Nani zaidi kati ya Joshua Nassari na Siyoi Sumari?

OLEWAO

Member
Jan 27, 2012
89
78
Wana JF,

Nimefuatilia kampeni za ubunge huko jimboni Arumeru mashariki kupitia vyombo vya habari.Kuna madai kuwa uelewa na uwezo wa mgombea wa CCM Bw. Siyoi Sumari juu ya mambo mbalimbali ya kijamii na kisiasa ya jimboni kwake ni mdogo ukilinganisha na ule wa mgombea wa CHADEMA Bw. Joshua Nassari. Ndiyo maana wakati fulani wapiga debe wa CCM waliwahi kumuombea mgombea wao kura za huruma kwa kusema apewe kura za kushinda ili afutwe machozi.

SWALI.

Je, uandaliwe mdahalo utakaorushwa moja kwa moja na TBC baina ya wagombea hawa wawili tarehe 31-03-2012(siku moja kabla ya kupiga kura) ili wana-Arumeru na sisi pia tujiridhishe na madai haya?

Naomba kuwasilisha.
 
Naona unatoa ratiba ya mdahalo utadhani wewe ndiyo mkurugenzi wa TBC. una tamani lakini hakuna kitu.
 
Ndugu yangu Josip,

Usipandwe na jazba,kama madai haya yanasemwa na watu,ni busara kuwakutanisha vijana hawa ili wanaodai Siyoi povu la sabuni kwa Nassari ama wajisifu kuwa ni watafiti wazuri ama tujue wana chuki binafsi na kijana Siyoi. Na siku nzuri ni siku ya mwisho ya kuhitimisha kampeni yaani kufanya majumuisho.

Lete mawazo ya kujenga usiingiwe na hofu kwani mdahalo unaua?
 
Magamba hawatakubali hatakidogo, wewe jiulize wakatae maswali kwenye kampeni zao sembuse mdahalo wa live? najua wanajua mpandikizwa hao ni mbu-mbu-mbu.
 
Unajua Makamba aliruhusu washiriki midahalo baadaye akagundua kichapo ni kikali wakaamua kulala mbele. Ile BAN iliyowekwa na Y. Makamba,nadhani W.Mukama anaweza kui-lift ili vijana wapambane kwa hoja.
Wakilala mbele tena basi itakuwa aibu kubwa sawa na mwanaume kumwogopa mwanaume mwenziye.
 
Acha ukenge ww, uwezo wa mtu kupambanua mambo ni pamoja na uwezo kujieleza na kutoa mikakati thabiti jinsi gani atawasaidia wana Arumeru kujiletea maendeleo.Tunataka kuwapima wakiwa pamoja na pia waulizwe maswali ili tujue ni mgombea gania anayetufaa.Magamba mnaogopa sana hilo sijui kwa sababu hamjui matatizo yetu na uwezo wa kung'amua mambo.
Naona unatoa ratiba ya mdahalo utadhani wewe ndiyo mkurugenzi wa TBC. una tamani lakini hakuna kitu.
 
tbc wenyewe mbaka wapewe kibali na ccm,sio kitu rahisi kama tunavo fikiri.....politics is not wat we think it is!!!
 
Mdahalo ungesaidia sana hebu tuipate hiyo , Nujuavyo mimi hawatakubali mdahalo kwa sababu wataumbuuka mapema
 
Mdahalo wa Nassari na Sioi?!
Magamba hawawezi kukubali itakuwa aibu!
Ni sawa na mdahalo wa Mbowe na Majimarefu/Lusinde/Wasira au Slaa na JK
 
Wana JF,

Nimefuatilia kampeni za ubunge huko jimboni Arumeru mashariki kupitia vyombo vya habari.Kuna madai kuwa uelewa na uwezo wa mgombea wa CCM Bw. Siyoi Sumari juu ya mambo mbalimbali ya kijamii na kisiasa ya jimboni kwake ni mdogo ukilinganisha na ule wa mgombea wa CHADEMA Bw. Joshua Nassari. Ndiyo maana wakati fulani wapiga debe wa CCM waliwahi kumuombea mgombea wao kura za huruma kwa kusema apewe kura za kushinda ili afutwe machozi.

SWALI.

Je, uandaliwe mdahalo utakaorushwa moja kwa moja na TBC baina ya wagombea hawa wawili tarehe 31-03-2012(siku moja kabla ya kupiga kura) ili wana-Arumeru na sisi pia tujiridhishe na madai haya?

Naomba kuwasilisha.

CCM katika uchaguzi ulipita waliwakataza wagombea wake kushiriki midaharo iliyokua ikirushwa na TBC hii inaonyesha kuwa wagombea wengi wa hicho chama hawana uwezo wa kisiasa bali wa kifedha,hivyo huo mdaharo ukitokea litakua ndo kaburi la CCM kwani chama kimesha kufa limebaki jina tu.
 
Back
Top Bottom