Naomba Jukwaa la MALENGA liwepo hapa...

Magulumangu

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
3,047
452
Mkuu Admin, kwa huzuni na taadhima, naomba kama upo uwezekano liwepo JUKWAA la Malenga maana wapo wengi na wenye uwezo wa kupanga verse kwaetu sisi twawaita wazee wa VINA na VISHARI, kuna jukwaa la Lugha, Mapenzi, Siasa na mengine mengi tu, Je malenga wavinjari wapi?...Nawakilisha tu...
 
Naunga mkono hoja, jukwaa liwepo hapa
Nasi sote kwa pamoja, mashairi kuyatupa
kwa wale wenye vioja, na wale walio supa
Tuwekeeni jukwaa, tupate kuwa wachuja
 
Hujaona jukwaa la sports? Au!


Tofauti sana ipo, kati ya bata na kuku,
japo ndege si popo,njiwa nae mauluku,
gama beta naipo, japo alama si kuku,
nimeona la spoti, japo si jukwaa malenga,

tuje hata kwa vinywaji, soda maji pombe,
leta mbege milaji,magufuli lake pombe,
tembelea hata ujiji,gongo ndo yetu pombe,
nimeona la spoti,japo si jukwaa malenga.....
 
Naunga mkono hoja, jukwaa liwepo hapa
Nasi sote kwa pamoja, mashairi kuyatupa
kwa wale wenye vioja, na wale walio supa
Tuwekeeni jukwaa, tupate kuwa wachuja

tuwekeeni jukwaa, tupate kuwa wachuja,
tumulike hata vitaa,kwa vina visiochuja,
waje wenye gitaa,tarabu hata unguja,
Weka letu jukwaa, tupate pia jirusha....
 
Kuna jukwaa la Lugha ambako kuna mashairi lukuki yanajadiliwa na Malenga waliobobea ndani ya JF

Jukwaa la Lugha


Mkuu ukisea jukwaa la lugha ni sawa na Jukwaa la malenga hapo unakosea ila ndani ya mashairi ndo kuna lugha ya kujadiliwa, Mapenzi nayo ni Lugha ya moyo ndugu yangu hivyo nalo jukwaa lipelekwe huko?
 
Naunga mkono hoja, jukwaa liwepo hapa
Nasi sote kwa pamoja, mashairi kuyatupa
kwa wale wenye vioja, na wale walio supa
Tuwekeeni jukwaa, tupate kuwa wachuja

Wazo lako linatija, hakuna wakulipinga
Tutajitosa wajanja,kwa pamoja kujipanga
Modi tupe uwanja, tujitose kama kanga
Tuleteeni jukwaa malenga wapate nafasi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom