ondoa hiyo milele, mimi naogopa pricker tu!nitapata wapi huo ujasiri mimi?na wametangaza hakuna dawa milele
Nichukue mimi basi smile
....Itabidi uutafute huo ujasiri haraka iwezekanavyo ili ukapime afya yako. Utakosa raha na kuwa na wasiwasi sana lakini huna jinsi inabidi tu ujitutumue na kwenda kujiangalia kama uko salama au umeshadhurika. Siku ile ya AIDS duniani kama sikosei December 1, 2011 nilikuwa naangalia kipindi kimoja walikuwa wanazungumzia kuhusu umuhimu wa kupima na wakasema sasa hivi ni 20 minutes tu tayari umeshajua hali yako. Kila la heri.
nitapata wapi huo ujasiri mimi?na wametangaza hakuna dawa milele
Feis Buku hujambo? Unaye nitafuta ni mimi?napita tu,kuna mtu namtafuta simuoni!!
Hilo ni kosa kubwa kwa nafsi yako. Lakini hujachelewa bado. Jipe moyo wa ujasiri kapime na uchukue majibu yako. Watu wengi wasichokijua ni kuwa yeyote anayefanya hivyo huwa kama amezaliwa upya, kwani majibu yoyote atakayopata yatamweka huru zaidi na kumpa uwezo wa kujua mustakabali wa maisha yake na namna bora ya kuishi kuanzia hapo. Kwa mfano usipokutwa na virusi utapata ahueni ambayo hujawahi kuipata kabla itakayokufanya uwe makini zaidi kwa vitendo vyako ili usijeambukizwa virusi. Na ukipatikana na Virusi itabidi ukubaliane na ukweli kwa kuanza kupima kipimo cha pili ili kujua kiasi cha uambukizo (viral load) ili ujue km unahitaji kuanza kutumia dawa za kurefusha maisha ARVs, na kuchukua tahadhari ili usiweze kuambukizwa aina nyingine ya virusi vya HIV. Kwa kufanya hivyo utakuwa unaishi kwa matumaini.Mbona kupima ki2 rahisi sana!! mi nishapima kama mara 3 hivi!! majibu ndio huwa sichukui.
nitapata wapi huo ujasiri mimi?na wametangaza hakuna dawa milele
Malaria haikubaliki!!Ukimwi----?jamani dawa ni kubadili tabia kwa wote wawili sio mmoja ni kazi bure kuishia kupima tu then mwendo mdundo,ni sawasawa na ujitibu malaria halafu unalala bila neti utauguwa tena na tenaaaa, ni hayo tu
acha uoga nenda angazasasa kama unajitolea kwenda kupima halafu unapewa majibu tofauti jamani inakuwaje hapo????