nani wa kulaumiwa, wananchi ama serikali?

wlfwilley

Member
Jun 22, 2010
32
2
wakati mwingi tunapopata matatizo tunahangaika kutafuta ni nani wa kumlaumu labda ni serikali ama raia wa nchi kwa kufanya kisicho sahihi mpaka tatizo fulani kutokea. naweza kutoa mifano kadhaa na sisi wanajamii tukazungumzia na kuona ni nani hasa anaistahili lawama husika.

kwanza, janga la mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea sasa, ni kweli kuwa serikali ili tangaza watu wasijenge mabondeni ilia ni serikali hiyo hiyo ilipeleka huduma kama umeme na maji katika maeneo hayo. swali, unaweza kunikataza kufanya jambo filani na wakati huohuo unaniletea ambacho kitafanya maisha yangu kwenda sawasawa katika eneo husika? upande wa pili wa jambo hili ni raia, ni kweli kuwa unakatazwa kuishi sehemu fulani na una hali ngumu ya maisha, ila kuna maeneo yalitolewa kule Vituka, ila kilichotokea ni watu kuuza yale maeneo na kuendelea kuishi mabondeni, baada ya mafuriko unasema serikali hainijali, ni sahihi hii?

pili, kupanda na kushuka kwa bei za mafuta, kumekuwa na kupanda na kushuka kwa bei za mafuta na hii imepelekea wafanya biashara wa bidhaa hii muhimu zaidi katika kipindi hiki cha kukosekana kwa umeme na foleni za ajabu brabarani. swali, kwanini serikali isifufue TPDC na kuhakikisha wafanyabiashara wote wenye kuhutaji wananunua mafuta pale na kusambaza kwa watumiaji? ama kwa wale wanaopenda kuingiza mafuta waingize ila serikali itoe bei kutokana na soko la dunia linavyouza mafuta? kuna haja ya wafanya biashara kugoma na serikali kutoa macho tu na wasijue cha kufanya juu ya wafanyabiashara hawa? unadhani serikali inawaonea wafanyabiashara ama wafanyabiashara wanawaonea raia?

tatu, foleni katika barabara, mtakubaliana na mimi kuwa kumekuwa na foleni za magari katika kiwango kisichoweza kuvumilia kwa kipindi hiki. ukiangalia kwa umakini utaona kuna vitu vingi vinachangia katika hili, barabara mbovu, alama sizoeleweka ama kutokuwepo kabisa, madereva wabovu, daladala, bajaji na pikipiki na sababu nyingine nyingi. ni kweli kwa serikali imeshindwa kutengeneza mfumo ambao utatutoa katika janga hili, ni kweli kuwa raia tunashindwa kufanya jambo juu ya hili?

nne, uchafu uliokithiri katika mzaingira tunayoishi, bila shaka mtakubaliana na mimi kwa wale mliopata fursa ya kutembelea baadhi ya masoko hapa jijini kuwa hayatamanishi kununua bidhaa sema ni vile tupo katika uhitaji na hatuna sehemu ingine ya kupata bidhaa hizo tunshindwa kuacha kununua. pia, ukienda katika mazira tunamoishi, hali ni mbaya, mchukua taka anatoa taka mtaa huu na kwenda kutupa mtaa unaofuata. ni kweli kuwa serikali inashindwa kufanya mpango wa kusababisha hili lisiwe kero tena kama lilivyo sasa? na pia, rahi tunafanya nini juu ya hili? tuna mifano hai na mikoa ambayo imefanikiwa katika hili, tunashindwa hata kuiga?

tuna mambo mengi ambayo serikali imekuwa ikilaumu raia na raia wamekuwa wakilaumu serikali. ila swali moja la mwisho, je serikali hajui ina nguvu kiasi gani katika kufanya yaliyosahihi kufuata mkondo wake, pia raia tuunangoja serikali itufanyie kila kitu, hatuwezi kuanza wenyewe?
 
Wewe ndio wa kwanza kulaumiwa, watu wamepoteza maisha, makazi, mali na miundo mbinu wanahitaji kuendelea na maisha kwanza.
Chakula, matibabu, makazi, ukarabati wa miundombinu na mahitaji muhimu ndio yanayohitajika sasa..
Lawama hazina msaada wowote kwa wahanga kwa wakati huu
 
Back
Top Bottom