Naoma ushauri wa kununua gari

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
216
za week end wandugu;

wajameni, nimeanza kukamata ngawira huku majuu na Mungu akipend nikitia mguu bongo nitaendesha kamashine kangu binafsi ka kwanza maishani mwangu. sasa naomba mnisaudie kuhusu ununuzi wa gari kwa dar manake mambo hayo ya magari mie siyajui kabisa.

wengine wanasema ukienda zanziba utapata kwa bei nafuu zaidi, wengine wanasema ukiagiza kwenye mtandao linachelewa (obvious) na linanyofolewa vifaa bandarini hivo hasara tupu, wengine wanasema nikinunua kwenye show room za bongo, naweza kuchomekewa la wizi au lililofanyiwa usanii wa kubadilishwa taarifa muhimu ili lionekane jipya kumbe choka mbaya, wengine wanasema show room za dar bei mbaya sana. n.k.

sasa ukweli ni upi, mnanishauri nini, niagize, niende zenji ama nilambe hapo hapo show room za bongo?

ushauri tafadhari
 
za week end wandugu;

wajameni, nimeanza kukamata ngawira huku majuu na Mungu akipend nikitia mguu bongo nitaendesha kamashine kangu binafsi ka kwanza maishani mwangu. sasa naomba mnisaudie kuhusu ununuzi wa gari kwa dar manake mambo hayo ya magari mie siyajui kabisa.

wengine wanasema ukienda zanziba utapata kwa bei nafuu zaidi, wengine wanasema ukiagiza kwenye mtandao linachelewa (obvious) na linanyofolewa vifaa bandarini hivo hasara tupu, wengine wanasema nikinunua kwenye show room za bongo, naweza kuchomekewa la wizi au lililofanyiwa usanii wa kubadilishwa taarifa muhimu ili lionekane jipya kumbe choka mbaya, wengine wanasema show room za dar bei mbaya sana. n.k.

sasa ukweli ni upi, mnanishauri nini, niagize, niende zenji ama nilambe hapo hapo show room za bongo?

ushauri tafadhari
kwanini usinunue huko uliko(majuu,sijui nchi gani)?gari jipya au used unanunua?kama ukinunua huko unaweza kupata exemption ukija nalo bongo,nafkiri huko majuu ni waaminifu zaidi tena na wewe uko huko utaliona na kukagua mwenyewe,sio kila gari inanyofolewa vitu bandarini, mimi naamini huko majuu bei ni nafuu,tafuta mtu anayejua magari huko akusaidie.
 
Hongera sana na nikukaribishe kwenye jumuia ya watu tuliyoisha shika fedha na kununua magari mengi tu. Naomba nikupe ushauri kama ifuatavyo:
1. zanzibar ni sehemu ya Tanzania, hawana kiwanda cha magari. Wote tunaagiza toka nje. matatizo ya Bandarini yanaweza kukupata hata kama ukinunua gari zanzibar maana ni lazima lipitie bandarini kwa meli (Hakuna barabara ya kuunganisha visiwa vya Zanzibar na Tanzania).
2. Mimi pia niko nje ya nchi lakini napendelea magari toka Japan na uingereza. Inategemea wewe huko nchi gani na unapendelea magari yapi? Nakushauri ununue magari ya Japan kwa barabara za bongo yanafaa!
3. Uagizaji ni rahisi na hakuna udanganyifu mkubwa!
4. Kuna stock ziko Bongo tayari na ni za dealers toka japan. hakuna udanganyifu hapo... go and buy!
5. Specify unataka gari la aina gani kwa maana ya Sedan, suv, pick up etc... then tutakuchangia mawazo wa aina nzuri ya kununua.
6. Kuwa mwangalifu usikurupuke na fedha zako ukaishia kujuta!
 
Nunua bongo mkuu, gari za zanzibar nyingi zinatoka dubai, zimeshakuwa used tena na tena!

ukinunua gari sehemu yoyote litapitia tu bandarini unless usafirishie nchi kavu au ndege

hawa jamaa nina waamini sana (sio kidogo) wanasifika sana, wazazi wangu walinunua gri hapo, na mimi hapo na kila ninayemjua nitamwelekeza hapohapo! they are genuine

yokohama motors;

www.alibabacars.com
0222110502
0786761102


Mtu mwingine ni member wa JF; alianzisha hii thread na nilishawahi kuwasiliana naye, I do trust him too, sema hakuwa na gari ninayoitaka kwa muda huo, but will surely use him in near future

https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/40473-unataka-kuagiza-gari-pitia-hapa-kwanza-7.html
 
kama uko majuu nunua gari uko uko uje nalo kwani uku magari yote yanaagizwa majuu kama unataka usitumie bandari agiza south afrika
 
ushauri!

Ni bora uagize kama

1. Utaweza kusubiri mpaka lifike na uvulimivu wa kulitoa bandarini na kumlipa mtu wa clearing na malipo mengi ambatanishi

2. kama huwezi nenda pale car junction au jananese vehicles show room zao za hapa dar es salaam pale ubungo opposite ubungu plaza unapata gari ya uhakika ila kwa bei juu kidogo ukilinganisha na magari ya show room za mitaani, mimi nilinunua mwaka jana july gari iko safi sana na mpaka leo hii huwa ni servise na kuweka mafuta na kuendelea kulitumia, ukisha lipia wanalitoa kwenye bond wanaweka jima lako na hakuna garama za kutransfer pia after one day kila kitu tayari na unaweka bima yako tu gari inaingia barabarani
 
.

sasa ukweli ni upi, mnanishauri nini, niagize, niende zenji ama nilambe hapo hapo show room za bongo?

ushauri tafadhari

Kununua show room na kuagiza japan hizo ndiyo option za kufikiria. sasa tofauti yake ni kama laki tatu mpaka tano.

Faida ya kununua show room ni gari unaipata muda huo huo ilivyo - hakuna usumbufu wa clearance - mi nilihangaika sana pale TRA na jamaa yangu kila siku natoa hela eti document zisongee mbele duh.

Cha msingi nunua show room ila kumbuka hapo juu kwamba utapata bei zaidi kwa laki 3 hadi tano mi naona hiyo ni sawa tu ukiringanisha na usumbufu ukiagiza hadi litoke.

mwisho hongera mzee kununua gari yako ya kwanza, mi yangu nilinunua miaka 10 iliyopita - ila siku nimenunua niliota kama mara mbili hivi gari inaibiwa - nikawa nachungulia dirishani kuicheki kumbe ipo, nilitamani nilale nayo ndani kwangu.

Sema aina ya gari unataka kununua then nitakushauri bei gani ukiagiza - na bei gani ukinunua show room then utafanya comparison ya usumbufu na kusubiria -
 
kwa yoyote mwenye kujua bei ya hizi Toyota harrier bongo price rang yake.. Nawasilisha
 
Milioni kama kumi na tano hivi unapata harrier hapo bongo,njoo nikuunganishe kwa kanumba ana uza Yake yeye kanunua nyingine.
 
Jamani ninatamani kumiliki ka Toyota Raum, kwa yeyote anayejua bei zake, na wapi naweza kukapata kwa unafuu, tafadhali anisaidie taarifa hizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom