Nani zaidi: Rose Muhando vs Bahati Bukuku?

Teamo

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
12,272
1,035
jamani eeh!
Tunasoma sana siasa,tunaudhiwa sana na mambo yanayofanywa na viongozi wetu,tunachangia kwa jazba kuu.sehemu kubwa ya michango yetu inasaidia kufungua akili za watu.na kuna wakati michango yetu huwa KELELE ZA CHURA,turelax kidogo wapendwa!

Muziki wa injili unakomaa siku hadi siku,na vipaji vipya vinaibuka kila inapoitwa siku.

Naomba tuwajadili wakongwe hawa wawili ambao wamefungua milango kwa waimbaji wengi wa muziki wa injili

PAMOJA NA LADHA YA MIZIKI YAO KUTOFAUTIANA,lakini kuna mtu kati ya hawa IS THE BEST?
..................TUJADILI
 
jamani eeh!
Tunasoma sana siasa,tunaudhiwa sana na mambo yanayofanywa na viongozi wetu,tunachangia kwa jazba kuu.sehemu kubwa ya michango yetu inasaidia kufungua akili za watu.na kuna wakati michango yetu huwa KELELE ZA CHURA,turelax kidogo wapendwa!

Muziki wa injili unakomaa siku hadi siku,na vipaji vipya vinaibuka kila inapoitwa siku.

Naomba tuwajadili wakongwe hawa wawili ambao wamefungua milango kwa waimbaji wengi wa muziki wa injili

PAMOJA NA LADHA YA MIZIKI YAO KUTOFAUTIANA,lakini kuna mtu kati ya hawa IS THE BEST?
..................TUJADILI



mie kwa kweli nampenda sana bahati bukuku, akiimba mie naccmukwa, video zake anacheza kwa utaratibu tu na zinanivutia sana, video za rose kwa kweli wachezaji wake wanacheza kwa fujo mno, hii latest yake ya sasa jamani hapana, kuna kale katoto kanacheza kwa nguvu zote, kichwa kile haaa nadhani wakimaliza shoo wanakunywa panadol.
 
Mkubwa hao wote mie naona wanafanana sana kwani licha ya kutofaotiana aina ya mapigo ya muziki wao bukuku ni kama alikuwa anataka kuwajibu watu katika albamu yake ya mwisho na muhando amebaki kuwa mburudishaji zaidi kuliko kuwa muhubiri. ukitaka tujadili nani zaidi mkubwa labda ungekuwa specific ni katika lipi? mauzo? Mavazi? Kufanikiwa kiuchumi au kiroho?
 
bukuku ni kama alikuwa anataka kuwajibu watu katika albamu yake ya mwisho na muhando amebaki kuwa mburudishaji zaidi kuliko kuwa muhubiri.

HOOPS UMESOMEKA!SASA NISAIDIE,bukuku alikuwa anawajibu wa akina nani?
 
Raha ya ngoma ni mdundo namzimia sana Rose Mhando anamashabiki wengi kuliko mwimbaji yeyote wa nyimbo za injiri.
 
Mhh jamani Bahati Bukuku namkubali sana,rose Muhando naona amekaa kimapepe mapepe sana + hao wachezaji wake nao ni hivyo hivyo tu,sijaona jipya kwake naona makelele tu,Nyimbo za Bukuku zina message nzuri sana,Just inshort namkubali Bahati Bukuku
 
rose Muhando naona amekaa kimapepe mapepe sana + hao wachezaji wake nao ni hivyo hivyo tu,sijaona jipya kwake naona makelele tu

KWA HILI HAPA,naunga mkono hoja!

Nyimbo za Bukuku zina message nzuri sana,Just inshort namkubali Bahati Bukuku

HILI PIA NALIKUBALI ZAIDI,the lady is so creative.she seems to be A GREAT THINKER!

ebu jamani sikilizeni ule wimbo wa ESTER.utagundua huyu dada 'ni special'
 
- Hapana Rose hana mpinzani ndani ya bongo, binafsi nina experience kubwa sana na muziki kwa sababu nimeushiriki sana katika course of my life, kuanzia kupiga mpaka kutayarisha maonyesho.

- Muziki ni entertainment kwanza regardless of the message, and then ni biashara, Rose anayaweza haya yote mawili kwa sababu anaweza kujaza ukumbi au uwanja wowote, bila supporting guest star na akawaridhisha walipa kiingilio wote bila kujali rangi wala dini zao. It takes very special and talented musicians kuliweza hilo, hata huko majuu ni waimbaji wachache sana wanaliweza hilo.

- Mwanamuziki anayesifiwa sana majuu, ni yule anayeweza kuwajaza wazungu na minorities katika uwanja mmoja, bila msaada wa wanamuziki wengine, Rose does that na she did that hata in US recently.

FMES!
 
ebu jamani sikilizeni ule wimbo wa ESTER.utagundua huyu dada 'ni special'


Umenikumbusha nyimbo nyingine za Bahati Bukuku,SONGA MBELE na MAJARIBU yaani nazikubali sana hizi nyimbo,huyu dada ana kipaji na pia ana kipawa amepewa na Mungu
KIPAJI - mtu anazaliwa nacho
KIPAWA- MTU HUPEWA NA MUNGU,sasa unapochanganya hivyo vyote + maombi lazima utatoa nyimbo ambazo zinakua na message nzuri sana.
 
NIMEKUWA,natizama gospel music for some time now,even before the current crop of gospel artists kuibuka tanzania.akina rose na bukuku ni waimbaji wazuri lakini mbona nikitazama gospel artists toka kenya,how come naona wanawaacha tanzanian artists in the shade.lugha inayotumika ni kiswahili lakini kenyans seems to be more composed and more proffessional.how come
 
Mhh jamani Bahati Bukuku namkubali sana,rose Muhando naona amekaa kimapepe mapepe sana + hao wachezaji wake nao ni hivyo hivyo tu,sijaona jipya kwake naona makelele tu,Nyimbo za Bukuku zina message nzuri sana,Just inshort namkubali Bahati Bukuku
Mie nampenda zaidi Rose, tena huo umapepe wake ndo unanichota kabisa. Labda na mie mwenyewe ni kati ya mapepes, sijui, ila naburudika sana. Najisikia kumtukuza Mungu kwa 'nguvu zangu zote'.
Kwa nyimbo zenye msg, nampenda Bahati.
 
- binafsi nina experience kubwa sana na muziki kwa sababu nimeushiriki sana katika course of my life, kuanzia kupiga mpaka kutayarisha maonyesho[/B][/U]

TUNASHUKURU KWA TANGAZO.

-
-Muziki ni entertainment kwanza regardless of the message, and then ni biashara[/B][/U]

HILI NALIKATAA KATA KATA!kwenye maswala ya imani,na umungu hatuna entertainment wala biashara.nausikitikia sana mtizamo wako wa kibiashara kwenye mambo ya mungu.

-
-Mwanamuziki anayesifiwa sana majuu, ni yule anayeweza kuwajaza wazungu na minorities [/B][/U]

kwenye mambo ya mbinguni hakuna kusifiwa na wazungu,wala kuwajaza minorities.

hapa tunamsifu mungu,na pengine kuutafuta ufalme wa mbingu.


WANA JAMII,TUBUNI.
MRUDIENI MUUMBA WENU.SIKU ZA MWISHO ZIMEKARIBIA,nayale yaliyotabiriwa yameanza kuonekana
 
Waimbaji wote hawa wawili - ROSE MUHANDO na BAHATI BUKUKU ni watumishi wa Mungu wanaohubiri kwa nyimbo za Injili - WOTE wanabariki kila mtu kwa namna yake - na nyimbo zao WOTE zina message. Katika kusifu kwa ROSE MHANDO KWA NGUVU ZOTE - ndivyo Mungu alivyomjalia na ametoa sadaka nguvu zake zote mbele za Mungu - na BAHATI BUKUKU katika kuimba kwake kwa deep expensive voice - ndivyo Mungu alivyomjalia na message inawafikia walengwa - TUSICHANGANYE MUSIC YA HIP HOPS etc na GOSPEL SONGS - unapofungua moyo wako wakati wa kusikiliza - LAZIMA UTAGUSWA - IWE ANAIMBA ROSE - AU BAHATI - TUKUMBUKE - MUNGU NI ROHO NA WAMWABUDUO YAWAPASA KUMWABUDU KATIKA ROHO NA KWELI
 
Kwanza wote wawili wanamtukuza na kuhubiri neno la Mungu kwa nyimbo za dini.
Bahati Bukuku-Ana sauti nzuri ya kipaji na anaimba kwa hisia kali yaani ujumbe wake mzuri na unawafikia walengwa sikiliza wimbo wake kama Songa Mbele.

Rose Mhando-Nayeye ni kama anavyoimba Bahati Bukuku,sikiliza nyimbo kama Nipe Uvumilimu halafu Yesu Nakupenda kwenye albamu moja. ILA burudani imeongezeka zaidi kwenye uchezaji wa hizo nyimbo zake,kwa style yake ni kuchangamsha zaidi na ujumbe unawafikia walengwa.

NB: Ndugu dgeouff unaweza kuwa na wimbo unaitwa Upendo wa Yesu(huku na huku kama mawimbi upendo wa Yesu wanizunguka) kaimba dada fulani anaitwa Pendo/Upendo kama sikosei,ningependa pata audio kama unapatikana hapo kwenye JF injili haupo! Asante.
 
Bukuku alinikera sana kwenye video yake moja aliwaonyesha marehemu wa ajali ya treini kule dodoma. Hivyo mimi siangalii nyimbo zake tena. Mhando yupo juu, analazimisha hata wale wasiotaka kusikiliza nyimbo za injili kufanya hivyo bila kujua.
 
Rose ni mwimbaji anayejituma sana haswa awapo kwenye stage. Na nyimbo zake zinaladha tofautitofauti. Tatizo la Bukuku ni kwamba nyimbo zake zina tune na beat moja. Namzimia sana Rose.
 
- Hapana Rose hana mpinzani ndani ya bongo, binafsi nina experience kubwa sana na muziki kwa sababu nimeushiriki sana katika course of my life, kuanzia kupiga mpaka kutayarisha maonyesho.



FMES!

Uzuri wa huyu jamaa ANAJUA kila kitu......watu wengine NUKSI?..

Sasa hivi atasema alikuwa anaishi Jirani na Timbarland, subirini.
 
Jamani kiukweli hawa wote wawili ni wazuri kwa namna tofauti tofauti, lakini mie nina kitu tofauti kidogo juu ya waimbaji wa gospel wa kiume, hivi wameambiwa kwa Mungu lazima uvae kizaire???
Naona waimbaji wote wa injili wanaume wanavaa masuti makubwa kila siku... you can easily tell kabla ya show wasanii wafuatao watavaa nguo za aina gani.. Ambele Chapa Nyota, Bon Mwaitege, Mwansasu, n.k kitu unachoweza kukosea ni rangi labda. Lakini pia hawachezi mbali na triangle...yaani njano, nyeupe au nyekundi. Ukitaka kuamini angalia hata video zao!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom