasa hawapendi mjue, walijaribu kusema wakati ule binadamu kupata umeme ni bora kuliko vyura; matokeo yake umeme wenyewe bado shida na vyura tumeshawaharibia mazingira yao).

Now, STOP SERENGETI HIGHWAY!
 
Kwetunikwetu umenena ya ukweli kabisa, wewe kwa kweli ni mwana mazingira.

Bwana Acid ukitaka kumwona chura wa Kihansi kabla ya hivi majuzi ni kwamba ulilazimika kupanda ndege na kwenda kwenye zoos huko Marekani. Huko walikohifadhiwa ni kwenye zoos kwenye mazingira ya kutengenezwa na sio makazi yao ya asili ambayo ni Kihansi.

Tulilojifunza ni kwamba lazima kufanyike tathmini nzuri ya mazingira na kuweka mpango mzuri wa kuhifadhi mazingira (environmental management plan) kabla ya kuruhusu miradi mikubwa ya maendeleo kama ya barabara au hydro power.

Mwenyezi Mungu ameamua kumuweka chura yule huko Kihansi peke yake, lazima alikuwa na maana yake ijapokuwa sisi binadamu bado hatujaweza kutambua hilo. Mwenyezi Mungu hakika amejaalia milima ya Udzungwa kuwa na aina nyingi za viumbehai ambavyo ni adimu na hupatikana katika maeneo hayo tu - ni bahati iliyoje!

Na ndio maana Wazungu kila leo wako huko wanafanya utafiti na sisi wenyewe tumelala kabisa.
 
Gonga Hapa Kuwasoma vyema.

1213639746OPComment2kihansiToad.jpg
 
Preta hili la Kihansi ni funzo lakini Watanzania tumeshasahau na sasa tunataka kuleta madhara mengine Serengeti kwa ujenzi wa highway.
Ni hivi wale vyura ni endemic kwa Tanganyika (wanapatikana kwa asili Kihansi tu!). Kipindi kile tulipolazimishwa HOJA ZA NGUVU na wanasiasa nchi yetu iliingia mkenge kujenga hydro power plant pale Kihansi. Wana-ikolojia walijaribu kutoa sababu kwa nini zoezi hilo linaweza kuleta madhara lakini wenye mamlaka waligoma kusikia. Sasa kilichotokea ni kuwa watafiti wakaomba baadhi wa vyura hao wapelekwe Marekani kutunzwa katika modified environment inayofanana na Kihansi. Hivyo shehena ya vyura ilipelekwa Marekani kuhifadhiwa na kufanyiwa utafiti zaidi.

Huku nyumbani baada ya lile bwawa kujengwa haikupita muda tatizo likajitokeza. Kutokana na maji yale kusimama kwenye bwawa ilisababisha kuzuka au kuongezeka wa aina fulani ya fungi. Hawa fungi wakasababisha aina fulani ya magonjwa ambayo iliwashambulia wale vyura almost wote wakafa. Kwa hivyo mpaka sasa hakuna vyura wale tena katika eneo la Kihansi (i stand to be corrected!). Majaribio yakafanyika kuwarudisha wale vyura Kihansi lakini hayakuwa successful kwa vile wale fungi waliendelea kusababisha madhara.

Sasa basi kinachofanyika sasa ni kuwarudisha stagewise kwa kumodify habitat i.e. vyura walioko kwenye modified environment ya awali huko Marekani wanabadilishiwa mazingira kwa mpangalio maalumu ili kuwaongezea immunity na pia resilience kwa wale fungi. Hivyo wakionekana kustahimili kuishi bila madhara then ndio wanaletwa Tanzania.

Kwa hivyo Preta kwa kifupi hiyo ndio historia ya vyura wa Kihansi (wanasiasa hawapendi mjue, walijaribu kusema wakati ule binadamu kupata umeme ni bora kuliko vyura; matokeo yake umeme wenyewe bado shida na vyura tumeshawaharibia mazingira yao).

Now, STOP SERENGETI HIGHWAY!

asante sana kwa taarifa hii....its really weird
 
.... Kwa hivyo Preta kwa kifupi hiyo ndio historia ya vyura wa Kihansi (wanasiasa hawapendi mjue, walijaribu kusema wakati ule binadamu kupata umeme ni bora kuliko vyura; matokeo yake umeme wenyewe bado shida na vyura tumeshawaharibia mazingira yao)..

Ona lile neno limerudia tena .... wanasiasa ....! Lakini sikuhizi si Wanasayansi mbona wengi mjengoni???!!
 
suala ni priority, hata wakiwa extinct so what? kuna vyura wangapi duniani na wana faida gani?
 
Tunalipa ela zote izo kwa ajili ya kuwatunza vyura,nchi imekosa vipaumbele hii.
Mfano wakipotea what do we loose katika dimbwi hili la umaskini.
Unaweza kuta huko USA wamewabakiza wachache ili nao wawaite vyura wa KIUSA
 
Nilishafika kihansi kama mmoja wa hao watafiti ambao walipewa kazi ya kuangalia, 1-Kama hao vyura bado wapo, 2- Kuona kama fungus ambao ndio chanzo cha kufa kwa hao vyura pale Kihansi bado wapo. Nilikaa siku 7 pale camp na nikapanda kule goji kutafuta hao vyura usiku na mchana bali tulikuta vyura wengine wengine tu, tulichofanya ni kuchukua swab ya wale vyura tuliochokua ili tuweze kujua kama nao wameadhiliwa na hao detrimental fungus. Utafiti bado haujakamilika na utachukua muda mrefu sana na ndipo serikali ikaamua kurudisha hai vyura baada ya kujenga aquarium pale UDSM. Kule marekani Boston wale vyura waliakuwa kwenye aquerium ambazo ni fungus free kwa hio walinusuriwa wasipotee kwani hawa ni unique species hapa duniani, na tulikuwa tunawalipa wamarekani kwa kuwafuga hao vyura dola laki 2 kwa mwaka ndipo JK akaamuru warudishe Tz. Pale UDSM pamejengwa aquerium kama zile za marekani kwa hio hao vyura waliokuja juzi watawekwa pale, hio aquarium ina kila kitu sawa na kihanzi yaani AC, water sprashes na Drosophia(wadudu) kama chakula chao.
 
Back
Top Bottom