Nani wa kuwajibishwa kati ya mwalimu na wizara ya Elimu?

KIMBURU

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
210
189
Nimesikitishwa sana na kauli ya Naibu Wazili wa Elimu kuwa wanafunzi watakaobainika kuwa hawajui kusoma na kuandika na wamefaulu kwenda sekondari, watarudishwa na kisha walimu wa shule walizotoka watawajibishwa.

Pia kuhusu wanafunzi ambao majibu yao yameonekana kufanana sana wamefutiwa matokeo na pia walimu wao watawajibishwa.

Wizara ilitegemea nini kuanzisha mfumo wa majibu ya kuchagua (multiple choice) kwa masomo na maswali yote? Hikujua kuwa mfumo huo unatoa mwanya mkubwa kwa wanafunzi kuigiliziana majibu? na pia haikujua kuwa mfumo huo unawawezesha hata wasiojua kusoma na kuandika kubuni majibu sahihi?

Miaka 50 ya uhuru bado tunaifanyia majiribio Elimu yetu?

Kwa hili naomba Rais KIQUETE awawajibishe watendaji wa wizara hii ambao wameleta mfumo huu usio na mantiki; na sasa wanajikosha kwa kukimbilia kuwaadhibu walimu wasio na makosa.

 
mtawalaumu walimu bure, mchawi ni JK, toka alivyotukana wafanyakazi mke wangu kasema hatofundisha ila benki wa kwanza
 
kama serikali ingekuwa imeweka mitihani ya kutoka darasa moja kwenda lingine kuwa ya muhimu bila shaka ingepunguza tatizo la wanafunzi kumaliza bila kujua kusoma. Nowdays ule mtihani wa darasa la nne uwe umefaulu au no wewe unasonga mbele, sasa hapa wanategemea nini! Dawa ni kuweka mtihani kila unapotaka kwenda darasa lingine lazima ufaulu, hili swala lingepunguza wanafunzi mambumbu na watu wangekuwa serious na elimu.
 
Tatizo siasa imeingilia taaluma,ni kwamba kila mtoto anatakiwa kusoma sekondari,ki taalam si kweli maana wanafunzi wanatofautiana katika uelewa,wapo ambao sekondari kwao ni mzigo tu maana understanding capacity yao ni ndogo saana
 
Back
Top Bottom