Nanyaro: James Ole Milya sahau kabisa uongozi ndani ya Chadema

kama maneno haya kayasema NANYARO kutoka kwenye kinywa chake na hakulishwa na muandishi wa habari wa Mwananchi kwa mikakati ya gazeti hilo kwa upande wa Arusha, atakuwa amegafilika kimtazamo, kwani Milya hakuja chadema kwasababu ya vyeo kwani huko atokapo aliviacha vyeo bali utashi wake na uzalendo wake ndiyo umemleta kuungana na makamnda kudai haki ya mtanzania, Hayo mengine ni hofu ya viongozi kuwa na wasi wasi wa nafasi zao na kutokujiamini. HAMNA JAMBO LISILOWEZEKANA KATIKA KIZAZI HIKI, WENYE HOFU MTAONDOKA KWELI.

Kiongozi Kilewo, hii habari ina aina fulani ya spinning na imeenda nje ya context. Na hii ni kwa sababu imechomolewa 'paragraph' katikati na hivyo kutoa maana potofu.

Binafsi nimesoma hii article na ni majadiliano kati ya Nanyaro na mwandishi wa Mwananchi. Nanyaro aliulizwa (na mwandishi) kuhusu Millya kupata uongozi CHADEMA, na majibu ya Nanyaro ni kwamba CHADEMA hawatoi uongozi kama pipi bali "huteuwa watu baada ya kujiridhisha sana ili kuepuka kuwa na watu wasio na nia na malengo sawasawa na chama hicho". Pia Nanyoro anesema CHADEMA "kimejifunza mambo mengi kutoka na makosa na historia hivyo wameweka utaratibu maalum wa kupata viongozi waadilifu.

Article ni ndefu na ukisoma kwa makini utaona kuwa Nanyaro hamuongelei Ole Millya kama Ole Millya bali anajaribu kueleza utaratibu wa kupata viongozi ndani ya Chama (CHADEMA) na viongozi wengine wanataowakilisha chama kwenye upande wa serikali i.e udiwani etc.

Kama kawaida mwandishi wa habari aliamua kuchomoa 'juicy headline' lakini ukisoma haiko hivyo.
 
huyu ni mfitini anataka kubadili upepo/ukweli. cdm walisema wote wanakaribishwa, watakapofika watapimwa kwa vigezo na itikadi za cdm na wakifaulu muda ukifika wanaweza wakagombea katika vyeo vitakavyokuwa wazi na wakishinda watapewa

au mm sikuwaelewa cdm??
 
FJM,
Mbona unapotosha makusudi kwa mapenzi yako! Kwa hiyo unataka kusema haya maneno "Nanyaro: James Ole Milya sahau kabisa ungozi ndani ya Chadema" hayakusemwa na Nanyaro? Ebu tuambie kwenye hii thread kuna maneno gani yameongezwa au yamepunguzwa?
 
huyu ni mfitini anataka kubadili upepo/ukweli. cdm walisema wote wanakaribishwa, watakapofika watapimwa kwa vigezo na itikadi za cdm na wakifaulu muda ukifika wanaweza wakagombea katika vyeo vitakavyokuwa wazi na wakishinda watapewa

au mm sikuwaelewa cdm??

Mkuu haya maneno sijayasema mie ni gazeti letu pendwa la Mwananchi.
 
Ritz, we bado unalia na CHADEMA tu.
Huna habari nyingine za kupost?

Ritz anatakiwa ajue sisi Chadema tuna mambo mengi sana tuyafanyayo na tuyajuayo ila ni siri yetu kama chama.. Nanyaro kasema kwa maana fulani ambayo anaijua yeye, ila asubiri atajua baadaye hiyo kauli ililenga nini! Millya tunamkubali sana kama ameamua kuja kwa nia moja maana tunajua Millya mwenyewe ni mpambanaji sana na atatufaa sana..asubiri aone..na Ritz aache kugombanisha watu kike! hizo ni mbinu za kike mkuu na watu wenye busara wanakushangaa sana
 
Kwa falsafa ya nguvu ya umma inayoiongoza cdm kwa sasa, hakuna ambaye si kiongozi. Wote tupo mstari wa mbele kukomboa taifa. Kama kunaanayejipeleka cdm ili akapate cheo basi atakaa sana!

Nimeipenda hii!
Pamoja Kamanda Filipo!
 
Back
Top Bottom