Nanyimwa haki ya kuoa ninayempenda

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,988
1,175
Wana JF,
Mimi ni mtanzani Halisi na nimempenda msichana toka Moshi kibosho ILA naambiwa na wazazi wangu kuwa wasichana watokao huko ni hatari.Naambiwa si sahihi kuoa msichana toka kibosho INGAWA sababu sipewi.Nisaidieni.
 
unampenda kweli? kama jibu ndio basi yeyote alietia mikono yake shambani kisha akatazama nyuma hafai katika ufalme ukigeuka nyuma utakuwa jiwe la chumvi
 
Pole, nakushauri kaa na watu wazima ambao wazazi wako wanawaheshimu washirikishe kwa hili kisha mkae pamoja na wazazi wakujulishe wanayoyajua kuhusu waliyokwambia, kuna vitu nyuma ya hayo maneno. Ila kwa tahmini yangu , hao wazazi wako ni 'wabaguzi' na wakitoka kuchagua makabila, watakuja dini, kisha uchumi, kisha elimu...mwisho wa siku utajikuta unaishi kwa kuwafurahisha wao... mwamuzi na mshauri wa ndoa ni MUNGU peke yake, ndo maana imeandikwa kuwa mtu ataachana na wazazi wake na kuungana na mke/ mume wake. Kila kabila lina mapungufu yake na faida zake, wewe unamuoa mtu na si kabila... "sifahamu njia kamili ya kufanikiwa kimaisha hasa, ILA nafahamu njia ya kutaka kufeli kimaisha ni kutaka kumfurahisha kila mtu"
 
Kwa hali hii hata wakikuambia unastahili kuolewa na si kuoa utaishia kukubali huku ukilalamika...mijitu mingine bwana....mke ni wako wewe,eti wazazi wameniambia,acha utoto......
 
pamoja na kuwa na haki ya kufanya kile unachotaka, ni busara kuchukua muda wako kufanya uchunguzi ili ujue sababu za wazazi kutokuwa comfortable na hilo kabila.....remember, to be fore-warned is to be fore-armed
 
To my experience, some extend is true.
These Kibosho girls are to determinant to some extend she ia able to terminate your life because of money and investment you with her invested.
 
Wana JF,
Mimi ni mtanzani Halisi na nimempenda msichana toka Moshi kibosho ILA naambiwa na wazazi wangu kuwa wasichana watokao huko ni hatari.Naambiwa si sahihi kuoa msichana toka kibosho INGAWA sababu sipewi.Nisaidieni.
wee si umefall bana muoe tu wangetoa reasons lyk level of education ,imani ya dini ndo zinge mata sababu nyepesi kama hizo walizokwambia tupilia mbali , ujue ni ishu kupata wyf nowadayz ohooo love is too fragile chukua hatua listen only God knows what will happen next btn the two of you bana
 
Wana JF,
Mimi ni mtanzani Halisi na nimempenda msichana toka Moshi kibosho ILA naambiwa na wazazi wangu kuwa wasichana watokao huko ni hatari.Naambiwa si sahihi kuoa msichana toka kibosho INGAWA sababu sipewi.Nisaidieni.

house girl wetu anatokea bagamoyo kwenye kabila linaloongea kikwere******,,,,,badili maamuzi umbebe,ili shem wako awe kei kei
 
Duuuuuuuuh were in da same pot! Ata mimi hili swala nilisha tahadharishwa na wazazi lakini sikupewa sababu pia ila walisema hawataki kusikia! Nikabadili studio
 
A real man always stands on his own desicions!!

Ni kweli hun wangu, lakini maamuzi mwengine yanawaathiri watu wengi na huyo real man hatoweza kuufanya huo uamuzi peke yake lazima amtafute mwenye hekima amshauri na washauri anaowaamini sana ndo wameshasema hivyo...
 
Wana JF,
Mimi ni mtanzani Halisi na nimempenda msichana toka Moshi kibosho ILA naambiwa na wazazi wangu kuwa wasichana watokao huko ni hatari.Naambiwa si sahihi kuoa msichana toka kibosho INGAWA sababu sipewi.Nisaidieni.

1)Its only fair uhakikishe unajua sababu ili ukifanya maamuzi uwe unajua madhara yake vizuri
2)Ki ukweli mara nyingi ukienda aganist watu kama hao utabeba mzigo mkubwa mabegani mwako hivyo unatakiwa kujiandaa hasa...
3) Always seek the truth and It shall set you free
 
mi ni mtu kutoka pande za kanda ya kaskazini ila msiniulize kabila gani ukweli mkuu wasichana wa kibosho wengi wao kama hujawazoea huwa wanapenda sana kuwatawala waume zao huo ni ukweli najua kuna wtu watanizodoa ila kwenye ukweli tuuweke nina huo uzoefu mwanamke wa kibosho hata wa kimachame hataki mchezo mchezo hasa ule mfumo dume nyumbani kwenu na vile vile shilingi unayoichuma lazima umuambie ni ngapi na matumizi lazima mpange wote hata kama yeye hafanyi kazi ukweli kama hujazoea hayo utaona ndoa ni chungu sana ila na vile vile usijaribu kumeletea mtoto wako uliyezaa na mwanamke mwingine aje aishi hapo kwenu hata kama ni mkubwa kivip utajuta. mkuu kama unajiamini utakuwa mwaminifu na muwazi kwa kila jambo uatakalolifanya katika ndoa yako poa muoe tu ingawa navyowajua wabongo wengi wao ni vigumu kumudu. nimesema wengi wao ila kuna baadhi hawana hiyo tabia na vile vile msaada kwao kwa mwanamke ni wa kwanza kupeleka kabla ya kupeleka kwenu kwa wazazi wako hiyo ni principle, ndugu yangu kaoa mkibosho ukweli naujua siwezi kusema anajuta ila kwa sisi tulionje tunaona anavyohangaika hata simu akipigiwa tu mida ya jioni utaona anabadilika uso kwa hofu kuwa sijui ataambiwa nini. kwa hiyo hao wazazi wako wanauzoefu huo na ndio sababu wamekupa tahadhari ila ukijifanya eti msomi na yamepitwa na wakati mambo hayo fuata moyo wako ila mwisho wa siku usije ukasema au ukaja hapa jamvini ukasema najuta. wazazi sio wajinga na usiseme wamepitwa na wakati maana wakati mwingine wazazi siku zote huwa hawapendi watoto wao waje wateseke kwa uzoefu walio nao. fikira tafakari chukua hatua zinazostahili kupitia mawazo ya watu na ya kwako uamue lipi jema kwako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom