Nani ni chanzo cha ugonvi ktk mapenzi?

mwalimu_salum

Member
Jul 14, 2011
12
2
Mara kwa mara wanaume tumekua tukilaumiwa na wanawake kuwa ni chanzo cha vurugu ktk mapenzi na hata ndoa pia.
Kwa upande mwingine,wanaume tumekua tukiwashutumu wanawake kuwa ndo waanzilishi wa migogoro ktk mahusiano.
Kwa uchunguzi mdogo niloufanya nimegundua kwamba wanaume tulio wengi tunaamin kwamba wanawake ni viumbe watenda maovu tu,kwa hiyo mabaya ambayo mwanaume hulifanya kila siku ni mema(ni sahihi) ila baya moja ambalo mwanamke amelifanya kwa siku moja ni dhambi kubwa sana.
Wana JF naomba mwongozo ktk hili.
 
mh MWalimu, ulivyoulizia chanzo mie ningeingia chaka.................ugomvi wa kimapenzi husababishwa na mambo mengi sana but kwa kuwa umeuliza nani ni mgomvi kati ya mwanamkek na mwanaume ntakwambia tu kuwa inategemea na hulka ya mtu. Kwa maisha ya sasa huwezisema eti wanawake ni wapole kuliko wanaume so wanaume ndo wakorofi. Inategemea na hulka na tabia ya wagombanao
 
Chanzo cha ugomvi ni mabadiliko ya tabia either kwa mwanamke au mwanaume.
 
Ni kweli kaka sisi wanaume tunaona kama wanawake wao kila kitu ni kukosea hata kama wako sahihi kiasi gani, jambo la muhimu ni kukubali kuwa kila mwanadamu hukosea jambo ni kweli wao ni vyombo dhahifu. N i hayo tu jamani.
 
wanawake tumepewa moyo wenye kuhifadhi sana mambo mazito kuliko wanaume, hawawezi kabisa kuhimili mikiki ya aina hii, ila wanawake wanaweza kabisa kuhimili, hivo kwa hali hiyo wote kila mtu kwa nafasi yake anaelewa nani ni mdhaifu zaidi, thats why wanaume kwa wanavotuchukulia, hawategemei tufanye mabaya coz tunajua wao hawawezi himili, ila kwa wao kujua kwamba sie tunaweza himili mikikimikiki, anafanya watakavyo
 
Sishangai kwamba katika uchunguzi wako umekuja na utambuzi kua wanawake ndo chanzo cha ugomvi... Wanaume wanaona kama mwanamke ndo kiumbe mtenda maovu tokana na mila na tamaduni zetu ambazo ziliwaandaa na kuwajengea akilini mwenu na mazingira kua Mwanamke ni mtu wa kufanya kila ambalo wewe mwanaume unataka... Ni lazima atii sheria kwa kuheshimu babu, baba, Mjomba, kaka na mume wake... Lolote atalo ambiwa ni lazima atii maana yeye (mwanaume ndo astahili kusikilizwa)... Hii imejenga tabia ya kwamba mwanaume anapokua ameoa ana expectations ambazo anaamini mwanamke ni lazima azifuate na kwamba ndo msingi wa ndoa....

However tokana na kwamba maisha yamebadilika saana na kwamba kwa kiasi kikubwa wanawake wamejua haki zao (hata zile ambazo hata hastahili) ndo hapo tatizo linapokuja sababu most men hawapo tayari kwa hio "change" na walo tayari wana a line ambayo hataki a cross... Hivo kupelekea a number of most hubbys' watupie lawama kwa wake zao hata makosa ambayo they are responsible wanayageuza....
 
Wote wanaweza kuwa chanzo ila wanaume mmezidi kwakweli, yaani mnataka kila mnachoongea ndo kifuatwe eti kwakuwa tu nyie ni kichwa cha familia!!
 
Labda ugomvi mkubwa na mpenzi wangu ni utarudi saa ngapi? hilo sijui litaisha lini? na sijui nitawahi lini?

Note. bado tuko pamoja sijui ndio niite mikwaruzano na si ugomvi
 
chanzo cha ugomvi ni disrespect....chanzo cha kutoelewana ni ubinadamu
 
Yeyote kati ya wapenzi wawili ananafasi sawa na mwenzie ya kuwa chanzo cha ugomvi katika mapenzi.
 
Hakuna jibu la moja kwa moja, inategemeana na tabia zenu wote wawili, kama mmoja kakulia Manzese na mwingine kakulia Masaki, obviously yule wa Manzese atakuwa ngumi mkononi hata akiwa mwanamke
 
Back
Top Bottom