Nani si gamba ndani ya ccm?

Dec 11, 2010
3,321
6,328
VITABU vya dini
vinatueleza kisa kimoja
kuwa enzi za utume wa
Isa bin Mariam (Yesu)
watu walikuwa
wakiwapiga mawe hadi
kufa wanawake
wanaobainika kuzini nje
ya utaratibu wa ndoa.
Katika pita pita yake Yesu
aliwakuta watu wakianza
kumpiga mwanamke, na
alipowauliza kwanini
wanafanya hivyo
walimjibu kuwa
mwanamke huyo ni
mzinifu.
Akawaambia yeyote
ambaye anajijua si mzinzi
basi na awe wa kwanza
kumrushia mawe
mwanamke huyo. Hakuna
mtu aliyethubutu kurusha
jiwe, ujumbe ukawa wazi
kwamba hakukuwapo
msafi baina yao bali.
Mfano huu ndiyo
ninaoweza kuutumia kwa
Chama Cha Mapinduzi
(CCM) ambacho hivi sasa
kimebeba ajenda ya
kuvuana magamba
(kuwaondoa watuhumiwa
wa ufisadi) dhana ambayo
inadaiwa haifanywi kwa
dhamira ya dhati.
Leo sina haja ya kujadili
uhalali au uharamu wa
dhana ya kuvuana
magamba ndani ya chama
hicho tawala ila
ninaangalia kuibuka upya
kwa tuhuma za vigogo
kutumia madaraka yao
kutafuna rasilimali za
taifa.
Wiki hii wabunge wa CCM
na wale wa upinzani
wamemtuhumu Makamu
Mwenyekiti (Bara) wa
chama hicho, Pius Msekwa,
kwa kutoa vibali vya
ujenzi wa hoteli za kitalii
katikati ya hifadhi za
Bonde la Ngorongoro.
Kwa mujibu wa wabunge
hao, Msekwa ambaye ni
Mwenyekiti wa Bodi ya
Ngorongoro amekuwa
akifanya hivyo kwa madai
Rais Jakaya Kikwete ndiye
aliyemuagiza aruhusu
uwekezaji huo kwenye
maeneo ambayo
hayastahili kufanya
shughuli za kibinadamu.
Binafsi nilishtushwa na
madai hayo ambayo
kimsingi nilipoyasikia kwa
wabunge wa upinzani
sikushtuka sana
kwasababu nimezoea
kusikia upande huo
ukiibua maovu ya
watawala lakini
nilivyoyasikia yametoka
kwa wabunge wa CCM
nilijawa woga.
Nasema nilijawa woga
kwa sababu kuu mbili,
mosi; Msekwa ni kiongozi
wa juu katika chama
kinachotekeleza
operesheni ya safisha
watuhumiwa wa ufisadi
lakini naye kumbe ni
miongoni mwao.
Pili, sioni kama kweli Rais
Kikwete au kiongozi
yoyote atakuwa na ubavu
wa kumkemea Msekwa
kwa hili alilotuhumiwa
nalo ambalo mpaka sasa
hajakanusha tuhuma hizo.
Hayati Baba wa Taifa,
Julius Nyerere alishawahi
kusema kiongozi ni lazima
aichukie rushwa na hata
akiangaliwa machoni
aonekane kuichukia, awe
na uwezo wa kuwakemea
ndugu, jamaa zake
wanaofanya vitendo
hivyo.
Kwa bahati mbaya
viongozi tulionao hivi sasa
wao na rushwa ni chanda
na pete, waliingia
maradakani kwa kutoa
fedha sasa wanarejesha
kile walichotoa katika
chaguzi bila kujali athari
wanayopata wananchi.
Umejengeka mfumo wa
kulindana ndani ya serikali
na chama tawala,
mtumishi au kiongozi
anabainika kufanya ufisadi
badala ya kufukuzwa kazi
anahamishwa kituo cha
kazi au kupandishwa cheo.
Viongozi wetu
wamegeuka wakoloni,
wameweka mbele maslahi
yao kiasi cha kutusahau
wananchi ambao hatuna
uhakika wa mlo mmoja
kwa siku
Kila kukicha wamekuwa
wakiteuana kwenye bodi,
taasisi na mashirika ya
umma kwa lengo
kutafuna rasilimali zetu na
kuigeuza nchi hii kama
shamba la bibi
Watawala wetu
wamekosa utu, wapo
radhi kushirikiana na
wageni kupora mali zetu
ilmradi wawe
wamehakikishiwa fedha
na wawekezaji.
Katika mazingira haya
nimeanza kupata hisia
kuwa hakuna aliye safi
ndani ya CCM ila tofauti
yao ni kwamba huyu
maovu yake yamebainika
ndiyo maana anaitwa
fisadi, yule ambaye maovu
yake hayajabainika
anaonekana si fisadi.
Leo hii ukiangalia wamiliki
wa ardhi kubwa
zisizoendelezwa ni kina
nani ndiyo utabaini
unyonyaji wa viongozi
wetu ambao umiliki wa
ardhi hizo wameupata
kwa sababu ya vyeo vyao.
Sisemi wasimiliki ardhi,
lakini kuna faida gani ya
kuhodhi maeneo
wasiyoyaendeleza wakati
kuna watu hawawezi
kulima au shughuli za
ufugaji kwa sababu ya
kukosa ardhi?
Tumesikia bungeni
viongozi wastaafu wa CCM
na taifa walivyojichukulia
maeneo katika mkoa wa
Morogoro halafu
wameshindwa
kuyaendeleza.
Ndani ya CCM kuna
magamba mengi lakini
bado hayajulikani maovu
yao, lakini nina hakika
kadiri muda
unavyokwenda ndivyo
tunatavyowabaini
magamba mengine
ambayo yapo mstari wa
mbele kuwashughulikia
wenzao.
Tukianza kufuatilia
mikataba kwenye
kampuni za madini, IPTL,
Kiwira, wizi wa EPA na
mingineo tutabaini
madudu makubwa
yaliyofanywa na wale
tuliowapa madaraka ya
kuongoza.
Njia pekee ya
kuwawajibisha viongozi
hawa ni kuindoa CCM
madarakani kwakuwa
ndiyo iliyojenga mfumo
wa rushwa ya kitaasisi na
kulindana.
Kama CCM kitabaki
madarakani kamwe
hatuwezi kuubomoa
mfumo rushwa na wizi wa
rasilimali za umma maana
hata waje viongozi wasafi
ndani ya chama hicho
hawataweza kupambana
na mfumo ulijengwa kwa
miaka 34.

Chanzo: Tanzaniadaima 21 august 2011.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom