Naogopa Majibu Ya DNA.

Pole sana mdogo wangu?
Hivi hivyo vipimo vinasemaga ukweli??? Ukijiangalia unafanana kwa jinsi yoyote ile na baba yako?

Mimi nina experience ambayo siyo nzuri kwenye hayo masuala ya DNA. Ninachokuomba piga moyo konde, kwa kuwa wameshaamua ukapime nenda tu ukapime. Wewe omba kwa Mungu na mambo yote ya mbeleni Mungu atakuwezesha. Na kama inawezekana ukiongea na baba yako, muulize Baba tunaenda kupima, mimi ni mtoto sijui lolote na wala sikuwepo na ufahamu wakati mimba yangu inatungwa. Na pia hatuna uwezo wa kujichagulia wazazi Mungu ndiyo anatuchagulia tuzaliwe wapi. Sasa ikitokea majibu ni negative itakuwaje? Unajua inabidi wakuandae kisaikolojia ili uweze kupokea majibu. Na baba yako kama ana mapenzi ya kweli pamoja naye atakuwa katika wakati mgumu (lakini si kukushinda wewe) akukubali tu kuwa ni mtoto wake either majibu ni positive au negative.

Nina mtoto wa kaka yangu, Kaka yangu alimpa mimba msichana wakati huyo akiwa form IV, akamkataa mtoto moja ya sababu zake ni mama yake alikuwa mwingi wa habari. Mama yetu akaamua kumchukua na kumlea akisema amefanana na sisi. Kwa sasa huyo kaka yangu kaoa muda, binti huyo ana miaka 21, step mother kamlazimisha kaka yangu akapime DNA kwa madai mtoto siyo wake. Na huyo kaka yangu aliamua kuishi na binti yake huyo mara alipoanza kujitegemea. Huyo mtoto kilimuuma sana, na walikuwa wanampenda sana na baba yake na hakuwa na mapenzi na mama yake kabisa. Kipimo kikafanyika, ilichukua majibu miezi sita ndiyo yakatoka na yakawa negative. Hatujui majibu yalichakachuliwa na step mother au la, maana yalichukua muda mrefu wakati kawaida ni wiki 2. Hatujui kama vipimo hivyo ni vya kweli au la! Yule binti hadi leo kachanganyikiwa, kashindwa kuendelea na shule, yaani hayo majibu yake yameharibu maisha yake kabisaa! Pamoja alikuwa anatunzwa na baba yake na ikafikia kiasi bibi yake yaani mama yetu akamchukua akae naye, pamoja na all the councelling za baada ya kuchanganyikiwa bado hajarudi sawa.

Hivyo naelewa ni situation gani unayo, lakini isikuharibie maisha yako, na uzuri wewe umelelewa kwa upande wa mama. Kwamba uko karibu na familia ya mama. Mungu bado anakuwazia yaliyo mema, kama itakuwa negative si wewe peke yako uliyepata mitihani hiyo, wengine wazazi wao wote wawili hawawafahamu, walisikia tu kuwa walikufa. JIPE MOYO, SONGA MBELE
 
kipimo cha DNA ni uthibitisho kwa wana ndugu kwamba mimi ni damu yao.

Muda wangu umeniishia hapa, ila najifikiria iwapo ungekuwa wewe kwenye umri huo unaambiwa lazima ufanye DNA
testing kuthibitisha uhalali wako kwa baba yako, kisha majibu yawe kinyume na unavyoyatarajia.
Nitakuja wasoma kesho, Inshaallah.

Sasa inamaana mama yako ndo haaminiki kwamba huyo ndo baba yako au hao wanaopinga wana baba mwingine wanataka kukupa...maana kama mama kasema huyo ndo babayo sasa iweje tena watu from nowhere to waanze kutafuta DNA?? Ndo mana nikauliza chanzo cha kufika huko ni nini...ndugu wa baba , au mama mwenyewe au nini!!?? na kama huyo baba haaminiki kama ni yeye inamaana kuna mwingine anayehisiwa...!! au kuna nini hapo!??
 
Hapana, niwie radhi unisomapo vibaya. Uchungu umenitawala ndo maana waona kama sitaki kupokea ushauri. Sawabho. Ninaloliongelea hapa ni post traumatic stress baada ya majibu ya DNA. Tayari najiona mdhaifu kuyapokea majibu yatayokuwa tofauti na ninavyoyategemea.

Sasa wewe ushaamua kwamba utapata PTS tayari kwasababu? We ni mdhaifu sana moyoni?

Acha kujiandalia mabaya. . . just be happy huyo mzee amekukubali bila kushinikizwa huku ukiomba majibu yawe yenye faida kwako hata kama sio leo.
 
Pole sana dada. But lets hope for the best. Hayo hayakuwa makosa yako, na kama baba anaamini wewe ni mwanae, naamini anajua anachofanya.
 
Hapana, nimekuwa natamani na mimi niwe na baba yangu. Nimevumilia mengi kuwaona wenzao na baba zao. Baada ya mwaka
na kufaidi raha na mapenzi ya baba niambiwe kumbe si baba'ngu kwakweli tayari ishaanza kuniuma kabla hata hatujapima. Natamani nikatae kupima Jamani. Sijui nimekosea nini Mwenyezi Mungu mie.

Kuna raha gani sasa ya kumuomba awe baba'ngu? mimi namtaka baba'ngu mzazi.

Mimi sikubaliani na hii dhana ya kuwa baba ni yule mwanaume aliyefanya tendo akatungisha mimba...it takes more than that to be a father, kitu ambacho nakiona kwa baba yako huyu Jasmine. Alikubali responsibilities kama baba, akamsaidia mama kukulea (japo kwa kugharamia) pale mapungufu yalipotokea, amebaki kuwa na mawasiliano na mama yako katika kipindi chote hicho...na baada ya kukutanishwa na wewe amekupenda na anakujali kama binti yake...Huyo ndio baba! What he has done make him a FATHER! Kama majibu ya DNA yatakuwa tofauti, huyo mwingine ni alitungisha mimba tuu, na hilo halimfanyi kuwa baba...anabaki kuwa mtungisha mimba...baba ni yule aliyeenda steps further than that!

Good luck nakuombea huyo 'baba' yako ndio pia awe baba kwa kipimo hicho cha DNA.
 
pole Jazmine
punguza wasiwasi na msongo wa mawazo maadam mama yako ametamka huyo ndio baba yako basi amini hivyo.......vinginevyo usema mama yako amekudokeza kwamba huyo sio baba mzazi

Mimi sikubaliani na hii dhana ya kuwa baba ni yule mwanaume aliyefanya tendo akatungisha mimba...it takes more than that to be a father, kitu ambacho nakiona kwa baba yako huyu Jasmine. Alikubali responsibilities kama baba, akamsaidia mama kukulea (japo kwa kugharamia) pale mapungufu yalipotokea, amebaki kuwa na mawasiliano na mama yako katika kipindi chote hicho...na baada ya kukutanishwa na wewe amekupenda na anakujali kama binti yake...Huyo ndio baba! What he has done make him a FATHER! Kama majibu ya DNA yatakuwa tofauti, huyo mwingine ni alitungisha mimba tuu, na hilo halimfanyi kuwa baba...anabaki kuwa mtungisha mimba...baba ni yule aliyeenda steps further than that!

Good luck nakuombea huyo 'baba' yako ndio pia awe baba kwa kipimo hicho cha DNA.
Ni kweli kabisa umesema...na l kuongezea tu hapo mi namshauri ajaribu kufuailia kwa ukaribu huyo anaeng'ang'aniza kwenda kupima hiyo DNA ana ajenda gani hapo nyuma..sababu kama mama na wewe mtoto mmemkubali baba (kwa mujibu wa mama) sasa inakuaje tena mtu baki (kwa interests anazozijua yeye) aanzae kuleta mambo yake? kwa nini mkapime DNA..hawamwamini huyo baba?

Na kama hawamwamini sasa wanamwamini nani...(siku ya kutungwa mimba walikuwepo)?? na huyo wanaemuamini kuwa ndo baba(kama yupo) siku zoooote hizo alikuwa waapi? Au wanatafuta manen tu na chuki binafsi!!?

Kimsingi kama ningekuwa ni mimi hata huko kwenye DNA nisingekubali kwenda bila kuwepo kwa sababu muhimu ya kwenda huko maana kama hao wanaotaka wanachuki zao wanaweza hata kucheza dili ilimradi tu kuharibu majibu na mpango wao ufanikiwe...!!HELL NOO...!!
 
Samahani kama hukunielewa awali. Ni ndugu wa baba'ngu wenye shinikizo hilo japo mwenyewe alishajikubalisha mie ni mwanae.

Sasa inamaana mama yako ndo haaminiki kwamba huyo ndo baba yako au hao wanaopinga wana baba mwingine wanataka kukupa...maana kama mama kasema huyo ndo babayo sasa iweje tena watu from nowhere to waanze kutafuta DNA?? Ndo mana nikauliza chanzo cha kufika huko ni nini...ndugu wa baba , au mama mwenyewe au nini!!?? na kama huyo baba haaminiki kama ni yeye inamaana kuna mwingine anayehisiwa...!! au kuna nini hapo!??
 
Akhsante Muinjilisti kwa mustakabali huu, nimesisimkwa na mwili kusoma haya uloyaandika kiasi cha kutamania aheri
ningekuwa switched at birth lakini naishi na wazazi wawili wanaonipenda na kunijali kuliko dhahma hii
niliyonayo.

Pole sana mdogo wangu?
Hivi hivyo vipimo vinasemaga ukweli??? Ukijiangalia unafanana kwa jinsi yoyote ile na baba yako?

Mimi nina experience ambayo siyo nzuri kwenye hayo masuala ya DNA. Ninachokuomba piga moyo konde, kwa kuwa wameshaamua ukapime nenda tu ukapime. Wewe omba kwa Mungu na mambo yote ya mbeleni Mungu atakuwezesha. Na kama inawezekana ukiongea na baba yako, muulize Baba tunaenda kupima, mimi ni mtoto sijui lolote na wala sikuwepo na ufahamu wakati mimba yangu inatungwa. Na pia hatuna uwezo wa kujichagulia wazazi Mungu ndiyo anatuchagulia tuzaliwe wapi. Sasa ikitokea majibu ni negative itakuwaje? Unajua inabidi wakuandae kisaikolojia ili uweze kupokea majibu. Na baba yako kama ana mapenzi ya kweli pamoja naye atakuwa katika wakati mgumu (lakini si kukushinda wewe) akukubali tu kuwa ni mtoto wake either majibu ni positive au negative.

Nina mtoto wa kaka yangu, Kaka yangu alimpa mimba msichana wakati huyo akiwa form IV, akamkataa mtoto moja ya sababu zake ni mama yake alikuwa mwingi wa habari. Mama yetu akaamua kumchukua na kumlea akisema amefanana na sisi. Kwa sasa huyo kaka yangu kaoa muda, binti huyo ana miaka 21, step mother kamlazimisha kaka yangu akapime DNA kwa madai mtoto siyo wake. Na huyo kaka yangu aliamua kuishi na binti yake huyo mara alipoanza kujitegemea. Huyo mtoto kilimuuma sana, na walikuwa wanampenda sana na baba yake na hakuwa na mapenzi na mama yake kabisa. Kipimo kikafanyika, ilichukua majibu miezi sita ndiyo yakatoka na yakawa negative. Hatujui majibu yalichakachuliwa na step mother au la, maana yalichukua muda mrefu wakati kawaida ni wiki 2. Hatujui kama vipimo hivyo ni vya kweli au la! Yule binti hadi leo kachanganyikiwa, kashindwa kuendelea na shule, yaani hayo majibu yake yameharibu maisha yake kabisaa! Pamoja alikuwa anatunzwa na baba yake na ikafikia kiasi bibi yake yaani mama yetu akamchukua akae naye, pamoja na all the councelling za baada ya kuchanganyikiwa bado hajarudi sawa.

Hivyo naelewa ni situation gani unayo, lakini isikuharibie maisha yako, na uzuri wewe umelelewa kwa upande wa mama. Kwamba uko karibu na familia ya mama. Mungu bado anakuwazia yaliyo mema, kama itakuwa negative si wewe peke yako uliyepata mitihani hiyo, wengine wazazi wao wote wawili hawawafahamu, walisikia tu kuwa walikufa. JIPE MOYO, SONGA MBELE
 
Pole sana, USHAURI MWINGI HAPA NI MZURI SANA KWAKO, OMBA MUNGU NA USIWAZE NEGATIVE KATIKA MAISHA HAKUNA KITU KIZURI KAMA KUWAZA POSITIVE, LAKINI ANAYEJUA BABA WA MTOTO NI MAMA, KWANI WEWE UMUHAMINI MAMA YAKO? MWAMINI MAMA YAKO NA AMINI ANACHOSEMA, USIOGOPE NA ONDOA MAWAZO, KUWA NA AMANI MOYONI UTASHINDA TU.
 
Inaonekana phenotypically uko kwa wajomba zaidi hivyo ndugu wa upande wa baba wanapata msukumo wa kutaka kujua genotypically umejengeka namna gani . Hata hivyo isikutishe maana unaweza kuta hata hao wanaong'ang'ania hawajawahi kwenda kupima na kujiridhisha , jipe moyo Mwenyezi MUNGU atakuwa upande wako.
 
mzazi wa kike ndio anejua nani baba halisi wa mtoto.
mamako keshakuambia huyo ndio babako
vipimo vya DNA wapi? bongo ama sehemu nyingine? wanashindwa kusoma majibu ya CT scan au MRI ndio wataweza DNA
NINA Mifano hai watu wengi wanapewa majibu sio.
AFU KWANI HAUFANANI NA babako hata ukucha? kama ndio kuna haja gani ya DNA bibie?????
 
Umri wangu ni miaka ishirini na mmoja. Wazazi wangu hawakuwahi kuoana wala kuishi pamoja kwani nilipokuwa conceived (wazazi) wangu walikuwa bado kwenye late teens, wakati huo wanafunzi. Katika mazingira hayo, umri wangu wote nimelelewa na familia ya mama yangu kisiwani zanzibar katika maadili ya kiislamu.

Kwa ung'ang'anizi wangu, Mwaka jana nimefanikiwa kumshawishi mama yangu mpaka akanikutanisha na baba yangu.
Yeye Mkristo na maisha yake yote ni Tanzania Bara, sababu familia ya mama'ngu hawakutaka aibu ya familia wala mahusiano na mawasiliano yeyote na baba'ngu. Nililelewa nao na kusomeshwa mpaka umri huu, ingawa mama'ngu amekiri mbele ya baba'ngu kwamba kwa takriban miaka kumi na moja wamekuwa wanawasiliana (kwa siri) na baba'ngu iwapo palikuwapo na mapungufu ya pesa na ambazo mama alishindwa jazilia.

Hivi sasa na mawasiliano ya mara na baba'ngu na kiukweli ananipenda sana, nami nampenda sana. Tatizo ni kwamba
limepitishwa azimio la kwenda kupima DNA kutokana na shinikizo la ndugu wa baba, japo mwenyewe baba ananambia kiukweli naye hajiskii kufanya hilo.

Woga wangu ni kwamba majibu yakiwa ni kinyume na ninavyoyatarajia, nami sitaki kumpoteza huyu baba ambaye kwa miaka mingi nimekuwa natamani nifahamiane nae, leo hii mwenyezi mungu katukutanisha halafu majibu yawe negative, kwamba sio baba yangu? Nisaidieni wanajamii forums, nijiandae vipi kulipokea hili. Natauficha wapi uso wangu majibu yakiwa kinyume na ninavyoyatarajia, kwa maana tayari tushazoeana sana na baba'ngu.
Honestly sioni kwanini mpime DNA, kwani huu ni uamuzi ambao huja kama kuna baba zaidi ya mmoja ambao wote wanadai mtoto ni wakwao. lakini issue yako nitofauti kabisa na inafanya suala la DNA likose nguvu.

Sasa wewe kataa hii issue ya DNA, wambie hautaki kabisa unless kama kuna mtu mwingine anae dai kuwa wewe ni mwanae, kama hayupo basi , kila la kheri msalimie dady
 
Umri wangu ni miaka ishirini na mmoja. Wazazi wangu hawakuwahi kuoana wala kuishi pamoja kwani nilipokuwa conceived (wazazi) wangu walikuwa bado kwenye late teens, wakati huo wanafunzi. Katika mazingira hayo, umri wangu wote nimelelewa na familia ya mama yangu kisiwani zanzibar katika maadili ya kiislamu.

Kwa ung'ang'anizi wangu, Mwaka jana nimefanikiwa kumshawishi mama yangu mpaka akanikutanisha na baba yangu.
Yeye Mkristo na maisha yake yote ni Tanzania Bara, sababu familia ya mama'ngu hawakutaka aibu ya familia wala mahusiano na mawasiliano yeyote na baba'ngu. Nililelewa nao na kusomeshwa mpaka umri huu, ingawa mama'ngu amekiri mbele ya baba'ngu kwamba kwa takriban miaka kumi na moja wamekuwa wanawasiliana (kwa siri) na baba'ngu iwapo palikuwapo na mapungufu ya pesa na ambazo mama alishindwa jazilia.

Hivi sasa na mawasiliano ya mara na baba'ngu na kiukweli ananipenda sana, nami nampenda sana. Tatizo ni kwamba
limepitishwa azimio la kwenda kupima DNA kutokana na shinikizo la ndugu wa baba, japo mwenyewe baba ananambia kiukweli naye hajiskii kufanya hilo.

Woga wangu ni kwamba majibu yakiwa ni kinyume na ninavyoyatarajia, nami sitaki kumpoteza huyu baba ambaye kwa miaka mingi nimekuwa natamani nifahamiane nae, leo hii mwenyezi mungu katukutanisha halafu majibu yawe negative, kwamba sio baba yangu? Nisaidieni wanajamii forums, nijiandae vipi kulipokea hili. Natauficha wapi uso wangu majibu yakiwa kinyume na ninavyoyatarajia, kwa maana tayari tushazoeana sana na baba'ngu.

Pole sana Jazmine, hili liko nje ya uwezo wako ushauri wangu ni kuomba Mungu sana ili majibu ya DNA yaje kama utakavyo na ninahisi utalia sana baada ya kufahamu majibu hayo. Ikiwa ni yale uyatakayo utalia machozi ya furaha kwa sala zako kutimia na kupata kile utakacho na yakiwa mabaya basi utalia kwa uchungu kwa vile dhana yako kwamba umemfahamu Baba yako haikuwa ya kweli. Kama ikitokea bahati mbaya huyu ulimfahamu sio baba yako, basi usiendelee tena na hili zoezi maana linaweza kukuumiza zaidi na kukosa furaha kabisa katika maisha yako hapa duniani. Kila la heri.

Usijali sana mamake..

Kwanza kabisa ombe tu majibu yatoke positive yaonyeshe ndo mzazi wako)
Na kama mama ako amekuhakikishia huyo ni babako. Basi usiogope sana dear.

Sema kwa upande mwingine majibu yakatoka huyo si babako. USIJALI KABISA
kwani si mwisho wa dunia. Angalia na shukuru una mama unaekupenda kwa kweli.
Na papo hapo itabidi umuulize tena mama . Babako ni nani?

Kwa sasa usubiri tu hayo matokeo , yaweza kuwa waogopa kitu ambacho hakipo.
Na majibu yakitoka visivyo ndipo uchukue muda na kufikiri cha kufanya next. yaweza
kuwa majibu ni ndio.. Kila lakheri. Kumbuka kila kinachotokea kuna sababu .. siku njema
 
kabla ya kwenda kupima mbane mama yako kwanza-coz yye ndie anayefaham ukweli
 
Back
Top Bottom